Lazaro Nyalandu arudi rasmi Chama cha Mapinduzi akitokea CHADEMA

Lazaro Nyalandu arudi rasmi Chama cha Mapinduzi akitokea CHADEMA

Inaonekana hujawahi kupitia nyuzi zangu vizuri, hilo la kwamba Lowassa alihonga ili apewe nafasi ya kugombea urais halina mjadala, na nimekuwa nikilisema mara kibao. Sina uhakika na kiwango, ila alihonga...
Kumbe Mbowe alikula milions kadhaa za Lowassa, na kumbe ndio sababu hatya kumnadi Lissu alishindwa kwasababu ilikuwa sawa na kujitolea kanisani?

tindo nimefurahishwa na jinsi unavyomwaga nondo zako hapa!
 
Inaonekana hujawahi kupitia nyuzi zangu vizuri, hilo la kwamba Lowassa alihonga ili apewe nafasi ya kugombea urais halina mjadala, na nimekuwa nikilisema mara kibao. Sina uhakika na kiwango, ila alihonga.

Na Nyalandu pia alihonga ili apate nafasi, bahati mbaya hakuwa na mvuto kwa wanacdm, na tulikuwa tunamponda waziwazi na nyuzi zetu Zipo humu humu jukwaani. Yeye kurudi ccm ni sawa na kuvuja kwa pakacha.
Walikuwa hawampendi?

Hivi unamoitishaje mtu ambae humpendi ashindane kwenye kinyang'anyiro cha urais?

Vipi kama hizo hela zake zingefua dafu kama kwa Lowasa..?
 
Wataanza kusema bora magufuli, laana ya kumtukana marehemu ita yatafuna mbaka yatubu.
Mimi najiuliza,haya mapambio wanayomyomuimbia mama na kumtukana JPM,inamaana 2025 watasimama na mama?
Kama hawatasimama naye,watabadili upepo kuelekea wapi?

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Upinzani utakuwa na maana pale tutapata katiba mpya, reform ya sheria zinazohusiana na siasa na chaguzi, watu kuwa na vipato binafsi huru na upinzani utakapoacha kuchukua makapi.
Mkuu, hata mimi nimeshindwa kuwaelewa wanasiasa wetu. Hawana utofauti kati ya wasomi na ambao sio wasomi, halikadharika na vyama navyo havinautofauti kwamba hiki ni kikongwe na hiki ni kichanga kwa maana kwamba kikongwe kionyeshe udhabiti wa kusimamia.

sheria, kanuni na taratibu zake. Leo wasiasa wanahama chama bila ya sababu za msingi na chama alichohamia kinampokea bila Sababu za msingi na anaweza kurudi kule alikotoka ndani ya mwaka mmoja bila sababu za msingi na akapokelewa kwa bashasha. Kwenye miaka ya 1970/80 kujiunga na CCM ni sharti uende kozi ya miezi 3 na ufaulu ndipo upewe kadi ya kujiunga. Aidha huwezi kuhamia CCM na kupewa cheo/uongozi ndani ya mwaka 1.

Leo mambo yamebadilika wanasiasa wabadilisha vyama kama abiria wavyobadilisha daladala/mwendokasi. Vyama siku hizi ni kama dodoki inachukua kila kitu, kiwe na tija ama kisiwe na tija. Wanasiasa ni watu muhimu sana katika ustawi wa nchi, maendeleo ya nchi kwa asilimua kubwa yanachangiwa na wanasiasa, kwa mantiki hiyo ukiwa na wasiasa legelege, masilahi, fuata mkumbo na vyama navyo vikawa hivyo hivyo.

Basi ni dhahili maendeleo TUTASUBILI sana.
 
Mkuu, hata mimi nimeshindwa kuwaelewa wanasiasa wetu. Hawana utofauti kati ya wasomi na ambao sio wasomi, halikadharika na vyama navyo havinautofauti kwamba hiki ni kikongwe na hiki ni kichanga kwa maana kwamba kikongwe kionyeshe udhabiti wa kusimamia...
kwani mkuu unaposema maendeleo tutachelewa sana uliambiwa kuwa maendeleo yapo CHADEMA? umefeli sana CCM baba lao
 
NYIMBO ZA SIFA HAZIIMBWI KWA JIRANI, JAMANI JAMANI, ZABURI KIBOKO. NYIMBO ZA MFALME DAUDI KWA MUNGU WAKE
 
Back
Top Bottom