Huyo chizi mvuta Mabange amenzisha nyuzi kwa kunidhihaki kuniita majina ya hovyo bila sababu za msingi ndio maana nikampokea kihuni kama alivyokuja . Amekuja kwa kunitukana na kunikebehi nikashindwa kumvumilia mpaka nikavuka mipaka katika kumrudishia ujinga wake.
Mimi nashirikiana sana tu na watu Wakristo tena mpaka wengine tunaitana Kaka na kula pamoja , sio Mtanzania tu binadamu yeyote hata awe Yahudi nitashirikiana katika mambo yote mazuri katika Dunia na kumsaidia ila sio kwenye ibada zake .
1. Akiumwa nitamchangia , koneksheni ya kazi na michongo nitampa hata akiwa mkiristo.
2. Sito mdhulumi , kumvunjia heshima yake wala kumnyanyasa sababu ya dini yake.
3. Mimi majirani na Wakristo mtaani na niliosoma nao wananiheshimu sana na kujiona best friend na sijawahi kuwaTreat vibaya kisa ukiristo wao Wala kuisema vibaya dini yao , tunashurikiana vizuri kwenye mambo mengine kwenye dini kila mtu na yake.
Ahsante, mkuu 'adriz', kwa jibu lako. nimekuelewa.
Nilitaka tu kuweka alama ya "like" kwenye bandiko lako hili zuri na nisepe zangu; lakini moyo ukakataa, nikalazimika niache maneno machache kwenye bandiko lako hili.
Niliposoma maandishi yako niliyo'quote' na kuuliza swali, nilikuwa bado sijasoma hayo mengine mliyokuwa mkijibishana kati yako na huyo 'chokonozi' aliyekuweka kwenye hali ya taharuki na kuandika yale maneno.
Sasa kabla ya kuona hili jibu lako kwangu, nikaona ni bora nami nisome haya majibizano yenu nione kilichozua taharuki hadi ukafikia kuandika yale uliyo andika..
Ni kweli kabisa, huyo 'looseNut' ni kama anatafuta tu uchokozi kwa maksudi kabisa.
Lakini:Unapomjibu mtu kama huyo, halafu ukawahusisha na wengine wooote kwenye kundi kama ulivyofanya hapo; matatizo huanzia palepale, maana nawe sasa unakuwa huna tofauti yoyote na huyo chokonozi. Nchi yetu itaingia kwenye mtafaruku kwa sababu tu ya hamaki za aina hii. Hapa jibu lako halikuwa la kumlenga tena huyo 'looseNut', ukawalenga wengine wooote wasiokuwa upande wako, kama ulivyoelezea waziwazi kabisa.
Binafsi siamini kamwe kuwa waislam woote huwaona waTanzania wenzao, bila kujali imani zao kuwa kama ulivyojieleza hapo; na kwa maana hiyo hiyo; huyu 'looseNut' kamwe hawezi kuwa yeye ndiye mwakilishi, au mfano wa kuigwa katika hao anaodhani wapo upande wake.
Umejieleza vizuri katika andiko lako hapa juu; na bila shaka moyoni mwako unatamani sana hali ya namna hiyo; lakini mara kadhaa unajikuta umelemewa na misuguano ya mara kwa mara inayotokea; hasa humu JF na katika siasa za nchi yetu hii. nayasema haya; kwa sababu michango yako humu JF naijuwa inasimamia wapi, na sioni ikikazia hayo uliyonieleza kwa ufasaha mkubwa hapo juu.
sasa umeniacha nimechanganyikiwa ni wapi hasa unakokusimamia wewe kama mTanzania .
Mimi ningependa sana sote tuweke maslahi ya nchi yetu hii Tanzania mbele, zaidi ya kitu kingine chochote; kwa maana, kufanya hivyo ndiko kutakakoleta thawabu hata huko kwenye imani walizonazo waTanzania wote, bila kujali ni imani ipi; ya kiislam, kikisto, kibuddha, n.,k.., n.k., Hakuna Mungu asiyependezwa na kuwepo kwa nchi iitwayo Tanzania, ambayo wananchi wake wanaishi kwa umoja na ushirikiano kati yako. Tofauti hizo ndogo ndogo zisisababishe kumchukiza Mungu wa kila upande husika.
naomba tena unisamehe kwa andiko refu hili kidogo. tuilinde Tanzania yetu hii kwa juhudi zetu zote.