Legacy kuu za Mwalimu Nyerere: Mwiba mkali kooni mwa Watanganyika

Kwa mfano kwenye katiba ya CCM na katiba ya nchi watu wametumia uhuni kubadili katiba nanyakatokea ya Oktoba 29.
Kwa hiyo hawa wahuni aliwatengeneza Nyerere?
Na bahati nzuri, katika mstari huo huo umeandika "KUBADILI". Sasa Nyerere angewazuia vipi hawa wahuni?
Nyerere alirithi mofumo ya kikoloni na aliiacha mofumo hiyo na yatumika hadi leo.
Nyerere hakutengeneza hiyo mifumo na kuifanya kuwa matakwa ya taifa nyakati zote. Kama ilifaa wakati wake kwa sababu mbalimbali, haina maana kuwa itafaa nyakati zote.

Lakini hapa la muhimu ni kuwa umeeleza uwepo wa "wahuni". Nyerere hakutengeneza taifa la wahuni hata siku moja.
 
Hoja ya mleta mada ni kwamba Nyerere RIP alirithi mifumo ya kikoloni na hadi anang’atuka Mwaka 1985 aliacha ikiwa hivyohivyo.

Mzee Mwinyi aliongezea biashara huria na utandawazi lakini mifumo ilikuwa palepale na Nyerere alikuwepo akiona hadi anafariki mwaka 1999 mifumo hiyo ilikuwa ipo palepale.

Mifumo hiyo imeendelea na imeimarika hadi leo na ni vigumu mno kuibadili.
 
Hivi mzazi wakk akikufungisha ndoa halafu ndani ya ndoa mkawa hamuelewani, kosa ni la mzazi? Aaah labda kwa sababu Kakuchagulia mke eeeh!

Sasa pengine mkorofi ni wewe ulokuwa mkorofi ndaninya ndoa, umekutana na mwanamke mwenye mdogo kutwa kukukera..

Katiba ni sawa na Mila na Desturi zetu, tatizo lenu Miafrika mnataka kuwa kama Wazungu yaani kila kitu chenye thamani kubwa kwenu lazima kimetokana na Wazungu. Mmerudi kwenye Ukoloni bila kujijua tena mnasifia.

Na nasikia siku hizi kama mwanao hazungumzi Kiingereza, hawezi ajiriwa. Rushwa rafiki wa kila mtu, hakuna fisadi labda kabambikiwa kesi! Ajira yenye kipato cha Juu Tanzania - KUSEMA SANA Yaani mdomo ni Rasilimali. Ukiona Wanasiasa wako juu ujue domokaya!, Wabunge -domo, Machawa - domo, Wasemaji sijui Yanga Simba domo, TV radio hiko kote wanaita wenyewe nini vile? 'Content Creator'au sio?.. kina Manara na Mange Kimambi wanapiga hela za nguvu utadhani wana Phd.

Yaani, mabalaa ya Dunia hii leo ni sawa na Muislaaam kumlalamikia Mohammed kwa nini aliwaletea Kuruan, au Yesu kwa nini alituachia Biblia ya Upendo na Amani wakati dunia hii tunataka kujiachia!

Well naweza andika siku nzima hapa kwa sabanu nawashangaa Wadanganyika. Wanashindwa kujitazama wenyewe walivyobadirika kwa hiyo wanataka na Katiba ibadirike kama wao.

Yaani sawa na kusema maada leo kuna Ushiga basi hiyo misahafu nayo itume HAKI yetu. Kwa haikuandikwa kwa ridhaa yetu.

Damn.... Am out!
 
Mkuu.'Richard', sasa unanichanganya akili kwelikweli!

Mimi nilidhani hiyo kura unayozungumzia, wananchi walisema wanataka chama kimoja tu, au kuna kura ya maoni nyingine?

Na ni nani huyo "aliyezunguka nchi nzima, Nyerere?
Mimi nilidhani ni Nyerere huyo huyo aliyeshawishi uwepo wa vyama vingi, au?

