Law School kufumbia macho tuhuma zinazowakabili haikubaliki

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kumekuwa na tuhuma mbaya sana kuihusu LST na kwa muda mrefu.

Hii ni taasisi ya umma na yeyote afanyaye kazi pale ni dhamana tu.

Kwa mahitaji ya ufafanuzi tuhuma hizi ziliorodheshwa kwenye uzi huu hapa chini:

Dokezo - Tuhuma za Siasa chafu "Law School of Tanzania" wahusika wajitokeze kuzijibu

Zaidi ya masaa 36 yamepita LST wako kimya.

Kwa hakika wazazi na walezi wa wanafunzi hawa tuko katika sintofahamu isiyo kifani.

Ni vipi taasisi ya umma inaweza kunyamaza kimya kukiwa na tuhuma mbaya kama hizo kuihusu?

Uko wapi usalama wa wana na binti zetu katika chuo hiki?

Iko wapi thamani ya pesa zetu tunazozipata kwa taabu kuwapeleka vijana wetu shule kwa kujinyima kwa ajili ya maisha yao ya baadaye na faida ya taifa kwa ujumla?

Kama LST haitoi ufafanuzi wa kuridhisha kuhusiana na hili, kuna umuhimu gani wa kuwa na chuo hiki kama taasisi ya umma?

Ni vipi watu hawa wakaendelea na shughuli zao yaani business as usual katika misingi ya tuhuma nzito hizi?

Post #2 na #3 chini ni kwa hisani ya wadau Aikambee na MALCOM LUMUMBA mtawalia zenye kuakisi vilivyo hali halisi ilivyo LST Leo. Wakuu, heshima kwenu.

Pia uzi huu unahusika:

Siasa zimezidi The Law School of Tanzania. Hiki chuo kimulikwe!

NInakazia: Kwenye hili LST hawawezi kuwa na option ya kunyamaza.
 
Kwa hisani ya mdau aikambe:

Anaandika mdau:

Nimeona mada za kuchambua taarifa ya kufeli kwa wanafunzi Law School of Tanzania.

Binafsi na mimi nimepitia Law School, na haya ndiyo ninayoyafahamu kuhusiana na hiki chuo.

1. Law School kiuhalisia, siyo sehemu ya mafunzo kwa vitendo kama mnavyosikia redioni.

2. Somo la field lipo, ila marks zake hazihusiki kwenye kubaini ufaulu. Yaani alama za somo la field hazina maana kwenye GPA calculation maana hazitambuliki.

3. Wanafunzi wa Law School hufundishwa kwa nadharia darasani, na kuingia semina kama ilivyo vyuo vikuu.

4. Mwalimu mmoja hutoa mhadhara kwa wanafunzi wote 600+ na akimaliza anaingia mwingine hadi siku inaisha.

5. Mada zinazofundishwa Law School ni zilezile mwanafunzi alifundishwa vyuoni ngazi ya degree na hakuna tofauti.

6. Muda wa mitihani haupo fair. Kwenye mtihani mmoja, kunakuwa na maswali ya kuandaa hati za mashtaka na madai nyingi mno kiasi kwamba muda wa kuandaa hati hizo hautoshi. Kwa wasijua, hati za kisheria uandaaji wake unahitaji kurejea vifungu vya sheria mbalimbali ambazo unakuwa unazo mezani(Acts).

7. Wahadhiri wa Law School huamini kwamba wanafunzi wao watafeli na mtu akifaulu wanashangaa sana. Yaani wapo kama miungu watu. Pale Law School hata secretary anamdharau mwanafunzi na anataka umuinamie kumsujudu.

8. Mahakimu, na waajiriwa wengine wenye uzoefu kwenye sheria wakienda kujiendeleza Law School nao hufeli pia.

9. Kuna wakati mahakimu walishauriwa wasijiendeleze Law School maana ni fedhea hakimu mzoefu unafeli Law School. Badala yake waliaambiwa watapewa utambulisho maalum kwamba wamefuzu vigezo vya sheria kwa vitendo.

10. Suplementary yaani mitihani ya kurudia haina kikomo Law School. Unaweza hata ukakaa na sup. hata miaka 40.

11. Law School ukikata rufaa ya matokeo haipatiwi majibu na unaweza ukaanza apya kusoma na kumaliza bila kupata majibu ya rufaa.

