Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Ma-DJ wakali kabisa wa enzi hizo walikua pamoja katika show Club Africana. DJ Meb, Neagre Jay, DJ Choggy Sly (RiP) , DJ John Peter Pantalakis, mratibu wao Nassoro Born City (RiP), DJ Kalikali (RiP) na DJ Eddy Sally (RiP) ... Masiku yamepita.
Mbona umemuacha Dj Jerry kotto aliyemfundisha kazi kalikali ? Au kwa vile aliwahi kupiga Mbowe club ?Ubaguzi hata kwenye burudani ?
 
Mtazamo wako na ulicho kiandika humu kimekuonyesha jinsi ulivyo.
Mm nakushauri tu watu wanapo jadili jambo ww uwe msikilizaji au msomaji tu.
Kwa aina ya uchangiaji huu na muandiko huu watu wanaweza kujua amendika kadada ka kazi kaliko ishia std 3.
 
Mwinyi aliichukua nchi kutoka kwa Julius K Nyerere, nchi ambayo ilikuwa inayumba kiuchumi kutokana na kutoka kupigana vita ya kumng'oa Iddi Amin dadaa, unategemea hizo huduma mzuri na wananchi kupata chakula bora vingetoka wapi?

Nani aliyekudanganya? Vita ile ya msalaba ilikwisha zamani sana na Tanzania haikuwa na gharama ya kifedha zaidi ya roho za Watanzania na Waganda waliouliwa. Gharama za vita zote zililipiwa na washirika wa msalaba.

Tanzania ilianza dhiki zake miaka 6 baada ya kukabidhiwa madaraka Nyerere, dhiki ilianzia Nyerere alipoanza kudhulumu mali na nafsi za watu alipotangaza azimio la Arusha.

Mwinyi kaikuta nchi hohehahe miaka zaidi ya kumi baada ya vita ya Uganda.

Nyie ndiyo wale hamkuwepo bali mmejazwa ujinga na mnaukubali bila kupepesa.
 

Arabuni ndiyo wapi? Na alimuoa nani?
 
Nasikitikia akili yako kujaa upepo,na unasema husicho kuwa na uelewa nacho masikini ya mungu,huo udini utakukondesha na kubaki kama Skelton
 
Mbona umemuacha Dj Jerry kotto aliyemfundisha kazi kalikali ? Au kwa vile aliwahi kupiga Mbowe club ?Ubaguzi hata kwenye burudani ?
Enzi hizo ukienda Rungwe Oceanic Beach Resort ya Mzee Mwakitwange ulikuwa unakuitana na majina kama vile DJ Ngomely, DJ Pop Juice na wengine. Ukiosea jirani na hapo Rungwe, yaani Silver Sands, unakutana na kina John Peter Pantalakis, Choggy Sly na Kalikali ambaye baadaye alihamia YMCA.Ukienda Africana ulikuwa huangalii simba aliyekuwa anafugwa hapo.

Baada ya Space 1900 discotheque kuhamia YMCA, disko la RSVP Discotheque likazaliwa Mbowe na Ma DJ wake walikuwa mkongwe Saidi Mknadara a.k.a DJ Seydou, akisaidiana na DJ Yaphet Kotto.Kwa ufupi, pamoja na kwamba DJ Eddy Sally na DJ Sweet Francis wa hoteli ya Keys mtaa wa Uhuru walikuwa juu kwa vyombo vya kwanza vya kisasa vya disko, lakini ni DJ Seydou na DJ Yaphet Kotto ambao ndio walikuwa vinara pale RSVP Mbowe. Yaani baada ya kuruka majoka kila sehemu uijuayo, lakini vijana wote wa Dar walikuwa wanakwenda Mbowe kumalizia usiku kwa DJ Seydou na DJ Kotto.Kwa ufupi huyu ndiye aliyekuwa baba wa disko Dar, sio pekee kwa uwezo usio wa kawaida wa kupanga muziki tu bali pia ngekewa ya kupata nyimbo mpya mpya kabla ya DJ yeyote nchini.

Umefurahi??
 
