Le Mutuz (W. Malecela) Vs Alberto Msando: Hii ni vita ya kupigania haki za wasanii au kopo la Coca?

Le Mutuz (W. Malecela) Vs Alberto Msando: Hii ni vita ya kupigania haki za wasanii au kopo la Coca?

Status
Not open for further replies.
Nilivyoelewa baada ya maelezo ya W. J. Malecela, Coka wamewachukua maceleb kwenye uzinduz na kuwapa personalised Le Kopoz kama token.

As it looks, wanazouza zina majina ya kawaida kabisa tena moja moja. Mfano kwa Tz unaeza kuta Mrisho, Benjamin, Ali, Julius, etc. Kwa maelezo ya Le Mutu, hutakuta Le kopo la koka la Le Mutu likiuzwa kitaa.

Hiyo ndo Albert alikataa wasanii 'wake' wasikubali. Mfano ukute Le Kopo la Kidoti, AY, MwanaFA, etc. Hiyo itaenda moja kwa moja kwenye kuhitaji mikataba na malipo.

To that extent, kuna yoyote mwenye ushahidi wa jina la staa ambalo si common name, hata huko nje, lililotumika madukani ukiacha lile Le Kopoz la token?
Mkuu ukitaka kujua hawajielewi cheki hapo chini sababu ni tofauti na unachosema kwamba majina yao hayatotumika kwenye kopo za mtaani

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=11639115
 
Last edited by a moderator:
Mkuu not necessary wachapishe majina yao kwenye chupa zinazouzwa street, NO! kitendo cha kutoa Picha ya FidQ et al na kichupa chenye jina lake tayari ni promotion ya bure kwa CocaCola. Unaweza kuwadharau sababu ni bongo flavour/movie lakini kama ungekuwa na idea ya marketing and sales strategies ungeweza kunielewa ni nini naongea.

Hawa watu wana-followers na kwa nafasi zao influence yao ni kubwa kulinganisha mimi na wewe regardless of their background or education level.

Kama mmeumia hivyo nendeni mahakamani basi mkafungue class-action lawsuit.

Kama kweli mna nia njema na kama kweli mnaona hawakutendewa haki, kwamba wamenyonywa (ingawa sidhani kama mna hoja yoyote ile iliyo ya msingi), basi hamtaishia kulalamika huku kwenye mablogu.

Mchukueni jenerali wenu huyo Msando (yeye si ni mwanasheria bana...) mwende mahakamani mkaishitaki Coca-Cola kwa kuwadhulumu wasanii wenu wapendwa.
 
Mkuu not necessary wachapishe majina yao kwenye chupa zinazouzwa street, NO! kitendo cha kutoa Picha ya FidQ et al na kichupa chenye jina lake tayari ni promotion ya bure kwa CocaCola. Unaweza kuwadharau sababu ni bongo flavour/movie lakini kama ungekuwa na idea ya marketing and sales strategies ungeweza kunielewa ni nini naongea.

Hawa watu wana-followers na kwa nafasi zao influence yao ni kubwa kulinganisha mimi na wewe regardless of their background or education level.

Kwa mfano Juma Nature kwenye kutoa albamu yake ya Ugali alijaza watu Uwanja wa Taifa hii inaonyesha huyo mtu ana nafasi yake kwenye jamii kwa mantiki hiyo kibiashara anaweza kutumika na akainfluence sales sababu ana followers.

Mfano mdogo tu na wa Mwisho sikiliza kwa makini sana wimbo wa Afande Sele "Kioo cha Jamii"

If you truly believe you have a solid legal case then mobilize your like minded troops and march to court and sue the hell out of Coca-Cola.

I don't think you have a prayer. Prove me wrong.
 
If you truly believe you have a solid legal case then mobilize your like minded troops and march to court and sue the hell out of Coca-Cola.

