LATRA yaruhusu Mabasi ya Dar - Mtwara yapite Barabara ya Songea, Makambako, Iringa kwa dharura

LATRA yaruhusu Mabasi ya Dar - Mtwara yapite Barabara ya Songea, Makambako, Iringa kwa dharura

TAREHE 6 MAY 2024

KATAVI RUKWA

BARABARA YAFUNGULIWA / DARAJA LILIJAA MAJI SIKU 18 / GARI ZAANZA KUPITA KATAVI -RUKWA


View: https://m.youtube.com/watch?v=dYQ92KKd69I
Barabara ya Sitalike kuelekea Rukwa imefunguliwa baada ya kufanyiwa ukaguzi na kukarabatiwa.

Meneja wa wakala wa barabara TANROADS mkoa wa Katavi mhandisi Martin Mwakabende amesema daraja lililokua limefungwa kwa takribani wiki mbili sasa imefunguliwa ikiwa ni tayari kuendelea na matumizi yake.

Barabara hiyo ilifungwa na mkuu wa mkoa wa Katavi Bi. Mwanamvua Mrindoko baada ya daraja la Sitalike lililoko halimashauri ya Nsimbo mkoani humo ambayo inaelekea mkoani Rukwa kujaa maji ambayo yalisababishwa na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha.

Aidha Mhandisi Mwakabende amesema serikali kupitia rais wa jamhuri ya muungano Dr Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya bilioni moja kukarabati barabara zote zilizoharibiwa na mafuriko
1715213227895.png
 
Huko Rukwa Katavi wataua watu kwa aina ya daraja hapo juu Barabara ya Sitalike kuelekea Rukwa


TOKA MAKTABA :
15 April 2024

View: https://m.youtube.com/watch?v=0EG6XRwmGh0
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amesitisha huduma za usafiri kupitia barabara ya Sitalike Kuelekea KIZI iliyoko mkoani Rukwa na badala yake watumie barabra ya kupitia Kibaoni huku akisisitiza usalama katika maeneo yote yenye changamoto ya kuharibika kwa miundombinu ya barabara inayosababishwa na mvua kubwa inayoendelea.Aidha Mrindoko amepiga marufuku kwa yeyote atakayelazimisha kupita kwenye mto uliojaa mara baada ya mvua kunyesha na kuleta mafuriko amesisitiza hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
 
Back
Top Bottom