Law School kufumbia macho tuhuma zinazowakabili haikubaliki

Law School kufumbia macho tuhuma zinazowakabili haikubaliki

Kwa hisani ya mdau aikambe:

Anaandika mdau:

Nimeona mada za kuchambua taarifa ya kufeli kwa wanafunzi Law School of Tanzania.

Binafsi na mimi nimepitia Law School, na haya ndiyo ninayoyafahamu kuhusiana na hiki chuo.

1. Law School kiuhalisia, siyo sehemu ya mafunzo kwa vitendo kama mnavyosikia redioni.

2. Somo la field lipo, ila marks zake hazihusiki kwenye kubaini ufaulu. Yaani alama za somo la field hazina maana kwenye GPA calculation maana hazitambuliki.

3. Wanafunzi wa Law School hufundishwa kwa nadharia darasani, na kuingia semina kama ilivyo vyuo vikuu.

4. Mwalimu mmoja hutoa mhadhara kwa wanafunzi wote 600+ na akimaliza anaingia mwingine hadi siku inaisha.

5. Mada zinazofundishwa Law School ni zilezile mwanafunzi alifundishwa vyuoni ngazi ya degree na hakuna tofauti.

6. Muda wa mitihani haupo fair. Kwenye mtihani mmoja, kunakuwa na maswali ya kuandaa hati za mashtaka na madai nyingi mno kiasi kwamba muda wa kuandaa hati hizo hautoshi. Kwa wasijua, hati za kisheria uandaaji wake unahitaji kurejea vifungu vya sheria mbalimbali ambazo unakuwa unazo mezani(Acts).

7. Wahadhiri wa Law School huamini kwamba wanafunzi wao watafeli na mtu akifaulu wanashangaa sana. Yaani wapo kama miungu watu. Pale Law School hata secretary anamdharau mwanafunzi na anataka umuinamie kumsujudu.

8. Mahakimu, na waajiriwa wengine wenye uzoefu kwenye sheria wakienda kujiendeleza Law School nao hufeli pia.

9. Kuna wakati mahakimu walishauriwa wasijiendeleze Law School maana ni fedhea hakimu mzoefu unafeli Law School. Badala yake waliaambiwa watapewa utambulisho maalum kwamba wamefuzu vigezo vya sheria kwa vitendo.

10. Suplementary yaani mitihani ya kurudia haina kikomo Law School. Unaweza hata ukakaa na sup. hata miaka 40.

11. Law School ukikata rufaa ya matokeo haipatiwi majibu na unaweza ukaanza apya kusoma na kumaliza bila kupata majibu ya rufaa.

12. Law School unasoma masomo yote uliyofundishwa kwenye shahada ya sheria kwa miaka minne, lakini ukifika Law School unafundishwa kwa miezi 6 na unapewa mitihani. Halafu miezi mingine 6 unaenda field.
WASOMI NI VILAZA HUO NDIO UKWELI PIA MMEZOEA KUTOA RUSHWA NA NGONO NA KUNUNUA MITIHANI
LUGHA PIA NI TATIZO KWENU ACHENI KUICHAFUA SHULE
 
Kwa hisani ya mkuu MALCOM LUMUMBA:

Anaandika mdau:

Binafsi naomba nisema yafuatayo kuhusu shule ya sheria Tanzania:

Mosi, kutokana na uhitaji wa elimu ya kusoma kwa vitendo (Post-Graduate Diploma in Legal Practice) haikutakiwa kuwe na shule moja nchi nzima tena ambayo iko kwenye mji kama Dar es salaam. Walau hizi shule zingekuwepo kikanda ili kuwaepusha na kadhia wale wanafunzi wanaotoka mikoa ya mbali kuja kurudia mitihani Dar es Salaam. Mtoto anasafiri kutoka Tarime, hana hata mkopo halafu anakuja Dar es salaam kufanya mtihani akiwa na 50/50 kwamba hilo somo analorirudia atafuaulu au lah.

Pili, mbinu ya kumpima mwanafunzi (Mode of Assessment) siyo rafiki kabisa na haizingatia utaalamu wa kisaikolojia kwamba wanafunzi wana uelewa tofauti. Mtoto anasoma mwaka mzima halafu anapewa mitihani 24 ndani ya mwaka ambayo kama akifeli hata mmoja basi anaweza kupoteza zaidi hata ya miaka 2 anarudia tu kozi hiyo hiyo. Kikawaida tulitegemea kwenye elimu ya vitendo wanafunzi wapimwe kupitia kazi nyingine muhimu ambazo lazima ziwe na alama, kama PRESENTATIONS, GROUP ASSIGNMENTS, CLINICS + WORKSHOPS and INTERNSHIP WITH MARKS.