12. Law School unasoma masomo yote uliyofundishwa kwenye shahada ya sheria kwa miaka minne, lakini ukifika Law School unafundishwa kwa miezi 6 na unapewa mitihani. Halafu miezi mingine 6 unaenda field.
 
Kwa hisani ya mkuu MALCOM LUMUMBA:

Anaandika mdau:

Binafsi naomba nisema yafuatayo kuhusu shule ya sheria Tanzania:

Mosi, kutokana na uhitaji wa elimu ya kusoma kwa vitendo (Post-Graduate Diploma in Legal Practice) haikutakiwa kuwe na shule moja nchi nzima tena ambayo iko kwenye mji kama Dar es salaam. Walau hizi shule zingekuwepo kikanda ili kuwaepusha na kadhia wale wanafunzi wanaotoka mikoa ya mbali kuja kurudia mitihani Dar es Salaam. Mtoto anasafiri kutoka Tarime, hana hata mkopo halafu anakuja Dar es salaam kufanya mtihani akiwa na 50/50 kwamba hilo somo analorirudia atafuaulu au lah.

Pili, mbinu ya kumpima mwanafunzi (Mode of Assessment) siyo rafiki kabisa na haizingatia utaalamu wa kisaikolojia kwamba wanafunzi wana uelewa tofauti. Mtoto anasoma mwaka mzima halafu anapewa mitihani 24 ndani ya mwaka ambayo kama akifeli hata mmoja basi anaweza kupoteza zaidi hata ya miaka 2 anarudia tu kozi hiyo hiyo. Kikawaida tulitegemea kwenye elimu ya vitendo wanafunzi wapimwe kupitia kazi nyingine muhimu ambazo lazima ziwe na alama, kama PRESENTATIONS, GROUP ASSIGNMENTS, CLINICS + WORKSHOPS and INTERNSHIP WITH MARKS.

Sasa wanaitwa DIPLOMA IN LEGAL PRACTICE huku wakichukua ada ya zaidi ya milioni moja, ilhali vipimo vyote vinatolewa kupitia mitihani. Hii siyo sahihi, kwasababu hata mahakamani kwenyewe wanasheria huwa hatuviziani ila tunapewa muda wa kujiandaa. Sasa mtoto anakaa INTERNSHIP miezi zaidi ya sita huku akija kukaguliwa kihunihuni tu mara moja, bila kupewa alama yoyote ile ya muhimu. Kwanini hawa wanafunzi wasipangiwe hata miezi miwili-miwili kufanya kazi la lazima zenye alamu mahakama za mwanza, mabaraza ya ardhi, mabalaza ya usuluhishi, dawati la jinsia ???

Jingine, ambalo nimeliona ni jambo la kipumbavu kufanywa na watu wanaojiita wasomi ni kitendo cha kutoa matokeo ya mitihani yote ya mwaka mzima ndani ya siku moja, baada ya mwaka mzima na miezi mitatu kupita. Kwanini matokeo ya ICA (Individual Continous Assessment), WPE (WRITTEN PRACTICAL EXAMINATION) na FINALS NON-CORE hayatolewi mapema, ili mwanafunzi ajue mbivu na mbichi na aweze kujipanga vizuri kwenye mitihani ya mwisho ??? Pia wawekewe utaratibu maalamu kabisa wa kuyarudia haya masomo wakati hata wako shule, hasa wiki moja baada ya kumaliza WPE ???

Lingine muhimu ni kwamba LST, kuna mitihani ya WPE (Written Practical Examination) ambayo kwingineko duniani mwanafunzi huifanya kwa kufanya tafiti pamoja na majadiliano na wanafunzi wenzake, kisha baadae huenda kufanya huo mtihani. Ilhali sasa pale LST, wanafunzi wanafungiwa masaa manne (4) wakisoma mavitabu, bila kuruhusiwa kuzungumza halafu wanapewa saa moja kupumzika, ili warudi kufanya mtihani huohuo kwa masaa matatu. (It's just emotional debilitating)

Tatu, hili la kulazimisha kila anayesoma sheria awe wakili nadhani ni jambo la kishenzi ambalo lilifanywa kwa mihemko bila kufikiriwa. Miaka yote huko nyuma watu tuliajiriwa kama STATE ATTORNEYS bila hata kuwa wanasheria. Tulitakiwa tu tufanye INTERNSHIP miezi tisa kwa ATTORNEY GENERAL halafu tunaenda kufanya BAR-EXAMINATION kule Arusha. Kinachoshangaza ni kwamba wengi ambao hawakupita Law School wako vizuri kuliko hata hawa watoto wenu wa Mawasiliano nyuma kule.