Hata katika hili la mabadiiko na fikra mpya kama unavyosema, tukubali kwamba hiyo ndiyo njia pekee katika jamii zote duniani? Hapawezi kuwepo fikra mpya nje ya kutokuwepo na vyama vingi vya siasa?
Naomba tu nieleweke hapa kuwa sipingani na dhana ya uwepo wa vyama vingi vya siasa nchini; lakini swala la "fikra mpya" halina uhusiano wowote na hivyo vyama vya siasa.
 
Mzee Mwinyi aliongezea biashara huria na utandawazi lakini mifumo ilikuwa palepale na Nyerere alikuwepo akiona hadi anafariki mwaka 1999 mifumo hiyo ilikuwa ipo palepale.
Kwa hiyo unachosema hapa ni kwamba uwepo wa mabadiliko uliwezekana; kwa huo mfano wa Mzee Ruksa.
Hii mifumo haikuizuia hayo mabadiliko aliyofanya Ruksa; lakini kwa sababu zisizoelezeka, mifumo hiyo hiyo ikazuia mabadiliko mengine yote.

Na kwa bahati mbaya kabisa, mifumo hiyo hiyo ikakubali "WAHUNI" waingie na kuitumia mifumo hiyo hiyo kuharibu kila kitu.
Na kwa maana hiyo, hata kama Nyerere angekuwa angali hai, hawa "wahuni" wanaotumia mifumo yake huenda angewapongeza!

Does it make sense?
 

Chama Cha Mapinduzi.
5th - February - 1977
 
Nchi nyingi duniani vyama vingi vyashindanisha sera zao na wananchi kazi Yao kupima sera hizo.

Lakini again, mifumo tulo nayo yazuia kuweka vyama vingi kwasababu ni mifumo hiyohiyo imekalia katiba mbovu na mifumo hiyo imejifunika blankets za jeshi, polisi na TISS.

Hivyo twahitaji kiongozi kutoka Sayari ya Mars aje avunje hiyo mifumo, kisha atangaze kura ya maoni wananchi waishinishe mabadiliko ya katiba.

Kisha tuamue ttwatumia rasimu ya Jaji Warioba au la.

Baada ya hapo waja uchaguzi mkuu wa kwanza wa kihistoria tangia tupate uhuru utaoongozwa na kusimamiwa na tume huru ya kweli ya uchaguzi.

Na baada ya uchaguzi mkuu wa kwanza wa kihistoria tangia tupate uhuru, ndo twapata serikali ya kwanza ya kihistoria itakayowafuta machozi watanganyika na kuanza kazi ingine mpya ya kuliponya taifa.

Itakuwa ndo mwanzo ya ukweli wa kaulmbiu isemayo SOTE PAMOJA KULIOKOA TAIFA.
 
Very interesting. 😅🤔
 
Juu-juu unaweza kudhani hii hoja ina mashiko lakini ni propaganda.

Nimeisikia hii hoja mara ya kwanza nikiwa chuo, kwamba Zanzibar ni tishio.

Ila sasa ni tishio kutoka kwa nani : WAKOMUNISTI au WAARABU ???

====================================================

Tukisema ni WAKOMUNUSTI, ukweli mchungu ni kwamba Tanzania ilikuwa na mahusiano mazuri sana na USSR na wamefanya kazi kwa ukaribu mkubwa kwenye mambo mengi. Wakomunisti walijenga kambi zao kubwa ANGOLA, MOZAMBIQUE na NAMIBIA ambako walikuwa wakiwasaidia SWAPO, FRELIMO na UMKHOTO-WE-SIZWE, ambao mafunzo yao walikuwa wanafanyia Tanzania. Hadi miaka ya 1992, taarifa kama za The Mitrokhin Archives zinaonyesha majasusi wa KGB/GRU-USSR ndiyo walikuwa wanafundisha IDARA YA USALAMA WA TAIFA. Hilo tishio la USSR dhidi ya Tanzania lilitokea wapi ???

Ukweli ni kwamba ukiangalia kwa ukaribu mapinduzi ya Zanzibar 1964, utamfahamu muhanga mkubwa: GENGE LA WAARABU/WAAJEMI ambao walijimilikisha Zanzibar na kuamua kutawala weusi wengi. Kama tishio lingekuwa ni UKOMUNISTI basi wahanga wa kwanza wa mapinduzi wangekuwa ni WAKOMUNISTI kina Prof Abdulrahman Mohammed Babu ambao ndiyo walimbatiza Mzee Nyerere kwenye UKOMUNISTI. Bahati mbaya sana, historia inaonyesha kwamba wahanga wakubwa walikuwa ni WAARABU/WAAJEMI ambao walikuwa ni WAISLAMU.