Sasa wanaitwa DIPLOMA IN LEGAL PRACTICE huku wakichukua ada ya zaidi ya milioni moja, ilhali vipimo vyote vinatolewa kupitia mitihani. Hii siyo sahihi, kwasababu hata mahakamani kwenyewe wanasheria huwa hatuviziani ila tunapewa muda wa kujiandaa. Sasa mtoto anakaa INTERNSHIP miezi zaidi ya sita huku akija kukaguliwa kihunihuni tu mara moja, bila kupewa alama yoyote ile ya muhimu. Kwanini hawa wanafunzi wasipangiwe hata miezi miwili-miwili kufanya kazi la lazima zenye alamu mahakama za mwanza, mabaraza ya ardhi, mabalaza ya usuluhishi, dawati la jinsia ???

Jingine, ambalo nimeliona ni jambo la kipumbavu kufanywa na watu wanaojiita wasomi ni kitendo cha kutoa matokeo ya mitihani yote ya mwaka mzima ndani ya siku moja, baada ya mwaka mzima na miezi mitatu kupita. Kwanini matokeo ya ICA (Individual Continous Assessment), WPE (WRITTEN PRACTICAL EXAMINATION) na FINALS NON-CORE hayatolewi mapema, ili mwanafunzi ajue mbivu na mbichi na aweze kujipanga vizuri kwenye mitihani ya mwisho ??? Pia wawekewe utaratibu maalamu kabisa wa kuyarudia haya masomo wakati hata wako shule, hasa wiki moja baada ya kumaliza WPE ???

Lingine muhimu ni kwamba LST, kuna mitihani ya WPE (Written Practical Examination) ambayo kwingineko duniani mwanafunzi huifanya kwa kufanya tafiti pamoja na majadiliano na wanafunzi wenzake, kisha baadae huenda kufanya huo mtihani. Ilhali sasa pale LST, wanafunzi wanafungiwa masaa manne (4) wakisoma mavitabu, bila kuruhusiwa kuzungumza halafu wanapewa saa moja kupumzika, ili warudi kufanya mtihani huohuo kwa masaa matatu. (It's just emotional debilitating)

Tatu, hili la kulazimisha kila anayesoma sheria awe wakili nadhani ni jambo la kishenzi ambalo lilifanywa kwa mihemko bila kufikiriwa. Miaka yote huko nyuma watu tuliajiriwa kama STATE ATTORNEYS bila hata kuwa wanasheria. Tulitakiwa tu tufanye INTERNSHIP miezi tisa kwa ATTORNEY GENERAL halafu tunaenda kufanya BAR-EXAMINATION kule Arusha. Kinachoshangaza ni kwamba wengi ambao hawakupita Law School wako vizuri kuliko hata hawa watoto wenu wa Mawasiliano nyuma kule.

Kubwa zaidi, wanasheria tuko kwenye nyanja kuu mbili ambazo ni LEGAL PRACTITIONER (ADVOCATES) na JURIST (LEGAL SCHOLARS/LEGAL RESEARCHERS). Hawa ni watu wawili tofauti na wanafanya kazi tofauti kabisa, sasa ukitaka kuwalazimisha wawe kitu kimoja utakuwa unapuyanga mno. Leo hii ushauri wa sheria wa JURIST unaweza kuwa una uzito kuliko hata ORDINARY LEGAL PRACTITIONER, kutokana na tafiti na ufahamu. Sasa kwenye nchi fulani ya kusadikika, wenyewe kwasababu hawana SPECIALIZATION basi wanalazimisha kila mtu awe wakili, kwamba hata JURIST haweza kutoa ushauri kama hana muhuri. Just Lackadaissical and Nonsensical....

Nne, mtaala wa shule ya sheria ni wa kizamani sana na hauwezi kumfanya mwanafunzi awe vizuri kwenye soko la kimataifa. Kuna baadhi ya masomo tulitegemea yafundishwe pale LST, lakini hayapo kwenye mtaala. Mfano, INTERNATIONAL COMMERCIAL ARBITRATION, INVESTMENT LAW, BASICS OF INTERNATIONAL ECONOMICS LAW/ INTERNATIONAL TRADE AND FINANCE LAW. Nchi haina wataalamu wa haya masomo, sisi tunakomaa kufundisha PROPABATE & ADMINISTRATION OF ESTATES, COMMERCIAL LAW, LEGAL ETHICS, HUMAN RIGHTS and ACCOUNTS FOR LAWYERS masomo ambayo vyuo vingi vinayafundisha na vinaweza kuyafundisha vizuri.