Kubwa zaidi, wanasheria tuko kwenye nyanja kuu mbili ambazo ni LEGAL PRACTITIONER (ADVOCATES) na JURIST (LEGAL SCHOLARS/LEGAL RESEARCHERS). Hawa ni watu wawili tofauti na wanafanya kazi tofauti kabisa, sasa ukitaka kuwalazimisha wawe kitu kimoja utakuwa unapuyanga mno. Leo hii ushauri wa sheria wa JURIST unaweza kuwa una uzito kuliko hata ORDINARY LEGAL PRACTITIONER, kutokana na tafiti na ufahamu. Sasa kwenye nchi fulani ya kusadikika, wenyewe kwasababu hawana SPECIALIZATION basi wanalazimisha kila mtu awe wakili, kwamba hata JURIST haweza kutoa ushauri kama hana muhuri. Just Lackadaissical and Nonsensical....

Nne, mtaala wa shule ya sheria ni wa kizamani sana na hauwezi kumfanya mwanafunzi awe vizuri kwenye soko la kimataifa. Kuna baadhi ya masomo tulitegemea yafundishwe pale LST, lakini hayapo kwenye mtaala. Mfano, INTERNATIONAL COMMERCIAL ARBITRATION, INVESTMENT LAW, BASICS OF INTERNATIONAL ECONOMICS LAW/ INTERNATIONAL TRADE AND FINANCE LAW. Nchi haina wataalamu wa haya masomo, sisi tunakomaa kufundisha PROPABATE & ADMINISTRATION OF ESTATES, COMMERCIAL LAW, LEGAL ETHICS, HUMAN RIGHTS and ACCOUNTS FOR LAWYERS masomo ambayo vyuo vingi vinayafundisha na vinaweza kuyafundisha vizuri.

Kesi kubwa kama zila za makinikia, DOWANS, ESCROW n.k zinahitaji mwanasheria walau awe anajua masomo ya INTERNATIONAL COMMERCIAL ARBITRATION, ambapo anatakiwa aifahamu mikataba mikubwa BIT (Bilateral Investment Treaties), pamoja na taasisi muhumu kama ICSID, PIC, ICC. Lakini sisi tunakomaa kuwafelisha watoto masomo kama ACCOUNTS. Sijui hii nchi haina watu wenye akili kabisa. Mambo ya ajabu yanafanyika na hakuna hata anayestuka.

Tano, mradi wa LST tangu mwaka 2006 marehemu Prof. Mukoyogo aliupinga kweli kwasababu aliona hauna maana zaidi ya kuwatengenezea ulaji baadhi ya wataalamu wa pale University of Dar es Salaam. Hivi kweli, tuna uhakika kwamba haya masomo ya LST hayawezi kufundishwa vizuri kwenye vyuo ambavyo wanafunzi wanasoma wakiwa wanatafuta Shahada ya kwanza kweli ???

Jambo jingine ni kwamba wataalamu wengi wa pale LST wameamua kufanya biashara ya vitabu. Wanatunga mitihani ambayo majibu yake utayapata kama tu umenunua vitabu vyao. Hili nilishawahi kuambiwa nikathibitisha mwenyewe kwenye baadhi ya vitabu. Hii ni tabia ya kishezi ambayo inaumiza na kukwamisha wengine huku wengine wakipata ukwasi mkubwa. Mwanafunzi anataoa pesa nyingi za Ada lakini hivyo vitabu havipo maktaba, utavipata mpaka umfuate mwandishi mwenyewe na umlipe 50,000. Kwanini msiweke vitabu vingi kule maktaba wanafunzi wakavisoma ???