Enzi ya Mwinyi akiwa na Omar Mahita ndio tulishuudia majambazi yakilelewa na Kuibuka majambazi Makubwa akina Alex Massawe e.t.c
 
Tuache ushabiki Mzee Mwinyi aliipokea nchi ikiwa na hali mbaya sana kiuchumi,tulikua hatuna fedha ya kuagiza mafuta na malighafi yeyote kutoka nje,Mwinyi aliongea na wa Iran tupate mafuta nakumbuka hata Mzee Mugabe alitusaidia fedha za kigeni wakati huu uchumi wa Zimbabwe ulikua juu,bila y mageuzi makubwa aliyoyafanya Mwinyi sijui huyo Mkapa angekusanya kodi kutoka wapi?
 


Wengi wao ni watu wa Tanga

Now naelewa why Tanga iliachwa nyuma kimaendeleo

what about YASIN MEMBA?
 
Una hakika na unchokiongea,aliyeongoza hilo vuguvugu ni nani?hao watu wa Tanga ni kina nani tuache ushabiki
 
Huyu mzee alimtoa mtanzania kutoka kuvaa kaniki mpaka,kuvaa katambuga mpaka kuvaa malapa..uchumi huria,demokrasia ya vyama vingi..anastahili pongezi.Alifanya mengi kwa wakati wake.Alikuta nchi ipo ovyo sana imemshinda nyerere mpaka akakimbia urais..wazungu walitaka kumuonyesha wao ni nani.Sadly magufuli anataka kuturudisha Enzi za nyerere tena!
 
Alipokea kijiti cha uongozi wakati nchi ikiwa katika hali ngumu mno kiuchumi.

Sijui kama ulikuwepo kipindi hicho mkuu.

Kama ungekuwepo sijui kama ungeandika hayo uliandika labda kama unaleta ubishi na ushabiki sawa.
athari ya utandawazi ambao wengi wasingeujua kama si Mwinyi ni kuwa watu wabishani tu ili mradi waonekane tofauti kimtazamo hata kama hawana facts. Waswahili wanasema "Asiejua Maana usimwambie Maana". Na kama mchangiaji mmoja alivyosema wengi humu ni Product za after 90's wala usibishane nao.
 
mkuu kula like tatizo humu wengine hawakuwai kupanga foleni kipindi cha unga wa njano na maharage mabovu unayapata kwa foleni
 
Arabuni ndiyo wapi? Na alimuoa nani?
Arabuni ni pamoja ghuba ya uajemi, ukingo wa magharibi pmj na mashariki ya Kati
Mzee mwinyi alijipatia toto la kiarabu safari zikawa hazikatiki huko alimaanusura ndoa yake na siti ivunjike kama si busara za mama Maria nyerere
 
mkuu kula like tatizo humu wengine hawakuwai kupanga foleni kipindi cha unga wa njano na maharage mabovu unayapata kwa foleni
Wengi wao ukiwaambia Mwinyi ama unga wa foleni wanarefer kwenye vitabu vya Historia kwahiyo kwao ni moja tu ya simulizi kama za sungura na fisi. Mbaya Zaidi ndio wengi walio humu ndani na ndio wachangiaji wakuu, inabidi tustahamili tu na kukubali kuwa uelewa wao ndio unaishia hapo.
 
Nimekuelewa mkuu wangu, Mzee Ali Hassan Mwinyi alikuwa na kibarua kigumu cha kufufua uchumi uliokufa kabisa hili watu hawataki kukubali sijui kwa nini.
 
Sasa naanza kuelewa kwa nini kina Hans Pope walitaka kumpindua Nyerere. Mzee alimess up mazima na uchumi wa nchi, na maisha yakawa magumu mno. Kwa hali ilivyokuwa alikuwa hana jinsi zaidi ya kung'atuka tu.
Ingekuwa China sijui wangempa hukumu gani maana huko nasikia wananyonga.
 
Mwinyi aliichukua nchi kutoka kwa Julius K Nyerere, nchi ambayo ilikuwa inayumba kiuchumi kutokana na kutoka kupigana vita ya kumng'oa Iddi Amin dadaa, unategemea hizo huduma mzuri na wananchi kupata chakula bora vingetoka wapi?
Ivi unafahamu Nyerere alianza kuungoza mwaka gani? Na vita ilikuwa mwaka gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…