Kesi kubwa kama zila za makinikia, DOWANS, ESCROW n.k zinahitaji mwanasheria walau awe anajua masomo ya INTERNATIONAL COMMERCIAL ARBITRATION, ambapo anatakiwa aifahamu mikataba mikubwa BIT (Bilateral Investment Treaties), pamoja na taasisi muhumu kama ICSID, PIC, ICC. Lakini sisi tunakomaa kuwafelisha watoto masomo kama ACCOUNTS. Sijui hii nchi haina watu wenye akili kabisa. Mambo ya ajabu yanafanyika na hakuna hata anayestuka.

Tano, mradi wa LST tangu mwaka 2006 marehemu Prof. Mukoyogo aliupinga kweli kwasababu aliona hauna maana zaidi ya kuwatengenezea ulaji baadhi ya wataalamu wa pale University of Dar es Salaam. Hivi kweli, tuna uhakika kwamba haya masomo ya LST hayawezi kufundishwa vizuri kwenye vyuo ambavyo wanafunzi wanasoma wakiwa wanatafuta Shahada ya kwanza kweli ???

Jambo jingine ni kwamba wataalamu wengi wa pale LST wameamua kufanya biashara ya vitabu. Wanatunga mitihani ambayo majibu yake utayapata kama tu umenunua vitabu vyao. Hili nilishawahi kuambiwa nikathibitisha mwenyewe kwenye baadhi ya vitabu. Hii ni tabia ya kishezi ambayo inaumiza na kukwamisha wengine huku wengine wakipata ukwasi mkubwa. Mwanafunzi anataoa pesa nyingi za Ada lakini hivyo vitabu havipo maktaba, utavipata mpaka umfuate mwandishi mwenyewe na umlipe 50,000. Kwanini msiweke vitabu vingi kule maktaba wanafunzi wakavisoma ???

Sita, hivi inawezekanaje mwanafunzi ambaye amefauli vizuri shahada yake afeli vibaya kwa kiwango cha DISCONTINUE pale LST ??? Ina maana huyu mwanafunzi hafahamu kitu chochote kabisa ??? Lakini, kubwa zaidi ni hili la wanafunzi 600 kuanza pamoja, lakini wanaofaulu ni watu 30, huku nusu ingine ikiwa inafanya SUPPLEMENTARY au DISCONTINUED. Sijui kwanini hili haliwastui Majaji na Wizara. Watu hufeli, lakini siyo kwa kiwango hicho ambacho kinafanyika pale Law School.

Pia, pale pana rushwa sana ya ngono, kukomoana na kubadilishiana matokeo. Kuna jamaa niliwahi kuwa naye mahakamani aliwahi niambia kwamba kuna rafiki zake wanafundisha pale walimuahidi kwamba watamfaulisha, na kweli alifauri vizuri hadi tukashangaa. Alikuwa na maswali hata kabla mitihani haijaanza. Nikasema HIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII...

TANZANIA HAKUNA KITU KINACHOFANYA KAZI VIZURI KUSEMA TUNAWEZA JIVUNIA
Wasomi wetu ni VILAZA
LUGHA ni Tatizo kubwa
 
Chadema tusaidie kulisemea hili. Nyie ndiyo sauti ya wanyonge. Unaweza kuiona kama vie Chadema inaingiza siasa kwenye elimu, lakini hapana, hakuna fairness katika kutunga mitihani. haya hao walimu wa Law shool naye ukimpa hiyo mitihani anayompa mwanafunzi kwa limited time kama ile hawezi kuipass! Wassaidieni wazazi.
Mbowe alisingiziwa Ugaudi mbona mliwaachia chadema wenyewe?
Kura mmewapigia CCM ila Chadema wawasemee WASOMI VILAZA NYIE
 
Mmeliwa vichwa mnaanza kulia lia,

Kasapueni, matokeo hayatabadilika.

Hongera LST kwa kuwafyeka hao mavilaza.

Si kila uzi yeyote anaweza ku comment na hasa akiwa hana ufahamu, uelewa au hoja.
 
Mkuu hata cohort ya 31 walifaulu 28 tu kati ya wote kama hivyo hivyo.

Muda wa kuchukua hatua ni sasa.

Penye nia Pana njia.

Yanayotokea LST na kwingine kote yafansnayo na haya hayakubaliki.
-Unataka watunge paper rahisi?
-unataka Roll number za mawakili ziwe nyingi sana?
-tatizo pia vyuo vikuu mnavyosoma elimu kiwango cha chini
 
Kwa hisani ya mdau aikambe:

Anaandika mdau:

Nimeona mada za kuchambua taarifa ya kufeli kwa wanafunzi Law School of Tanzania.

