Lawama zote za umeme ziwaendee Kitila Mkumbo na Nehemiah Mchechu

Halooo.


Porojo zinaendelea, Mara, Naibu Waziri Mkuu, mara TANESCO wenyewe amekuja Makonda na hadithi nyingi na ni zile zile tu..... mpaka Januari akahamishwa for rocking the boat. B.S

Watu wanaumia. Uchumi unaumia.

Haijalishi, tukirudi hapa kwenye ushauri wako bibie nashuku this is part of of a hidden agenda. Ndio, ushauri wako huu ni kutupotosha tufikiri kwamba hakuna mpango huo(this is a smokescreen), wakati tunafahami miezi kadhaa iliyopita wakiwa Dubai kulikuwa na dili la kuuza au kugawiwa TANESCO kwa wajomba na wawekezaji wengine, Itoshe palikuwa na ujumbe mkubwa kutoka marekani ulioambatana na wabobezi wa sekta ya ugavi wa Umeme, binafsi najua kuna jambo huko nyuma ya pazia ila tatizo lilikuja na IGA ile ya bandari. Fastforward, nakumbuka jinsi TANESCO walivyoanzisha mchakato wa kuweka ramani ya vikoa vyao,(domains) yaani maeneo ya nyaya na nguzo za umeme. Nilishtuka niliposikia kuwa wanafanya asset and land valuation. Hiyo inaashiria kuwa wanatafuta net worth au siijui total worth ya TANESCO ili ikae mkao wa kuuzwa.

Inawezekana kabisa hayo juu yakawa ni ya kawaida na kama ulivyosema huko juu TANESCO ina "bust na hivyo kuna uhitaji wa kutafuta suluhisho la kudumu.

Tatizo langu linakuja pale wanapolazimisha kutafuta mapungufu ndani ya TANESCO wakati ni dhahiri hakuna shida kubwa sana kama tunavyo taarifiwa au tunavyo aminishwa. I'm ready to be corrected. Why all this smokescreens? Why mislead us?

Again, mimi nadhani mpango huu unaoushauri upo and its just a mater of time. Nafikiri mnatafuta a best equlibrium kati ya wadau wanaotaka hizi kampuni zibakie serikalini na wale wanotaka ziuzwe na kugawiwa kama njugu. In short a balanced public opinion.

But, at what costs?
 
Kulikata vipande Tanesco haitoleta tija zaidi litayumba haijawahi tokea, shirika lipate safu nzuri ya Uongozi kuanzia Waziri, Katibu mkuu, Mkurugenzi yaani viongozi wafuatiliaji siyo wa kukaa nyuma ya pazia kuvizia upepo kama alivyokuwa Jmakamba na DBiteko sasa. Tanesco ni dude moja kubwaaaa linataka mtu makini sana shida za umeme zitakuwa kitendawili yote yanaanzia Kwa mtawala akiwa na uthubutu linanyooka vizuri tena Kwa muda mchache, Raisi SSH ajivishe Bomu la Tanesco maana zigo ni lake Kwa tukio lolote.
 
Umeongelea kila mkoa uwe na shirika lake la kujitegemea, na vipi kuhusu mgawanyo wa vyanzo vya umeme?
Vyanzo vya umeme vijitegemee. Shirika la uzalishaji umeme Tanzania. Wauze umeme kwa mashirika ya mikoa(Regional Power Supply Authorities or companies)
 

Ushauri wako wa kila mkoa kuwa nashirika lake la umeme hautekelezeki kwani Zaidi ya nusu ya mikoa Tanzania haina source yoyote ya umeme
Nafikiri kungekuwa na mashirika mawili
Moja lijikite katikauzalishaji na moja liwe lina sambaza
Lakini kuna vimiradi vina anzishwa karibia kila mwaka vya mabilioni ambayo vipo kiupigaji
kwa nini wasiweke nguvu kwanza kwa hii miradi iliyopo isimame badala yake utasikia mara iringa sijui kuna kamradi, mara bukoba etc yaani hawana focus au pengine wana mahela mengi tu yanatengenezewa kazi .........ili yaonekane yametumika
 
Hawatathubutu kamwe kuliweka rehani Tanesco wataishia kupima maji Kwa fimbo tu, Shirika ni kubwa mno lakini likipata msukumo wa siasa nzuri litanyooka mapema hapa Mh Raisi ni kuweka mtu makini mwenye weledi wa wafanyacho Tanesco mengine yatakuwa hadithi.
Ndani ya shirika wapo wataalamu wengi lakini weupe mno kichwani ndiyo maana hata kwenye vetting hawatoboi ingekuwa kete nzuri sana la kulinusuru shirika, akili kama za Maharage zilikuwa nzuri mno shida ni vile jMakamba alikuwa na agenda zake nyuma ya pazia dhidi ya kiti kile pendwa.
 
Hiyo mikoa isiyo na "source" Kwani sasa hivi wanatoa umeme kutokea wapi?
 
Vyanzo vya umeme vijitegemee. Shirika la uzalishaji umeme Tanzania. Wauze umeme kwa mashirika ya mikoa(Regional Power Supply Authorities or companies)
Yale yake tu, kutwanga maji kwenye kinu.
 
Hakuna kunyooka wala kupinda. Hatuna uwezo wa kuendesha vishirika vidogo vya umma kama mwendokasi tu, tutaweza jishirika kubwa namna hiyo?
 
Utakufa kwa presha za chuki na kukosa adabu na heshima. Huyu mama kalikuta hili shirika lipo katika hali mbovu kuliko lilivyo sasa.
Watu kama wewe hawana mchango ila uchochezi na chuki.
Mleta mada katoa pendekezo la tanesco kuvunjwa na kila mkoa uwe na shirika lake. Wewe badala ya kuleta hoja yako hapo umeganda kwenye chuki kwa wazanzibari na uislamu.
Akili mgando kama zako italizamisha hili taifa
 
Ana macho yanaona sana na ana masikio yanasikia sana, ndiyo maana akawateua Kitila na Msechu wayasimamie mashirika yasiyofanya vizuri.

Lawama ziwaendee wao, ndiyo wenye majukumu ya mashirika ya umma kwa sasa, zisiwaendee wengine.
Tehe tehe, Afrca kuambiana ukweli badi ni safari ndefu sana, nina uhakika unajua kabisa tatizo ni Mama ila sasa kusema hii ni nyeupe na hii ni nyeusi huwezi kwa sababu unazo zijua mwenyewe
 
Kitila na Mchechu ndiyo wenye dhàmana ya kuhakikisha mashirika ya umma yanafanya kazi ipasavyo au yana reform au yanakuwa rebuilt au yanafutwa kabisa.

Best option kwa tanesco ni Rebuilding tu kwa sababu Reforms zimefanyika nyingi na zimeshindwa kutatuwa matatizo.
 
Huna hoja unaleta viroja.

Sikushangai, nafahamu hapo ndipo akili za Mtanzania zilipoishia.
 
Tuweke records sawa kwanza: Kwani Kitila na Mchechu wameteuliwa lini? Vipi hali kabla yao ilikuaje?

Kwani strategic/sustainable plans za Taifa kwenye masuala ya nishati zikoje ? Nimeona nichangie kwa style hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…