LATRA tumieni technolojia kudhibiti madereva barabarani kabla ya kuongeza sheria nyingine.

LATRA tumieni technolojia kudhibiti madereva barabarani kabla ya kuongeza sheria nyingine.

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Kama madereva wana uwezo wa kutumia teknolojia ya kidigitali kuhamasishana kugoma nchi nzima kwanini nyinyi LATRA mnashindwa kutumia teknolojia hiyohiyo kuwadhibiti madereva wasifanye makosa barabarani yanaosababisha ajali?. Badala yake bado mnatunga sheria zitakazofanyakazi manually kuwapa madereva adhabu zenye mashaka zenye human errors nyingi.

Uzoefu wangu wa kuendesha vyombo vya moto mjini na kwenda mikoani unaonyesha kuwa kila mkakati wa Latra wa kujaribu kupunguza ajali barabarani unageuka kuwa fursa kwa polisi wa barabarani kujipatia kipato zaidi kuliko hata kuzipunguza ajali zenyewe. Hatimaye mkakati huo unakuwa kitega uchumi kwa matraffic na kero kwa madereva, wamiliki wa magari; kwa wenye mizigo na kwa abiria wanaotumia usafiri huo.

Siku moja usiku mimi na waswahili wenzangu 2 tulikuwa kwenye mgahawa mmoja kule Marekani tunapata kilevi. karibu na meza yetu wakaja wasichana wawili, mmoja akaagiza pombe aina ya Margarita na mwingine akaagiza juice. Pombe iliponikolea kidogo mm nikahamia kwenye meza ya wale dada wenyeji wa kule. Baada ya kuwasalimia swali langu la kwanza la kizushi kwao lilikuwa ni kwanini mwenzio anakunywa juice wewe unakunywa margarita?. Jibu lake lilikuwa fupi sana, akasema leo ni zamu yake kuendesha, mimi itakuwa kesho. Ikawa ooooooh kumbe!!!. Yaani hanywi hata kidogo tu kwani usiku huu atamkamata nani?. Akanishangaa kidogo na kuniuliza, kwani wewe una muda gani hapa? Nikamwambia nipo muda tu lakini siendeshi gari hivyo sijui chochote kuhusu magari na udereva hapa. Akasema barabara zetu zimefungwa kamara na vipima pombe (alcohol detectors) kila baada ya umbali kadhaa, hivyo kama ukiendesha vibaya watakuona na kama umekunywa watajua pia na bill yako utaikuta huko mbele na lazima utailipa kutokana na aina ya kosa. Na kuna wakati unaweza kusimamishwa kuendesha au kufungiwa kwa muda fulani au milele. Nikatikisa kichwa na kuendelea na mambo mengine lakini nikwa nimepanuka akili kwa kiasi fulani kwa kuhamia meza ile kuliko kama ningebaki na waswahili wenzangu tusiokuwa na magari kule.

Nikajiuliza maswali mengi kuwa hivi viongozi wetu wa Tz na Afrika hawaendi ulaya na marekani kila siku? Hivi LATRA hawajui kama kuna kamera za barabarani ambazo zinaweza kufungwa japo kwenye taa nyekundu, vivuko vya waenda kwa miguu, madaraja, kona kali na sehemu nyingine muhimu kwa usalama wa barabarani ili kupunguza ajali na matraffic wengi barabarani? Kwani kufunga vifaa vya kupima kiwango cha pombe kwa madereva barabarani ni bei gani? Kwanini hawafungi? Kwanini hawaanzi na barabara chache na maeneo hatarishi tu kwanza?

LATRA wana weledi kiasi gani au wanasubiri amri kutoka juu?

Kwanini serikali lazima igombane kwanza na raia ili kufanikisha jambo ambalo wangeweza kulifanikisha bila ugomvi? Sasa hivi ugomvi ni kuwatoa machinga mitaani, kumbe wangeweza kuuepuka ugomvi nao kama wangeupanga mji kuonyesha wapi kuna nafasi na wapi kumejaa, wapi panastahili kufanyia biashara na wapi biashara ni mwiko kabisa kuonekana. Vijana wangejipanga wenyewe hadi wengine wangeamua kubaki hukohuko kijijini kwao maana Dar es Salaam nafasi za biashara zimejaa.
 
Kwamba hawajui kuna hy tech?
Nop hapo ni makusudi ili kutengeneza mazingira ya kupiga noti
 
Kwamba hawajui kuna hy tech?
Nop hapo ni makusudi ili kutengeneza mazingira ya kupiga noti
Kama wenzetu wana mfumo ambao unamlazimisha dereva anywe soda tu siku hiyo kwanini tusiulete hapa hata kwa gharama ya sisi kula hata manyasi ikibidi ili tuokoe ajali, majeruhi na vifo kwa watu wetu? Mfumo ambao unamnyang'anya dereva leseni yake kihalali kabisa bila ya yeye kubisha. Mfumo ambao unakupi faini kihalali kabisa bila wewe kulalamika badala yake unajilaumu mwenyewe.

Ni kweli traffic ni kero ya kupitiliza japo kugoma kama vile bila kutoa notice kwa abiria na wote wanaotarajia kusafiri na kusafirisha sio sawa na sahihi.
 
Back
Top Bottom