I don't think you have a prayer. Prove me wrong.

huyo uliyomjibu kwa english una uhakika gani anajua english? we msukuma tushajua ni mkali wa english uwe una comment kwa kiswahili labda kama unaomjibu naye ameandika kwa english bila hivyo utakuwa unajibu watu hawaelewi
 
quote_icon.png
By Muuza Sura

Tatizo la msando anataka kuwachukulia wasanii au viceleb vya bongo vyote vijinga na kwa kiasi kikubwa kawawin wengi amesahau kama Le mutuz kuna mambo huwezi kulipeleka. ..ujue ukiwa mtoto wa town hata ukiwa boya kiasi gani huwezi kupelekeshwa na mtu wa mkoani. ..Le mutuz town moja,msando mkoa moja

- MWanasheria wenu uchwara amekosea sana na siamini kama kweli anajua Sheria I mean yeye angewaongelea Wasanii wake ambao kwa kuwakataza amewanyima opportunity ya kujiendeleza wenyewe kwani hao wasanii wake average kwa mwezi wanatengeneza pesa ngapi? Shaq mchezaji wa zamani wa NBA unakumbuka aliwahi kusema nini wakati Ewing anawahimiza kuigomea NBA kwa sababu ya malipo, alisema hakutegmea Ewing mtu aliyesoma shule kubwa kama Gerogetown anaweza kuwa mjinga namna ile kutaka kushindana na Mkuu wa NBA Stern na wamiliki matajiri wa timu za NBA ni simply kwamba niggaz hawatashinda na ni kweli kesho yake Stern aliwapa onyo la mwisho wa wachezaji wote wa NBA kuwa kama hawakukubali hela wanazolipwa atawafukuza wote na kuajiri wapya, wachezaji wakashindwa na kukubali.

- Huyu Mwanasheria wenu anaamini Wasanii wanaweza kushindana na Cocacola na wakashinda? Hivi kweli Cocacola inahitaji Msanii yoyote wa bongo ili kuendelea kama ilivyokuwa miaka yote? Please alitakiwa kutafuta njia ya accomodation, kwenye Capitalism as we are now unatakiwa kuona opportunity at anything, unamkataza msanii leo kesho tunasikia amesaini mkataba na Pepsi sawa it make a sense lakini unamkataza msanii ambaye anaweza kukaa miaka hata 2 bila kazi unasema una akili sana that is foolish to me!!

- Ni client gani babu kubwa anaweza kumkubali huyu Mwanasheria na hizi tactics zake za kutukana watu wasiokubali ushauri wake Instagram? Mimi sijawahi kusikia hata siku Mwanasheria aneytukana watu anaowahitaji kuwa Clients wake, mimi sihitaji ushauri wa Mwanasheria kama huyo never na siamini kwamba ana akili za kutosha eti anasema mimi ninaishi kwenye jengo la NHC ambalo linamilikwa na baba yangu now niambie toka lini kuna baba wa mtu hapa mjini anamiliki Jengo lolote la NHC? hahahaha halafu huyu jamaa kwani alikuja lini hapa mjini cause miezi Sita iliyopita sikuwahi kumsikia huyu jamaa, ninakumbuka wakati flani alikuwa akimsaidia Zitto mahakamani that is all, hapa mjini mbona kuna Wanasheria wengi tu na wana pesa kuliko zake lakini hawana matusi?

- I mean unawakataza wasanii a golden opportunity ya kujiendeleza wenyewe bila sababu ya msingi halafu huwapi alternative? please!! Msanii mwenye akili akipewa kopo anatakiwa kulitumia kujiongeza like the way I did kama hawezi ina maana hana akili, unamuomba Mungu msaada anakueltea unasema sikuomba msaada huu ok tafuta basi msaada unaoutaka, huyu Mwanasheria wenu uchwara ajifunze na ajipange tena asiingilie mji kwa papara!!

Le Mutuz
 
Le mutu kwa akili ya kifisadi ya ccm bado anajitetea kijinga kuwa ni WIVU anadhani inatosha kabisa.
 
Le mutu kwa akili ya kifisadi ya ccm bado anajitetea kijinga kuwa ni WIVU anadhani inatosha kabisa.

- so far wanaomjua kwa karibu wanasema ni tabia zake za kukasirika kwa kukosa kupewa kopo lake hahahahaha sio mimi cause simjui kabisa wala sijawahi kumuona in my life!!, sasa imagine mtu mjanja na mimi simjui hapa mjini?

Le Mutuz
 
Nyani Ngabu kumbe jamaa alinadi zitauzwa shop kwa jina lake hilo Le Mutuz ingawa leo kabadilika.