Sita, hivi inawezekanaje mwanafunzi ambaye amefauli vizuri shahada yake afeli vibaya kwa kiwango cha DISCONTINUE pale LST ??? Ina maana huyu mwanafunzi hafahamu kitu chochote kabisa ??? Lakini, kubwa zaidi ni hili la wanafunzi 600 kuanza pamoja, lakini wanaofaulu ni watu 30, huku nusu ingine ikiwa inafanya SUPPLEMENTARY au DISCONTINUED. Sijui kwanini hili haliwastui Majaji na Wizara. Watu hufeli, lakini siyo kwa kiwango hicho ambacho kinafanyika pale Law School.

Pia, pale pana rushwa sana ya ngono, kukomoana na kubadilishiana matokeo. Kuna jamaa niliwahi kuwa naye mahakamani aliwahi niambia kwamba kuna rafiki zake wanafundisha pale walimuahidi kwamba watamfaulisha, na kweli alifauri vizuri hadi tukashangaa. Alikuwa na maswali hata kabla mitihani haijaanza. Nikasema HIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII...

TANZANIA HAKUNA KITU KINACHOFANYA KAZI VIZURI KUSEMA TUNAWEZA JIVUNIA
 
Huu mjadala ushakuwa wa Kitaifa , sijui kwanini hawajitokezi

Wasipojitokeza tunao wajibu wa kuwalazimisha kujitokeza.

"Si nadra kwa viongozi wasiojitambua kama hawa kuzuiliwa kuingia maofisini, ofisi zao kubadilishwa au kuongezwa makomeo mengine au hata wanafunzi kusitisha ushirikiano wote nao.

Hawana namna. Kuwataka ufafanuzi mbona ilikuwa ni courtesy ya kiutu uzina mno?
 
Hongereni sana LST mnafanya kazi nzuri.

Ongezeni jitihada.

Tupo nyuma yenu.
 
Hongereni sana LST mnafanya kazi nzuri.

Ongezeni jitihada.

Tupo nyuma yenu.

Kuna tuhuma mbaya zinawahusu. Jibu(ni) tuhuma. Bila majibu, mengine yote ni kelele za chura tu.
 
Chadema tusaidie kulisemea hili. Nyie ndiyo sauti ya wanyonge. Unaweza kuiona kama vie Chadema inaingiza siasa kwenye elimu, lakini hapana, hakuna fairness katika kutunga mitihani. haya hao walimu wa Law shool naye ukimpa hiyo mitihani anayompa mwanafunzi kwa limited time kama ile hawezi kuipass! Wassaidieni wazazi.
 
Mmeliwa vichwa mnaanza kulia lia,

Kasapueni, matokeo hayatabadilika.

Hongera LST kwa kuwafyeka hao mavilaza.
 
Unapoteza muda wako...
Ulianza na Panyaroad ukapuuzwa sasa umekuja na LST kisa wajinga wenzako wamefeli
 
Kwa hisani ya mdau aikambe:

Anaandika mdau:

Nimeona mada za kuchambua taarifa ya kufeli kwa wanafunzi Law School of Tanzania.

Binafsi na mimi nimepitia Law School, na haya ndiyo ninayoyafahamu kuhusiana na hiki chuo.

1. Law School kiuhalisia, siyo sehemu ya mafunzo kwa vitendo kama mnavyosikia redioni.

2. Somo la field lipo, ila marks zake hazihusiki kwenye kubaini ufaulu. Yaani alama za somo la field hazina maana kwenye GPA calculation maana hazitambuliki.

3. Wanafunzi wa Law School hufundishwa kwa nadharia darasani, na kuingia semina kama ilivyo vyuo vikuu.

4. Mwalimu mmoja hutoa mhadhara kwa wanafunzi wote 600+ na akimaliza anaingia mwingine hadi siku inaisha.

5. Mada zinazofundishwa Law School ni zilezile mwanafunzi alifundishwa vyuoni ngazi ya degree na hakuna tofauti.

6. Muda wa mitihani haupo fair. Kwenye mtihani mmoja, kunakuwa na maswali ya kuandaa hati za mashtaka na madai nyingi mno kiasi kwamba muda wa kuandaa hati hizo hautoshi. Kwa wasijua, hati za kisheria uandaaji wake unahitaji kurejea vifungu vya sheria mbalimbali ambazo unakuwa unazo mezani(Acts).

