KERO Lecturer wa NIT ametutapeli Pesa za leseni wanafunzi zaidi ya 100 wa mwaka huu 2026

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Leseni yenyewe haina hata barcode ukitaka kuingia kwenye store ili wasome taarifa zako hakuna kitu wanapata harafu milolongo ya kuipata ni hatari pamoja na rushwa..
Nilikuwa na mpango wa kurudi pale.
Hapo Arusha kuna sehemu gani naweza kujifunza driving na leseni hamna mlongolongo?. Mimi pale nishawahi pita nikachukua degree yangu ya biomed
 
kwani mfumo si ulibadilika au?,suala la leseni sikuhizi vyuo vya udereva sidhani kama vinahusika,leseni unaipata online kama sikosei
 
Inauma sana. Nimepiga hesabu hii: 70K+170K = 240K. Hii 240K * 110 = 26,400,000/=. Muhuni akaiweka mfukoni kirahisi tu halafu jioni yupo bar na Serengeti lite mezani anajisifia kuwa yeye ni mjanja kawapiga mafala.

Ametumia nafasi yake ya utumishi ktk umma kujinufaisha binafsi.
Ikifika siku 3 mbele hajawekwa mtu kati na mamlaka husika, ndiyo nitajua kweli Kuna watu wengi wanaichukulia nchi yetu kama shamba la bibi.
 
Nimeambiwa huyo jamaa ni mhuni. Alisingizia mpaka kifo cha babake na akalipwa na chuo kumbe babake mzima kabisa.
Kawazalisha wanawake kibao.

Aliwadanganya mpaka RC , akafunga ndoa ya pili kanisani.

Ila nimeambiwa ni genius kwa uwezo wa darasani.

Poleni sana. Huyo ni tapeli mkomavu. Chuo wanajua matatizo yake Ila wanamlinda tu labda Shauri ya uwezo wake wa shule.
 
wanachuo wanachanga hela ya leseni, nchi hii inakua ngumu hata kwa viongozi kwa sababu viongozi na sisi wananchi hatujapishana sana
 
Kwahiyo unabishana na aliyetendewa?, kama jambo halikuhusu na hulijui acha kutoa hitimisho.....kwanini awe huyo mwalm na sio wengine?.
 
Huyu angekuwa kenya.....angesha Huyu angekuwa kenya angekutana na wahuni wenzake
 
Sitetei Chuo Wala Mwanafunzi
Suala La Leseni Ni Baada Ya Kuhitimu Na Hakuna Mtu Anaweza Mfano Kupigwa Picture Kwa Niaba Yako Wala Kuchukuiwa Alama Za Vidole Kwa Niaba

Haya Majizi Nilitaka Kujua Tu NIT Hapo Ilikuwa Kama Daraja La Kuwaaminisha
 
NIT si inakozi za driving? Tatizo mnapenda kitonga , veti na leseni bila kusoma.
 
Nyie haki yenu kuibiwa mana mlitaka leseni bila ya kusoma na mlivokua vichwa upande mkampa shirima hela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…