- Yaaap makopo yatauzwa kwa yenye jina langu ni kweli hiyo ni lugha ya biashara to the mass kwanza, na ndio makubaliano behind the scene ambayo huwezi kuyasema siku ya kwanza unless umeulizwa na media kuhusu mkataba ukoje, hivi kweli unaamini cocacola in theior right minds wanaamini wanaweza kuuza makopo yenye majina ya watu bila kuwalipa ni nchi gani hiyo imewahi kutokea?

Le Mutuz
 
Cheyo, labda jamaa alikua anajipa tu promo huku mitandaoni kwamba kakamata dili kubwa.

- Jokate kasain mkataba mkubwa na Wachina Billioni 8.1 hivi wewe unajua masharti ya mkataba wake? Hapana unatangaza the deal kwanza mengine yatakuja to the public ikibidi kwa sababu mimi najua kwamba sio kweli watampa tu Billioni 8.1 no lakini to the public lazima useme the general idea, people jipangeni kwanza!!

- Jokate na Cocacola walichofanya tofauti yake ni nini hasa, mbona huyu Mwanasheria wenu ushwara hajalalamika wasanii ku promote sandals za jokate bure?, unakumbuka mkataba wa Beckham LA wa kuvuna USD $ 250 Million kwa mwezi? kwani ni kweli alipata hizo pesa? No ile ilikuwa ni the general idea kwamba ile timu wakiweza kuuza jezi na vifaa vingine kwa kumtumia Bekham wanaweza kumpa hizo pesa lakini sio kweli kwamba alilipwa hizo pesa!!

Le Mutuz
 
Nyani Ngabu kumbe jamaa alinadi zitauzwa shop kwa jina lake hilo Le Mutuz ingawa leo kabadilika.

Well, labda vidole vyake viliteleza.

Ila kama ikitokea hizo chupa zenye jina lake zitaanza kuuzwa rejareja basi hapo ndo itahesabika kama endorsement na mambo ya fidia ndo yataingia kwenye mlinganyo.

Lakini hii ya uzinduzi wa kampeni ambapo inawezekana kabisa hata raia wengine wa kawaida na wasio maarufu nao walipata chupa na makopo yenye majina yao sambamba na hao watu maarufu, sioni uhalali wa fidia yoyote.

Nadhani wengi wetu hatuna taarifa za kutosha kuhusu uzinduzi wa hiyo kampeni na tunajenga hoja kwa kutegemea picha za Instagram na mabandiko ya watu kwenye mablogu ambao hata siyo wahusika.
 
- so far wanaomjua kwa karibu wanasema ni tabia zake za kukasirika kwa kukosa kupewa kopo lake hahahahaha sio mimi cause simjui kabisa wala sijawahi kumuona in my life!!, sasa imagine mtu mjanja na mimi simjui hapa mjini? Le Mutuz
NSSF tayari ndio walikuwa wanalia na serikali ya CCM wanaotafuna nao hela kuwa fao la kujitoa lifutwe.Sasa hivi wanaweza slot ya hela kwa week ya kutoa ambayo ni ndogo kuliko madai ya kutoa ya watu.Km unavyojua mifuko ni mingi,na wanaojitoa ni wengi kuliko wanaoingi aktk huu upatu.NSSF sasa hivi ni piramid km nyingine,wanategemea hela za wanaoingia kuwapa wanaotoka km DESI tuu.Baada ya kutangaza kutoa hela za matibabu na materninity muda si mrefu wanacheza faulu.Wanakata ktk akiba ya mwanachama huku wakichukua sifa kuwa wanajali wanachama.Na mbaya wanakata nyingi zaidi kuliko wlaiyotoa.Ipo idadi kubwa sana ya watu wana paper evidence ya nianyoyasema hapa,na wapo ktk madai sehemu mbalimbalia mikoani.Sasa miaka si Mingi,itakuweje baada ya miaka 20 ,walioiba wakiwa hawapo tena NSSF na majengo yameshauzwa kwa dili na issue nyingine?KWA SASA TZ SI BANK WALA MASHIRIKA YA AKIBA NI SALAMA KUWEKA HELA.
 
hivi kweli unaamini cocacola in theior right minds wanaamini wanaweza kuuza makopo yenye majina ya watu bila kuwalipa ni nchi gani hiyo imewahi kutokea?

