KERO Lecturer wa NIT ametutapeli Pesa za leseni wanafunzi zaidi ya 100 wa mwaka huu 2026

KERO Lecturer wa NIT ametutapeli Pesa za leseni wanafunzi zaidi ya 100 wa mwaka huu 2026

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mtoa mada ana lake jambo siyo bure, ukienda pale NIT mitaa ya Mabibo mwisho wale walimu wengi wa NIT mambo ya Udereva wana vituo vyao binafsi ambavyo wanakufundisha udereva na wanakupa cheti tu Ila leseni unaenda kuchukua TRA. Kwa nlivomuelewa mtoa mada ni kwamba yeye katapeliwa kituo cha Essence driving School kinachomilikiwa na mwalimu wa NIT.
Kwa kurahisisha unaambiwa lipia kabisa na hela ya lessen inakuwa Rahisi kwa chuo au Wakala Kushughulikia kwa pamoja Maana mnakuwa wengi, which is ok
 
1792301643050.jpeg
 
Uongozi wa chuo cha NIT , na TRA na Jeshi la Polisi , tunaomba mtusaidie kupata haki yetu .


Lecturer wa NIT ambaye anaitwa Manala T Mbumba, ametutapeli pesa za leseni zaidi ya Wanafunzi miamoja tuliokuwa tunahitimu mwaka huu na ambao tunaingia mwaka wa tatu.


Alikuja chuoni kupitia kwa CR wa kozi mbalimbali na kutangaza offer ya mafunzo ya Udereva yanayoambatana na Leseni.


Mafunzo Alisema ni 170K na Leseni 70K


Baada ya kumpa hizo pesa ni miezi takribani minne hatujapata leseni.


Tulianza kujua ametutapeli baada ya kufunga magroups ya Whatsapp

Na pia kutuambaia hakuna Vyeti wala leseni.


Utapeli huu ameufanya kwa kutumia nembo ya chuo cha NIT akishirikiana na mke wake anayeitwa Georgina Shirima na Rafael Sungura.


Historia inaoensha sio mara ya kwanza anatepeli watu huyu Manala T Mbumba hii imekuwa tabia yake .


Tunaomba TRA na uongozi wa NIT kupitia mkuu wa chuo na Jeshi la police, mtusaidie kupata haki yetu.


Maana wengi tulijinyima pesa zetu ili tupate mafunzo ya Udereva hapo katika shule yake ya Udereva ila tumeishiwa kutapeliwa .


Jina la Shule yake ya Udereva linaitwa Essence Driving School

Ana Tawi Mabibo , Goba na Tegeta.


Huu ni utangulizi tu ila nipo tayari kutoa Taarifa zaidi kuhusu huyu Manala T Mbumba kuhusu utapeli wake

Huyo jamaa alikuwa anauza na viwanja ametapeli watu wengi sana

Huyo ni tapeli wa miaka mingi na mwaka 2025 aligombea ubunge kula za maoni akapigwa chini

Mke wake ni mchaga anaitwa Georgina Shirima, wote ni matapeli wa miaka mingi

Huyo hakuna sehemu hajatapeli kuanzia wafanyakazi wake , Wanafunzi n.k


Huyo ni muhuni pia ana chuo pale kahama Kuna MTU kamtapeli kiwanja , na Kuna mtu kamtapeli gari

Wafanyakazi kazi wakike amekuwa akiwaomba ngono huyo ni muhuni tu poleni sana

Ukiingia Facebook anajiita Manala Mbumba ni tapeli mkubwa sana
 
ikiwa ni kweli.. fungueni kesi mahakamani mkiwa na vielelezo vyote bila kusahau kila mmoja wenu stakabadhi yake ya malipo kukomesha utapeli usiendlee.. hela ni imekuwa ngumu sana mtaani kupatikana.
Huyo
Haihusiani na chuo hiyo ni scandal binafsi

Huyo ni mwizi anabidi ashtakiwe yeye na chuo chake
 
Chuo cha Arusha wanachukua rushwa wazi wazi kabisa na usipotoa rushwa sidhani kama utapata hiyo Leseni yao mimi waliitoa E nilikua sina cheti ila C na madaraja mengine cheti kipo nilipoenda kuuliza kwanza wanasema nisome wiki mbili au wana kidampa wao anakusanya hela ili uende siku ya kupiga picha na test tu nikaachana nao kwa sababu daraja E sio kipaumbele changu kwa Tanzania ingawaje nina leseni ya kaburu ina code 14 sawa na hiyo E yao..
Tanzania kila kitu deal aisee..
Kiongozi, Ni Arusha tech au??
 
Back
Top Bottom