Lazaro Nyalandu arudi rasmi Chama cha Mapinduzi akitokea CHADEMA

Lazaro Nyalandu arudi rasmi Chama cha Mapinduzi akitokea CHADEMA

Jamani changieni tu maana yametokea mengi mi sichangii, kwani Nyalandu amefungua mpaka maandiko ya Biblia kumsindikiza yakiwa na maana kule ugenini ngoma hazichezeki.
 
Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu ametangaza rasmi kurejea CCM mbele ya Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Samia Suluhu kupitia Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Dodoma leo, akitokea CHADEMA.
 
Mabeberu rasmi ndani ya chama.
1619778408242.png
 
CHADEMA kunahitaji wanasiasa wapambanaji na sio watafuta fursa.

Nashukuru sana sijawahi kuwa na imani na hao wanaccm wanaokuja cdm. Hilo la Nyalandu kurudi ccm nilikuwa nalifahamu vyema. Ni ngumu sana kwa mwanaccm kutoka nje ya ccm na kuendelea na siasa za ushindani, kwani wengi hutegemea siasa za mbeleko. Hata wakati Nyalandu anagombania kuwa mgombea wa Cdm, nilisema wazi kuwa Nyalandu hastahili nafasi hiyo maana sio mwanacdm, bali ni mwanaccm aliyetofautiana na Magufuli.
 
Back
Top Bottom