7. Wahadhiri wa Law School huamini kwamba wanafunzi wao watafeli na mtu akifaulu wanashangaa sana. Yaani wapo kama miungu watu. Pale Law School hata secretary anamdharau mwanafunzi na anataka umuinamie kumsujudu.

8. Mahakimu, na waajiriwa wengine wenye uzoefu kwenye sheria wakienda kujiendeleza Law School nao hufeli pia.

9. Kuna wakati mahakimu walishauriwa wasijiendeleze Law School maana ni fedhea hakimu mzoefu unafeli Law School. Badala yake waliaambiwa watapewa utambulisho maalum kwamba wamefuzu vigezo vya sheria kwa vitendo.

10. Suplementary yaani mitihani ya kurudia haina kikomo Law School. Unaweza hata ukakaa na sup. hata miaka 40.

11. Law School ukikata rufaa ya matokeo haipatiwi majibu na unaweza ukaanza apya kusoma na kumaliza bila kupata majibu ya rufaa.

12. Law School unasoma masomo yote uliyofundishwa kwenye shahada ya sheria kwa miaka minne, lakini ukifika Law School unafundishwa kwa miezi 6 na unapewa mitihani. Halafu miezi mingine 6 unaenda field.

Kwakweli miafrika sisi ni mijitu ya hovyo sana.
Hiyo yote wanafanya kukomoa watu tu
 
Hicho kizazi cha School of Law kilichozinduka ndio mawakili watakao ikomboa nchi hii.
Bravo Mawakili watarajiwa!
Komaeni
 
Huu uzi umeshiba nondo, inahitaji kuwa makini unachosema.

My take on hili, i think ni wakati muafaka kungekua na transparency ya jinsi haya mambo yanavofanyika maana hata huku mtaani hua hatuelewi hawa jamaa wana deal vipi.

Sijui, lakini maybe wanajitahd kupunguza mrundikano wa wataalam wa sheria ili watu waendelee kupiga noti kimyakimya, maana scarcity ikiwa kubwa tgen rates zitakua juu.
 
Kama mwaka huu wamevunja rekodi, wanafunzi 26 Kati ya 600 wamefaulu.

Mkuu hata cohort ya 31 walifaulu 28 tu kati ya wote kama hivyo hivyo.

Muda wa kuchukua hatua ni sasa.

Penye nia Pana njia.

Yanayotokea LST na kwingine kote yafansnayo na haya hayakubaliki.
 
Kwa hisani ya mkuu MALCOM LUMUMBA:

Anaandika mdau:

Binafsi naomba nisema yafuatayo kuhusu shule ya sheria Tanzania:

Mosi, kutokana na uhitaji wa elimu ya kusoma kwa vitendo (Post-Graduate Diploma in Legal Practice) haikutakiwa kuwe na shule moja nchi nzima tena ambayo iko kwenye mji kama Dar es salaam. Walau hizi shule zingekuwepo kikanda ili kuwaepusha na kadhia wale wanafunzi wanaotoka mikoa ya mbali kuja kurudia mitihani Dar es Salaam. Mtoto anasafiri kutoka Tarime, hana hata mkopo halafu anakuja Dar es salaam kufanya mtihani akiwa na 50/50 kwamba hilo somo analorirudia atafuaulu au lah.

Pili, mbinu ya kumpima mwanafunzi (Mode of Assessment) siyo rafiki kabisa na haizingatia utaalamu wa kisaikolojia kwamba wanafunzi wana uelewa tofauti. Mtoto anasoma mwaka mzima halafu anapewa mitihani 24 ndani ya mwaka ambayo kama akifeli hata mmoja basi anaweza kupoteza zaidi hata ya miaka 2 anarudia tu kozi hiyo hiyo. Kikawaida tulitegemea kwenye elimu ya vitendo wanafunzi wapimwe kupitia kazi nyingine muhimu ambazo lazima ziwe na alama, kama PRESENTATIONS, GROUP ASSIGNMENTS, CLINICS + WORKSHOPS and INTERNSHIP WITH MARKS.