Tukisikiliza PROPAGANDA za WAISLAMU za kusema Kanisa Katoliki ndilo lilimtuma Mzee Nyerere kuvamia Zanzibar na kuanzisha MFUMO KRISTO, maswali mengine mengi yataibuka, kwasababu vinara wakubwa wa mapinduzi walikuwa ni WAISLAMU wenzao kina Abeid Aman Karume, Kassim Hanga, Abdulrahman Mohammed Babu, Thabit Kombo n.k ambao ndiyo walikuja kutawala Zanzibar punde baada ya mapinduzi. Kwenye hili WAISLAMU huwa wanatapika UJINGA bila kuzingatia UKWELI wa wakati huo kwasababu kama wangetaka kuanzisha UKRISTO, ingekuwa ni jambo rahisi mno kwasababu Zanzibar kipindi cha mapinduzi ilikuwa na watu laki moja tu (100,000), ilhali Tanganyika ina watu Milioni Kumi (1,000,000)

=====================================================

HOJA KUU, ambayo huwa ina mashiko ni kwamba Mzee Nyerere miaka ya 1961-1964 alikuwa na mahusiani mazuri na U.K na USA. Baada ya The Cuban Missile Crisis 1962, wao ndiyo walimshurutisha na kumshawishi aivute Zanzibari ili kuzuia UKOMUNISTI wa USSR usisambae. Mzee Nyerere mbali na kuwa MJAMAA alikuwa ni MODERATE ukilinganisha na wenzake kama Nkrumah ambao they turned RED inside-out.

=======================================================

SWALI LA MSINGI: Kama tatizo lilikuwa ni USSR, kwanini COLD-WAR ilipoisha walilazimisha MUUNGANO uendeleaa, hata wale G55 walipoanza harakati zao mwaka 1993 Mzee Nyerere aliwafanyia vimbwanga na fujo ???
​
 
MALCOM LUMUMBA Nyerere kabla hajafariki aliwaambia,mchukue mema yake na muyaendeleze.Mabaya au yasiyowafurahisha myaache.Sasa,kuanza kumlaumu tu wakati mna muda, akili,maamuzi na uchaguzi ni kutozitendea haki nafsi zenu.Tumieni.Wakati ni huu!
Mzee Nyerere kabla hajafariki alihujumu mchakato wa kidemokrasia katika ngazi za kichama na ngazi za kitaifa, kulazimisha Mzee Mkapa awe Raisi na CCM iendelee kubaki madarakani kimabavu ilhali ilikuwa ishapoteza mwelekeo. Aliwadhuru watu waliopingana na mawazo yake. Kina Kolimba na Kombe walipoteza maisha kisa Nyerere's Fragile EGO.

Halafu baada ya miaka 4 anaanza harakati za chini-chini kutaka kumhujumu Mzee Mkapa mtu ambaye alizunguka kumnadi kusema ni MSAFI a.k.a MR CLEAN. Akianza kulalamika kwamba anauza mali za taifa kiholela.

The Paradox of Nyerere's Repentance: Yeye ndiyo alilazimisha watanzania wakubaliane na kurudisha VYAMA VINGI mwaka 1992 kinyuma na TUME YA JAJI NYALALI, lakini hapohapo kwa upande wa nyuma akaanza kuvihujumu vyama vya upinzani kwenye uchaguzi mkuu 1995, kwa kuwaita wapinzani "Mbwa-Dogs".

Hao-hao watu ambao alikuwa anawaita "Mbwa-Dogs" na hawawezi kuongoza nchi, kwa nyakati tofauti-tofauti wamewahi kushika nyadhifa kubwa nchini Tanzania, tena sehemu nyeti huku wakifanya vizuri sana. Mzee Edwin Mtei, (RIP) alikuwa ndiyo Gavana wa Kwanza wa Fedha Tanzania, na Waziri wa Fedha, kazi ambazo alizifanya kwa uwezo mkubwa sana. Unaposema mtu kama huyu ni "Mbwa-Dog". unataka sisi tukueleweje labda ???

