Lazaro Nyalandu arudi rasmi Chama cha Mapinduzi akitokea CHADEMA

Lazaro Nyalandu arudi rasmi Chama cha Mapinduzi akitokea CHADEMA

Lazaro Nyalandu alipandisha ndege kwenda ughaibuni hakupandisha ?




Sasa ni zamu ya Lazaro kupondwa na CDM na upinzani kwa ujumla na kupata utetezi kwa vijana wa CCM


KUSIFU ,KUSHFU kiongozi kisa hayupo upande wako siyo afya kabisa mtu apewe sifa zake kwa kuzingatia ukweli bila itikadi hii itasaidia vinginevyo vijana wafuata upepo watakimbia mbele na kurudi nyuma sanaaa


Mimi naendelea kusema mchafu ni mchafu na msafi ni msafi haijalishi yupo chama gani
Hajawahi kusifiwa na wapinzani, usitake kupotosha. Kwanza Nyalandu hakuwa na swaga za siasa za kipinzani.
 
Kabisa mkuu Nyarandu sasa atakoma
Jamaa aliendaga hadi nje nchi, siasa ni rahisi when you got nothing to lose ni ngumu when you got to much to lose. No wonder Marshall Mathers apigi zile spana zake za early 2000[emoji23][emoji23]
 
Usiseme alinyimwa! Bali alishindwa na Lisu kwenye kura za maoni.

Chadema wangukuwa na akili hata ile kumpa formu agombee wasingempa

Fomu anaweza kupewa mtu yoyote maana ni hela yako na uwe mwanachama. Ila kupitishwa ndio shughuli.
 
Yaani hata kwa kuangalia tu kwa macho mlifikiri Nyalandu ni Chadema kweli? Wataka maslahi tu hawa. Pia nahisi kama Chadema walimshtukia mapema wakamuweka bench kiasi kikubwa. Alishaona ameshakataliwa hivyo amerudi kwao.
 
Hahahah.. Bavicha mnapata tabu, sasa hapa itabidi

Hahahah.. Bavicha mnapata tabu, sasa hapa itabidi mbadili gia muanze kumnanga Nyarandu?
Tukizungumzia unafiki, uchu wa madaraka, matumizi mabaya ya dola, na wizi wa kura vyote unavipata CCM kwa pamoja! So mtu akijaribu kubadili mazingira atashindwa
 
Nyumbu watasingizia nini?
Mbowe ameendelea kupuuzwa
 
Ndivyo ninavyosikiliza hapa nikiwa Live kutoka Dodoma.

===
Lazaro Nyalandu amerejea CCM akitokea CHADEMA. Amerejea Aprili 30 katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM ulifanyika Dodoma.

Nyalandu aliwahi kuwa mtia wa kugombea urais kupitia Uchaguzi Mkuu 2020 kupitia CHADEMA. Ambapo katika hotuba yake ameshukuru kwa kumpokea.

Amesema katika nchi ya Ugenini wimbo hauimbiki.
Maisha haya 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Wewe acha zako bhana! Nyarandu mkampa hadi uenyekiti wa kanda alafu unataka kusema nini hapa?
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji19]
giphy.gif
 
Hata hvyo aliwasaidia sana mgonjwa wao lissu ameonesha utu
 
Fomu anaweza kupewa mtu yoyote maana ni hela yako na uwe mwanachama. Ila kupitishwa ndio shughuli.
Mpaka anaenda kupigiwa kura maana yake kamati kuu ya chama imempitia na kuona anafaa kwahiyo wakaona aende akashindane na wenzie ili yeyote atakae pita awe rais.

Kwa hiyo Nyarandu aliaminiwa mpaka na kamati kuu ya chama.
 
Lazaro Nyalandu wa Chadema amerejea CCM kupitia mkutano mkuu wa CCM leo jijini Dodoma.

Nyalandu aliyekuwa mjumbe wa kamati kuu ya Chadema amesema walikuwa wamechukuliwa na walilazimishwa kumwimbia bwana lakini wao pamoja na mzee Lowassa, Sumaye na Dr Slaa wamegoma kuimba kwani bwana yuko CCM peke yake.

Nyalandu ameiomba radhi CCM na amewashukuru kwa kumpokea tena.

Kadhalika mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Lindi Dr Suleiman Methew naye amerejea CCM alikokuzwa kisiasa.

Kazi Iendelee!
🤣🤣🤣👆👆👆👆Ila kigogo aliwaonya mapema
 
Tukizungumzia unafiki, uchu wa madaraka, matumizi mabaya ya dola, na wizi wa kura vyote unavipata CCM kwa pamoja! So mtu akijaribu kubadili mazingira atashindwa
Si mmesema yote hayo kaondoka nayo Magufuli na mambo yote ni safi?
 
Back
Top Bottom