Le Mutuz

Ma nigga...hicho ndo kinachonifanya mimi nisite kabisa kuamini kwamba eti kampuni kubwa ya Kimarekani kama Coca-Cola inaweza kufanya kitu kama hicho tena kwenye hizi zama za utandawazi.

Yaani wauze soda zilizo kwenye makopo yenye majina ya wasanii maarufu bila ridhaa au makubaliano yoyote yale?

Are they that dumb?

Ingekuwa ni kampuni ya kibongobongo labda....lakini Coca-Cola?

Hard to believe.

Nadhani wengi wetu humu hata hatujui ins and outs za uzinduzi wa hiyo Share a Coke campaign na ndo maana baada ya kuwauliza watu humu kama wanajua taarifa zozote zile ma makubaliano na maafikiano yaliyofikiwa kati ya Coca-Cola na hao 'influencers' pamoja na vigezo na masharti yake, hakuna hata mmoja aliyejitokeza na kusema kuwa anajua au anazo taarifa husika.

Nadhani watu wengi watakuwa wameingizwa mkenge na huyo Msando aka lawyer wa Instagram.
 
- so far wanaomjua kwa karibu wanasema ni tabia zake za kukasirika kwa kukosa kupewa kopo lake hahahahaha sio mimi cause simjui kabisa wala sijawahi kumuona in my life!!, sasa imagine mtu mjanja na mimi simjui hapa mjini? Le Mutuz
Le Mutuz tunapokuwa tofauti kifikra na aina ya watu wa kundi lenu lililo karibu na watawala walioifikisha hii nchi kujiendesha yenyewe(Auto pilot/self drive) ni haya.Ni Kweli Alberto anajulika kwa vitabia vingi sana vyenye shida ktk jamii ,ila kuitaja hapa haifanyi hoja yako kuwa na nguvu.Ila inawafanya muwe wengi tuu ktk kundi linalofanya vitu vya madhara bila kujua au kutojali madhra kwa wengi na jamii pana ya kitanzania. Wewe kuweka HOJA ya yeye kukosa ili utetee huu wizi wa cocacola,inaonyesha shida ya hii nchi,hata mafisadi wakijitetea huwa wanasema wengine wanaona wivu kwa vile wamekosa,km vile inaondoa ufisadi.Unaweza dhani kuwekwa ktk vizibo kunakukuza kisiasa ,ila kumbe kunakudhalilisha na kukufanya kiongozi wa kuwauza wengine ktk dili kichaa.Alberto weather amekosa au anabeep ili atulizwe bado haiondoi ukweli kuwa wote mnayo shida.Cha kujiuliza kiu yenu ya Hela na madaraka itaishia wapi?Mna malengo kuwa wapi mkifika mtarealize mafanikio au kuwa financially free?
 
- Jokate kasain mkataba mkubwa na Wachina Billioni 8.1 hivi wewe unajua masharti ya mkataba wake? Hapana unatangaza the deal kwanza mengine yatakuja to the public ikibidi kwa sababu mimi najua kwamba sio kweli watampa tu Billioni 8.1 no lakini to the public lazima useme the general idea, people jipangeni kwanza!! - Jokate na Cocacola walichofanya tofauti yake ni nini hasa, mbona huyu Mwanasheria wenu ushwara hajalalamika wasanii ku promote sandals za jokate bure?, unakumbuka mkataba wa Beckham LA wa kuvuna USD $ 250 Million kwa mwezi? kwani ni kweli alipata hizo pesa? No ile ilikuwa ni the general idea kwamba ile timu wakiweza kuuza jezi na vifaa vingine kwa kumtumia Bekham wanaweza kumpa hizo pesa lakini sio kweli kwamba alilipwa hizo pesa!! Le Mutuz
Le mutuz mbona logic uliyotumiwa kuficha dili yako hujatumia kuficha ya Jokate?Na wewe uliingia dili km nani maarufu nchini?Dalali..?Details zitakuja wakati wasanii umeshawapiga ..sasa hivi watashtuka waongeze dau hadi wewe upunguze mgao wa kuwaburuza?Now ninapata picture..hayo beckham najua unaburuza...Nijuavyo Bekham hela yake alipewa ingaw ilikuwa spread ktk miaka yake ya mkataba kuweka ktk vitabu vya account km mwaka.Kuuza Jezi na vitu vingine chini ya makampuni si kazi yake.
 
