mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Njaa mbaya sana! Njaa haimshindwi mtu, ni suala la muda tu! Kinachokera hawataki kusema ukweli!! Nyalandu umerudi kwa wazazi wako wa kisiasa kiri kuwa huko nje njaa kali!!Lazaro Nyalandu wa CHADEMA amerejea CCM kupitia mkutano mkuu wa CCM leo jijini Dodoma.
Nyalandu aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA amesema walikuwa wamechukuliwa na walilazimishwa kumwimbia bwana lakini wao pamoja na mzee Lowassa, Sumaye na Dkt. Slaa wamegoma kuimba kwani bwana yuko CCM peke yake..
Hivi watu wazima unatudanganya eti ulilazimishwa kumwimbia bwana mmoja? Wewe ndio wa kulazimishwa? Umaskini jeuri mgumu! Uliondoka ccm kwa jeuri sawa na mwana mpotevu!!
Kama vile njaa ilivyomrudisha mwana mpotevu kwa baba yake hali kadharika njaa imemrudisha Nyarandu CCM! Ila kama alivyosema JPM, hao ni ng'ombe waliokatwa mkia!! karibuni nyumbani ila kila tukiwaona hamna mkia tunakumbuka mliwahi kutukimbia!! Tutawaamini waliobaki nasi kwa majukumu mbali mbali kwanza kabla ya kuwatazama ninyi! huo ndio ukweli!!!
Ndio maana hata kina Mpenda Zoe bado wanasota!! na wameshaanza kusahaulika!! Hivi mnafikiri joka la makengeza limetulia pamoja na kusemwasemwa mnadhani Halina akili? Mzazi akikusema Shakuru!! Hamna pa kukimbilia!