Binafsi na mimi nimepitia Law School, na haya ndiyo ninayoyafahamu kuhusiana na hiki chuo.

1. Law School kiuhalisia, siyo sehemu ya mafunzo kwa vitendo kama mnavyosikia redioni.

2. Somo la field lipo, ila marks zake hazihusiki kwenye kubaini ufaulu. Yaani alama za somo la field hazina maana kwenye GPA calculation maana hazitambuliki.

3. Wanafunzi wa Law School hufundishwa kwa nadharia darasani, na kuingia semina kama ilivyo vyuo vikuu.

4. Mwalimu mmoja hutoa mhadhara kwa wanafunzi wote 600+ na akimaliza anaingia mwingine hadi siku inaisha.

5. Mada zinazofundishwa Law School ni zilezile mwanafunzi alifundishwa vyuoni ngazi ya degree na hakuna tofauti.

6. Muda wa mitihani haupo fair. Kwenye mtihani mmoja, kunakuwa na maswali ya kuandaa hati za mashtaka na madai nyingi mno kiasi kwamba muda wa kuandaa hati hizo hautoshi. Kwa wasijua, hati za kisheria uandaaji wake unahitaji kurejea vifungu vya sheria mbalimbali ambazo unakuwa unazo mezani(Acts).

7. Wahadhiri wa Law School huamini kwamba wanafunzi wao watafeli na mtu akifaulu wanashangaa sana. Yaani wapo kama miungu watu. Pale Law School hata secretary anamdharau mwanafunzi na anataka umuinamie kumsujudu.

8. Mahakimu, na waajiriwa wengine wenye uzoefu kwenye sheria wakienda kujiendeleza Law School nao hufeli pia.

9. Kuna wakati mahakimu walishauriwa wasijiendeleze Law School maana ni fedhea hakimu mzoefu unafeli Law School. Badala yake waliaambiwa watapewa utambulisho maalum kwamba wamefuzu vigezo vya sheria kwa vitendo.

10. Suplementary yaani mitihani ya kurudia haina kikomo Law School. Unaweza hata ukakaa na sup. hata miaka 40.

11. Law School ukikata rufaa ya matokeo haipatiwi majibu na unaweza ukaanza apya kusoma na kumaliza bila kupata majibu ya rufaa.

12. Law School unasoma masomo yote uliyofundishwa kwenye shahada ya sheria kwa miaka minne, lakini ukifika Law School unafundishwa kwa miezi 6 na unapewa mitihani. Halafu miezi mingine 6 unaenda field.
Wangeifuta tuu wameiga CPA ila kwa kuwa hawajui hesabu masomo ya miandiko mara nyingi ni kuchomekea tu na kujidai ndio wanaweza watu wanatoa CPA kwa kufanya mitihani mara mbili tuu na masomo magumu sembuse huko mnaferishana ili muonekane ni vitu vya maana kweli..
 
Chadema tusaidie kulisemea hili. Nyie ndiyo sauti ya wanyonge. Unaweza kuiona kama vie Chadema inaingiza siasa kwenye elimu, lakini hapana, hakuna fairness katika kutunga mitihani. haya hao walimu wa Law shool naye ukimpa hiyo mitihani anayompa mwanafunzi kwa limited time kama ile hawezi kuipass! Wassaidieni wazazi.

Erythrocyte ni bahati mbaya sana vyama vya siasa vimeshindwa kutambua ni wajibu wao kuwatia shime wananchi kudai haki zao bila kujali ni zipi wala maslahi ya moja kwa moja kwao.

Kwenye hili vyama hivi vinapaswa kutambua tatizo hili ndilo lililo kikwazo kikubwa linalopelekea agenda zingine zenye maslahi makubwa ya taifa kukwama pia.
 
Wangeifuta tuu wameiga CPA ila kwa kuwa hawajui hesabu masomo ya miandiko mara nyingi ni kuchomekea tu na kujidai ndio wanaweza watu wanatoa CPA kwa kufanya mitihani mara mbili tuu na masomo magumu sembuse huko mnaferishana ili muonekane ni vitu vya maana kweli..
-"mnaferishana" au sio?
-kwa hiyo mkuu sheria sio kitu cha maana?
-kwa hiyo masomo ya miandiko ni rahisi?
 
-tatizo linaanzia TCU hawakagui hivi vyuo kikuu vinavyofundisha sheria, na kuhakikisha wanadhibiti Ubora wa elimu, ndio maana Mi-Gpa mikubwa isiyo na tija.
 