Sasa wanaitwa DIPLOMA IN LEGAL PRACTICE huku wakichukua ada ya zaidi ya milioni moja, ilhali vipimo vyote vinatolewa kupitia mitihani. Hii siyo sahihi, kwasababu hata mahakamani kwenyewe wanasheria huwa hatuviziani ila tunapewa muda wa kujiandaa. Sasa mtoto anakaa INTERNSHIP miezi zaidi ya sita huku akija kukaguliwa kihunihuni tu mara moja, bila kupewa alama yoyote ile ya muhimu. Kwanini hawa wanafunzi wasipangiwe hata miezi miwili-miwili kufanya kazi la lazima zenye alamu mahakama za mwanza, mabaraza ya ardhi, mabalaza ya usuluhishi, dawati la jinsia ???

Jingine, ambalo nimeliona ni jambo la kipumbavu kufanywa na watu wanaojiita wasomi ni kitendo cha kutoa matokeo ya mitihani yote ya mwaka mzima ndani ya siku moja, baada ya mwaka mzima na miezi mitatu kupita. Kwanini matokeo ya ICA (Individual Continous Assessment), WPE (WRITTEN PRACTICAL EXAMINATION) na FINALS NON-CORE hayatolewi mapema, ili mwanafunzi ajue mbivu na mbichi na aweze kujipanga vizuri kwenye mitihani ya mwisho ??? Pia wawekewe utaratibu maalamu kabisa wa kuyarudia haya masomo wakati hata wako shule, hasa wiki moja baada ya kumaliza WPE ???

Lingine muhimu ni kwamba LST, kuna mitihani ya WPE (Written Practical Examination) ambayo kwingineko duniani mwanafunzi huifanya kwa kufanya tafiti pamoja na majadiliano na wanafunzi wenzake, kisha baadae huenda kufanya huo mtihani. Ilhali sasa pale LST, wanafunzi wanafungiwa masaa manne (4) wakisoma mavitabu, bila kuruhusiwa kuzungumza halafu wanapewa saa moja kupumzika, ili warudi kufanya mtihani huohuo kwa masaa matatu. (It's just emotional debilitating)

Tatu, hili la kulazimisha kila anayesoma sheria awe wakili nadhani ni jambo la kishenzi ambalo lilifanywa kwa mihemko bila kufikiriwa. Miaka yote huko nyuma watu tuliajiriwa kama STATE ATTORNEYS bila hata kuwa wanasheria. Tulitakiwa tu tufanye INTERNSHIP miezi tisa kwa ATTORNEY GENERAL halafu tunaenda kufanya BAR-EXAMINATION kule Arusha. Kinachoshangaza ni kwamba wengi ambao hawakupita Law School wako vizuri kuliko hata hawa watoto wenu wa Mawasiliano nyuma kule.

Kubwa zaidi, wanasheria tuko kwenye nyanja kuu mbili ambazo ni LEGAL PRACTITIONER (ADVOCATES) na JURIST (LEGAL SCHOLARS/LEGAL RESEARCHERS). Hawa ni watu wawili tofauti na wanafanya kazi tofauti kabisa, sasa ukitaka kuwalazimisha wawe kitu kimoja utakuwa unapuyanga mno. Leo hii ushauri wa sheria wa JURIST unaweza kuwa una uzito kuliko hata ORDINARY LEGAL PRACTITIONER, kutokana na tafiti na ufahamu. Sasa kwenye nchi fulani ya kusadikika, wenyewe kwasababu hawana SPECIALIZATION basi wanalazimisha kila mtu awe wakili, kwamba hata JURIST haweza kutoa ushauri kama hana muhuri. Just Lackadaissical and Nonsensical....

Nne, mtaala wa shule ya sheria ni wa kizamani sana na hauwezi kumfanya mwanafunzi awe vizuri kwenye soko la kimataifa. Kuna baadhi ya masomo tulitegemea yafundishwe pale LST, lakini hayapo kwenye mtaala. Mfano, INTERNATIONAL COMMERCIAL ARBITRATION, INVESTMENT LAW, BASICS OF INTERNATIONAL ECONOMICS LAW/ INTERNATIONAL TRADE AND FINANCE LAW. Nchi haina wataalamu wa haya masomo, sisi tunakomaa kufundisha PROPABATE & ADMINISTRATION OF ESTATES, COMMERCIAL LAW, LEGAL ETHICS, HUMAN RIGHTS and ACCOUNTS FOR LAWYERS masomo ambayo vyuo vingi vinayafundisha na vinaweza kuyafundisha vizuri.

