LATRA yavunja rekodi ongezeko la nauli, wananchi wataharuki, patashika kwenye madaladala, Viongozi wakaa kimya

Siyo kweli. Taarifa za ongezeko la nauli zilitolewa na kuandikwa kila mahali lkn watanzania kama kawaida yao walikuwa bize na habari za ngono, umbea na Simba na Yanga.

Pambaafu kabisa!!
Simba, yanga, singeli, vigodoro, ngono, kwa mparange, fumanizi, tamthilia na uchawa ndizo habari zinapata Wateja![emoji1787]Watanzania ni biumbe special.
 
Mkuu uwezo wako wa kufikiri na wananchi unaowatetea upo chini sana.
Kwanza Latra wametangaza sana ongezeko la nauli.Kabla ya ongezeko waliitisha mkutano wa maoni na ulifanyika na maoni yalitolewa kwa uwazi.Pili kiwango kilichoombwa na wawekezaji Latra wamepunguza sana kwa kuwatete hao wanaoitwa wananchi.Tatu Serikali haimiliki mabasi,mabasi yanamilikiwa na wawekezaji ambao hawapati ruzuku.Wawekezaji wanatafuta mitaji yao na wanawekeza hili wapate faida.
Waambie hao unaowaita wananchi waibane Serikali iwekeze kwenye usafiri wa umma.Binafsi nailamu Latra kwa kuwakandamiza wawekezaji na kuwabeba wananchi.
 
Faraja ya nn unataka serikali imetangaza sisi tupo bize nakufuatilia mpira kati ya simba na yanga nani atavuka acha watu nyooshe mpaka tubaki mifupa ndio akili itarudi
 
Hichi ndicho nachoshangaa pia. LATRA wanasema eti kuna makampuni sijui mawili yamelalamika. Ni wazi kuna mchezo mchafu (rushwa) umetumika
 
Ukweli uko wazi kwamba vigogo wengi serikalini now wameagiza mabasi iwe kupitia majina Yao halisi au ya wengine na ndio kichocheo Cha nauli kupanda. Mama Samia basi tu acha aendelee kukaa kimya. Hawa watu ndomana magu aliwadhibiti mno! Waandishi wetu nao Wana ukiande Fulani hivi. Wakat huyo mkurugenz wa LATRA anasema sababu za kupanda ni gharama za uendeshaji wangeuliza tu mafuta yakishuka na spea kupungua beo je watashusha nauli? Kama sio uhuni wao tu
 
Watu wanalaumu tu ila hawajui namna wafanyabiashara ya usafirishaji wanapata hasara kwa kupanda kwa bei ya mafuta.
Watu mpaka wamepaki yale magari yanayokula mafuta sana na wengine wanaahirisha safari wasipojaza gari ili tu kuepuka hasara yote sababu ya kupanda kwa bei ya mafuta.
Sasa tunataka wafanya biashara wabebe gharama za kupanda kwa mafuta?
What is way forward wakati bei za mafuta zimepanda na gharama za uendeshaji zimeongezeka?
Nani abebe hii gharama?
 
Toka Toka lini ulionao bei ya mafuta imeshuka Kama si juzi wakati wa korona baada ya viwanda kusitisha uzalishaji?
Ndio bei ya mafuta ikishuka wanaweza kushusha bei za nauli.
Hivi ubajua hizi bei za nauli ni za lini na toka zimewekwa mafuta yanepanda kwa kiasi gani?
 
Mimi naamini kabisa CCM haipo tena nchi hii,ila Kuna Lindi linajiita CCM.
Ccm ipo ndugu yangu kupitia kwenye mpira wewe ngoja siku waseme mpira marufuku halafu huone kitakachotokea na wao wana amini watanzania hawana shida kupitia mpira huo huo ndio maana mkilalamika wanawaona wazushi ebu fikiria watu wanaojazana kwa mkapa simba ikicheza au yanga umati unaojazana pale kwa mkapa halafu umuaminishe kiongozi gani wa serikali kwamba watanzania wanaishi maisha magumu hawana hela hata wewe usinge amini wata amini endapo itacheza simba au yanga kwa mkapa halafu hakuna hata mtu mmoja wa hali ya chini aliyekwenda kwa mkapa hapo ndio wata amini kweli hali ngumu lakini kwa hali hilivyo sasa hawawezi kuamini ndio maana wanapandisha vitu hovyo wakijua watanzania hawana shida hila ni watu waliozoea kulalamika na washatuzoe wanajua kabisa hawa watalalamika mwisho watanyamaza huo ndio ukweli
 
Suku zote mateso yakizidi uoga wa kifo huondoka.
Tusubiri yanakuja.
 
Shinda yenu Watanganyika mnajua sana kulalama ila kuchukua hatua ndio kimbembe. Ata viongozi wenu wameisha wajua na ndio maana wanawageuza wanavyo taka wao na wako kimya tu. Maana wanajua mtapinga nduru tu kisha mtasahau na maisha yataendelea.

Amkeni nyie mazombi ipiganieni haki yenu, haki yenu haiwezi patika kwenye foleni ya masanduku.
 
Mkuu weka "figures" ili tuone nauli zimepanda kwa kiasi gani ili tuweze kufanya tathimini kupitia ongezeko la bei ya mafuta. Tukumbuke kuwa ijapokuwa wananchi wanaumia lakini wamiliki wa mabasi nao pia ni wawekezaji, na hutaka kuendesha biashara zao kwa faida.

Kitu ambacho serikali inaweza kukifanya ni kuweka ruzuku ili pande zote zisiweze kuumia. Lakini wanachi wanayo silaha moja kubwa ya kuitumia, nayo si nyingine bali kutumia turufu ya kura zao na kuzilinda kwa hali na mali ili kutoa fundisho, endapo wanaona serikali yao inawachukulia kimchezo mchezo.
 
Ongezea na matamasha ya fiesta wasafi watu wanajazana
Sahv watu wanajazana misomisondo
Serikali wakiona hvyo wanajuwa maisha burdann[emoji41]

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…