-Unataka watunge paper rahisi?
-unataka Roll number za mawakili ziwe nyingi sana?
-tatizo pia vyuo vikuu mnavyosoma elimu kiwango cha chini

  • Unayasoma wapi yenye kutaka paper nyepesi?
  • Nini tatizo la number za mawakili kuwa nyingi kama utahini ni WA haki?
  • elimu vyuo vikuu elimu Iko chini isipokuwa LST?

Hivi ndugu, mada umeisoma? Umetambua kuwa kuna tuhuma ambazo haziwezi kufunikwa tu? Kwamba ingependeza kupata majibu?

Kwamba kutokutoa majibu hakuwezi kuwa option?

Kwanini blah blah? Kwanini hamtoi majibu? Kwani mnataka kuficha nini?
 
-tatizo linaanzia TCU hawakagui hivi vyuo kikuu vinavyofundisha sheria, na kuhakikisha wanadhibiti Ubora wa elimu, ndio maana Mi-Gpa mikubwa isiyo na tija.

Hukusikia mbaazi ikikosa maua husingizia jua? Tuhuma ya rushwa ya ngono IST, uwajibikaji alaumiwe TCU?
 
-"mnaferishana" au sio?
-kwa hiyo mkuu sheria sio kitu cha maana?
-kwa hiyo masomo ya miandiko ni rahisi?
Huko kuna tuhuma za ngono nje nje kwa wadada...mnasoma nini watu wengine washindwe kufanya kwa kiwango hicho mnachoferishana...
 
Hukusikia mbaazi ikikosa jua husingizia jua? Tuhuma ya rushwa ya ngono IST, uwajibikaji alaumiwe TCU?
-kama hizo tuhuma zipo basi ni hatari
-kuna rushwa ya ngono halafu bado wanafeli, au unatoa rushwa ya ngono halafu hufaulishwi i.e hupasishwi?
 
Huko kuna tuhuma za ngono nje nje kwa wadada...mnasoma nini watu wengine washindwe kufanya kwa kiwango hicho mnachoferishana...
-kiswahili chenyewe hujui kuferishana eti
-hapo ni Law School sehemu ambayo wanawaandaa Mawakili Wasomi sio undergraduate kwenye kupeana First Class
 
-kiswahili chenyewe hujui kuferishana eti
-hapo ni Law School sehemu ambayo wanawaandaa Mawakili Wasomi sio undergraduate kwenye kupeana First Class

Tofautisha typo mistakes na hoja ndugu.

Kwanini hamjibu hoja? Yako wapi majibu ya tuhuma zinazowakabili?
 
  • Unayasoma wapi yenye kutaka paper nyepesi?
  • Nini tatizo la number za mawakili kuwa nyingi kama utahini ni WA haki?
  • elimu vyuo vikuu elimu Iko chini isipokuwa LST?

Hivi ndugu, mada umeisoma? Umetambua kuwa kuna tuhuma ambazo haziwezi kufunikwa tu? Kwamba ingependeza kupata majibu?

Kwamba kutokutoa majibu hakuwezi kuwa option?

Kwanini blah blah? Kwanini hamtoi majibu? Kwani mnataka kuficha nini?
-tatizo lipo ndio kwenye roll number kwa sababu sio kila mtu ni lazima awe Wakili pengine Law School wame set standard za kutunga mitihani migumu ili kuwapunguza
-ni kweli elimu ya Vyuo vikuu vingi vya sheria iko chini except Udsm,Mzumbe main campus hivyo vyuo vina LLB za maana siyo kama KIU,and the like wakifika Law school pale ni mkazo paper ngumu.
 
Tofautisha typo mistakes na hoja ndugu.

Kwanini hamjibu hoja? Yako wapi majibu ya tuhuma zinazowakabili?
-huyo jamaa hajui tofauti ya L na R
-miongoni mwa majibu mlishapewa na pasco kuwa baadhi ya vyuo vikuu vya sheria vinatoa chini ya kiwango hizo LL.B
 
-kiswahili chenyewe hujui kuferishana eti
-hapo ni Law School sehemu ambayo wanawaandaa Mawakili Wasomi sio undergraduate kwenye kupeana First Class
Mkuu kiswahili kweli sijui ila hoja kuu ni rushwa ya ngono kwa wanawake mimi ni mtaalamu wa hesabu kiswahili sijui kweli ila hizo hesabu watu wanafanya vizuri kwa level zote iweje hayo masomo yenu ya kawaida tuu...ina maana wewe uliefanya vizuri umewazidi nini hao wengine?
 
Back
Top Bottom