Augustino Lyatonga Mrema (R.I.P), aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Naibu Waziri Mkuu na Afisa Usalama Mkubwa tu, ambaye alifanya kazi yake kwa weredi mkubwa. Alikuwa anaifahamu nchi vizuri sana, NJE-NDANI. Kusema kwamba Mrema ni "Mbwa-Dog" ilhali amewahi kusaidia hili taifa kuwa salama, unataka tumueleweje huyu Mzee Nyerere ambaye mnataka kumsifia hapa ???

=====================================================
KIUFUPI, wapinzani wote wa kisiasa kuanzia mwaka 1994-1998 walikuwa ni watu wenye uwezo mkubwa na wamewahi kulisaidia hili taifa kwa nyakati na majira tofauti. Kuanzia Kolimba, Kombe, Kambona, Babu, Mrema, Mtei na Malima wote hawa wana mchango mkubwa sana kwa nchi kuliko hata alivyokuwa Mzee Mkapa kabla hajawa Raisi.

KILICHOMPONZA, ni kutaka kuendelea kuwa Raisi hata baada ya kustaafu, kutokutaka kuruhusu MABADILIKO YACHUKUE MKONDO WAKE yenyewe. Sikupenda kabisa ambacho Mzee Mkapa alimfanyia Mzee Nyerere mwishoni mwa uhai wake, lakini ukweli mchungu ni kwamba Mkapa was Nyerere's very own creation.
​
 
Alianza kitambo tatizo wagumu kuelewa
Huenda hujamuelewa mleta mada alichozungumzia kumhusu Lissu.
Pia hukumsikia Lisssu alichoongea bungeni na kwenye mikutano kuhusu Nyerere..
Alijenga hoja kwa namna ipi kiasi kwamba akakosa uungwaji mkono kiasi kikubwa.
Naamini angekosoa jinsi alivyokosoa MALCOM LUMUMBA au walivyo kosoa kitaalamu na kwa staha akina Nyalali Lissu anagepata uungwaji mkono mkubwa.
 
Mimi namkubali sana Tundu Lissu, is exceptionally brilliant japo tatizo lake ni UROPOFU.

FRIJI LA LISSU HALIGANDISHI, yeye kila ambacho kinapita kwenye ubongo wake kinatoka.

Kauli za kusema kwamba Zanzibar ni Koloni la Tanganyika ni kuchochea tu matatizo baina ya watu binafsi kuliko serikali. Zanzibar na Tanganyika, zote kwa pamoja zinatawaliwa na koo fulani zilizojimilikisha CCM. Mtanganyika wa kawaida hanufaiki na huu muungano kiwango cha kusema kwamba anapata faida kubwa kutoka Zanzibari, kwasababu hata pato la taifa hawachangii kubwa kivile.

Baadaye mwaka 2023 akabadilika na kuanza kusema Tanganyika inauzwa na Wazanzibari. Kiharaka unaweza ukahisi kuna hoja kubwa, ila ukweli ni kwamba anachokifanya SSH ni muendelezo wa ambacho kimefanywa na Mwinyi, Mkapa na Jakaya. Maraisi ambao hawakuuza kabisa nchi kwa wageni ni Mzee Nyerere na JPM. Hawa walikuwa na wivu na mali za ummah (They never took advantage).
=====================================================

Mada kama hizi watu huwa hawazielewi kwa kupitia mihadhara, ila wanazielewa baada ya matatizo kuwakuta kama yale ya 29 Oktoba 2025. AU watekwe, waporwe mali zao na kuendelea kufungwa huku uchumi wao ukizidi kuwa mbaya.

WATANGANYIKA watakubali tu ukweli.
NI SUALA LA MUDA TU...
​
 
Katiba mpya yenye serikali 3 ndio mwarobaini wa yote
 
Andiko la kisomi hili. Ubarikiwe sana
 
Kwa hiyo tuendelee kulalamika/kumlalamikia marehemu au tutafute njia bora kujinasua?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…