Kesi kubwa kama zila za makinikia, DOWANS, ESCROW n.k zinahitaji mwanasheria walau awe anajua masomo ya INTERNATIONAL COMMERCIAL ARBITRATION, ambapo anatakiwa aifahamu mikataba mikubwa BIT (Bilateral Investment Treaties), pamoja na taasisi muhumu kama ICSID, PIC, ICC. Lakini sisi tunakomaa kuwafelisha watoto masomo kama ACCOUNTS. Sijui hii nchi haina watu wenye akili kabisa. Mambo ya ajabu yanafanyika na hakuna hata anayestuka.

Tano, mradi wa LST tangu mwaka 2006 marehemu Prof. Mukoyogo aliupinga kweli kwasababu aliona hauna maana zaidi ya kuwatengenezea ulaji baadhi ya wataalamu wa pale University of Dar es Salaam. Hivi kweli, tuna uhakika kwamba haya masomo ya LST hayawezi kufundishwa vizuri kwenye vyuo ambavyo wanafunzi wanasoma wakiwa wanatafuta Shahada ya kwanza kweli ???

Jambo jingine ni kwamba wataalamu wengi wa pale LST wameamua kufanya biashara ya vitabu. Wanatunga mitihani ambayo majibu yake utayapata kama tu umenunua vitabu vyao. Hili nilishawahi kuambiwa nikathibitisha mwenyewe kwenye baadhi ya vitabu. Hii ni tabia ya kishezi ambayo inaumiza na kukwamisha wengine huku wengine wakipata ukwasi mkubwa. Mwanafunzi anataoa pesa nyingi za Ada lakini hivyo vitabu havipo maktaba, utavipata mpaka umfuate mwandishi mwenyewe na umlipe 50,000. Kwanini msiweke vitabu vingi kule maktaba wanafunzi wakavisoma ???

Sita, hivi inawezekanaje mwanafunzi ambaye amefauli vizuri shahada yake afeli vibaya kwa kiwango cha DISCONTINUE pale LST ??? Ina maana huyu mwanafunzi hafahamu kitu chochote kabisa ??? Lakini, kubwa zaidi ni hili la wanafunzi 600 kuanza pamoja, lakini wanaofaulu ni watu 30, huku nusu ingine ikiwa inafanya SUPPLEMENTARY au DISCONTINUED. Sijui kwanini hili haliwastui Majaji na Wizara. Watu hufeli, lakini siyo kwa kiwango hicho ambacho kinafanyika pale Law School.

Pia, pale pana rushwa sana ya ngono, kukomoana na kubadilishiana matokeo. Kuna jamaa niliwahi kuwa naye mahakamani aliwahi niambia kwamba kuna rafiki zake wanafundisha pale walimuahidi kwamba watamfaulisha, na kweli alifauri vizuri hadi tukashangaa. Alikuwa na maswali hata kabla mitihani haijaanza. Nikasema HIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII...

TANZANIA HAKUNA KITU KINACHOFANYA KAZI VIZURI KUSEMA TUNAWEZA JIVUNIA
Halafu kuna mjinga mmoja anajiita Linguistic kasoma huko Uganda analeta ubishi ubishi hapa..........

Nimeona mada za kuchambua taarifa ya kufeli kwa wanafunzi Law School of Tanzania.

Binafsi na mimi nimepitia Law School, na haya ndiyo ninayoyafahamu kuhusiana na hiki chuo.

1. Law School kiuhalisia, siyo sehemu ya mafunzo kwa vitendo kama mnavyosikia redioni.

2. Somo la field lipo, ila marks zake hazihusiki kwenye kubaini ufaulu. Yaani alama za somo la field hazina maana kwenye GPA calculation maana hazitambuliki.

3. Wanafunzi wa Law School hufundishwa kwa nadharia darasani, na kuingia semina kama ilivyo vyuo vikuu.

4. Mwalimu mmoja hutoa mhadhara kwa wanafunzi wote 600+ na akimaliza anaingia mwingine hadi siku inaisha.

5. Mada zinazofundishwa Law School ni zilezile mwanafunzi alifundishwa vyuoni ngazi ya degree na hakuna tofauti.

6. Muda wa mitihani haupo fair. Kwenye mtihani mmoja, kunakuwa na maswali ya kuandaa hati za mashtaka na madai nyingi mno kiasi kwamba muda wa kuandaa hati hizo hautoshi. Kwa wasijua, hati za kisheria uandaaji wake unahitaji kurejea vifungu vya sheria mbalimbali ambazo unakuwa unazo mezani(Acts).

7. Wahadhiri wa Law School huamini kwamba wanafunzi wao watafeli na mtu akifaulu wanashangaa sana. Yaani wapo kama miungu watu. Pale Law School hata secretary anamdharau mwanafunzi na anataka umuinamie kumsujudu.

8. Mahakimu, na waajiriwa wengine wenye uzoefu kwenye sheria wakienda kujiendeleza Law School nao hufeli pia.

9. Kuna wakati mahakimu walishauriwa wasijiendeleze Law School maana ni fedhea hakimu mzoefu unafeli Law School. Badala yake waliaambiwa watapewa utambulisho maalum kwamba wamefuzu vigezo vya sheria kwa vitendo.

10. Suplementary yaani mitihani ya kurudia haina kikomo Law School. Unaweza hata ukakaa na sup. hata miaka 40.

11. Law School ukikata rufaa ya matokeo haipatiwi majibu na unaweza ukaanza apya kusoma na kumaliza bila kupata majibu ya rufaa.

12. Law School unasoma masomo yote uliyofundishwa kwenye shahada ya sheria kwa miaka minne, lakini ukifika Law School unafundishwa kwa miezi 6 na unapewa mitihani. Halafu miezi mingine 6 unaenda field.
 
Hizo comments mbili hapo juu, za aikambe na MALCOM LUMUMBA nikiri tu, zimemaliza kila kitu.

Wameonesha ni kwa kiasi gani hiyo shule ya sheria haikidhi vigezo, na imegeuzwa kuwa ya wajanja wachache wanaofanya kazi kwa interest zao kwa ajili ya wale wawapendao.

Ajabu mpaka mtu anayetoka mahakamani, aliyezoea kufanya kazi kwa vitendo, nae akienda Law School [shule ya sheria kwa vitendo] anafeli! sasa hivyo ni vitendo vya aina gani wanavyofundisha huko Law School?

Ukweli, hao jamaa wamejigeuza miungu watu, ambao naamini kabisa wanajua kwenye vichwa vyao kila "intake" inapoanza, watafaulu wangapi, na kufeli wangapi, wanachosubiri kufanya ni kuthibitisha kwa vitendo tu [kwangu hii ndio maana ya hiyo shule - ya kufelisha kwa vitendo].

Na kwasababu bahati mbaya hakuna wa kuwauliza, wanasifiwa kwa "kazi nzuri" wanayoifanya ya kufelisha wanafunzi wengi, kama vile hicho ndicho kipimo cha utendaji kazi wao tofauti na shule nyingine zote tulizozizoea hapa duniani, basi wanaendelea kuharibu future ya watoto wa masikini bila hofu yoyote.

Matokeo mabaya ya aina hiyo, naamini kabisa yanaharibu "psychology" ya wanafunzi wanaoendelea na masomo yao hapo kwa wakati huu, hawa sasa wanajua kabisa siku yao ya kuchinjwa iko njiani, na bahati mbaya hawana cha kufanya kwani ada wameshalipa, najua walimu watawaliwaza at the moment, but end of the day, nao wajue watachinjwa tu.

Nashindwa kuelewa, kwanini pasiwepo taasisi, au chombo chochote kitakachofanya kazi ya kufuatilia mienendo ya hao walimu wa hiyo shule ya sheria kwa vitendo Tanzania, hasa perfomance na tabia zao, wasiachwe huru sana mpaka kujiona miungu watu, tunakosea.

Ili wale waliokaa hapo kwa miaka mingi wahamishwe, kwasababu naamini hawa wanatengeneza ukiritimba unaowaumiza wanafunzi, na wale wengine watakaoonekana masomo yao yanaongoza kufelisha wengi kila mwaka, nao waondoshwe/kubadilishwa.
 
Nchi hii kila mtu ni kula kwa urefu wa kamba yake,polisi Rushwa kila siku kwenye madaladala,maofisa ardhi,hupati kibali mpaka utoe pesa,
Nchi ipo jalalani
 
Back
Top Bottom