Well, labda vidole vyake viliteleza.

Ila kama ikitokea hizo chupa zenye jina lake zitaanza kuuzwa rejareja basi hapo ndo itahesabika kama endorsement na mambo ya fidia ndo yataingia kwenye mlinganyo.

Lakini hii ya uzinduzi wa kampeni ambapo inawezekana kabisa hata raia wengine wa kawaida na wasio maarufu nao walipata chupa na makopo yenye majina yao sambamba na hao watu maarufu, sioni uhalali wa fidia yoyote.

Nadhani wengi wetu hatuna taarifa za kutosha kuhusu uzinduzi wa hiyo kampeni na tunajenga hoja kwa kutegemea picha za Instagram na mabandiko ya watu kwenye mablogu ambao hata siyo wahusika.

- Mamen kilichotokea ni kwamba ICL ndio wanaosimamia zoezi hili na ndio waliofanya party ya juzi Mliman City, makopo ya kwanza yalikuwa ni uamuzi wa mwenye jina kuna waliokataa lakini majina ya kwanza yalichaguliwa na Cocacola wenyewe ila hata kama sio Star ukitaka kopo sasa hivi ukiwaendea wanakutengezea that is all, MWanasheria wa Instagram alichokosea na ni kosa la wengi sana hapa mjini kuamini maneno ya mtaani kwamba watu wote ni wajinga mwenye akili ni yeye tu hapo ndipo alipoharibu,

- Maneno mengi yanayorushwa hapa kuhusu LE Mutuz huwa hayana ukweli ila kwa sababu ya itikadi ndio maana haya maneno huwa yanarushwa hapa, sasa kuna watu wengi sana huwa wanakuja hapa kichwa kichwa na kuamini kila kitu wanachokisoma hapa hasa kuhusu mimi sasa kivumbi kinakuja tukikutana uso kwa uso, huwa wanaishia kuja kuniuliza eti wewe ndio Le Mutuz tunayemsoma JF huwa nawajibu why, always neno moja tu kwamba mbona hufanani kabisa na tunayoyasoma mimi nilidhani wewe ni mjinga mjinga flani au mlevi flani hivi masikini ya Mungu I go through this kila siku, sasa na huyu Mwanasheria wenu ameingia huo mkenge wa kuamini kwamba ana akili kuliko sisi wote na alipokosea ni pale aliposema mambo ya utabiri waumri wangu, kwamba nina miaka 56 kama baba yake ndio maana sina akili, sasa imagine MWanasheria wa kweli hasa hapa mjini unaweza kwenda kujiingiza kwenye huu ujinga wa maneno hewa namna hiyo?

- Yaani huyu Mwanasheria wenu uchwara ili kushinda hoja na mimi ni lazima atumie maneno ya chini kama kunitabiria umri wangu hahahaha? hapo ndipo nilipomdharau kabisa kwamba jamaaa ni mjinga flani hivi ila kasoma sheria kidogo maana Mwanasheria wa kweli ili kushinda argument ya kisheria na mtu kama mimi hawezi kukimbilia kutabiri umri wangu kwanza ili niongope ndio aseme hoja yake that is childish na foolish!!

Le Mutuz
 
Le mutuz mbona logic uliyotumiwa kuficha dili yako hujatumia kuficha ya Jokate?Na wewe uliingia dili km nani maarufu nchini?Dalali..?

- Well, deal ya Jokate ilitangazwa to the public na majuzi Jokate alikuwa anatoa sandals kwa watu wengi maarufu hapa mjini kwa kupiga picha nao na kuzitangaza to the public hata mimi aliniomba nikamfanyia bure sasa mbona hakuna aliyepiga kelele kwa jokate ila kelele kwa cocacola wakati the idea ni ile ile?

- Hivi kweli wewe hujui kwamba mimi ni maarufu hapa Tanzania? I mean I am a Social Media King kwa sababu nina followers wengi sana my blog in 2 years imepitiwa na watu Millioni 15 ina maana watu Millioni 7 kwa mwaka mmoja, ndio maana niliweka mguu chini mpaka Miss Tanzania akarudisha taji, kweli kwenye hili jukwaa wewe unaweza ukajadiliwa hata kwa page moj tu mkuu? unauliza majibu hahahaha

Le Mutuz
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom