Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Wewe ndiye unataka kumlinganisha nyerere na alhaji Ally Hasan mwinyi, hiyo haitatokea

Wewe achana na hawa watu. Wanajibishana wao kwa wao ha

Nenda kaangalie "Waraka wa Panama",

Linganisha na orodha ya makwepa kodi ya yaliyoagiza malori kwa ajili ya ibada!.

Tanzania haitakuwa himaya ya mashetani. Rudi kuzimu sehemu uliyoandaliwa miele. Ibilisi!
 

Achana na List ya Panama,
Mahakamani JoPoMa kawapeleka watu wa kutoka pande zipi? Mmejaa kibao.
Tatizo lenu nikuwa mkiwa huko nafikiri pia huwa mnafundishwa na jinsi ya kuiba badala ya kumuabudu Mungu.
Kweli mmebalikiwa mali, ila zote zimejaa damu na dhuruma. Mwendo wenu ni kwa Mwendo wa Nguvu za shetani.
 
Kibaya zaidi matatizo hayo bado yanaendelea mpaka leo.
 
kina Memba wangeteka nyara ndege leo hii na kwenda London kusema maisha ni magumu sana na hali ni mbaya ndiyo maana wamechukua uamuzi huo wangeshangiliwa sana.

Wangeonekana wanaharakati,mashujaa,wanamapinduzi, walioandamana kueleza hisia zao wapambanaji wana uchungu na taifa letu.
 
Naona members wenzetu humu wamekasirika kweli kumuelezea Mzee Mwinyi basi nimeacha maana mpaka wasomaji wanaitwa malimbukeni.
Nini kukasirika, wakiweza hata wafe kabisa. Ukweli utabaki kuwa ukweli. Muslims ndio wakombozi wa nchi hii.
Mwinyi na JK wanaingia katika kundi moja na akina Songea Mbano, Mkwawa, Milambo, Takadir etc
 
Unapomsifia Mwinyi usisahau kuandika pia kwamba yeye kwa kushirikiana na kina marehemu Kolimba alitaka kuibadili katiba ili aendelee kuongoza. Pia usisahau Nyerere ndiye aliyewalazimisha CCM kuingia katika demokrasia ya vyama vingi wakati kamati ya Judge Nyalali ilipotoa matokeo ilisema watanzania 80% wanataka chama kimoja na 20% wanataka vyama vingi. Usisahau pia kampeni za vitisho za CCM kuwa vyama vingi vitaleta maafa. Halafu kuhusu biashara huria hili lilikua wazo la serikali iliyopita ila lilitekelezwa katika awamu ya Mwinyi aliyelianzisha alikua Marehemu Sokoine. Mwinyi atabaki katika Historia kama rais mpole lakini pia Historia itamuhukumu pia kwa kuibadilisha ikulu kuwa dangulo la wezi na ndiye aliyewapa mwanya waliomfuata kuibadili IKULU kuwa kijiwe cha uwizi.
 
Watu wanang'ang'ani alibadili uchumi, mimi najiuliza kama uchumi ulibadilika kwanini bado tupo masikini? Huu ujinga wetu wa kudhani watu wakiwa na TV wameendelea ni wangapi walikua na TV huko vijijini? Kwani maendeleo ya Nchi ynaletwa na kuwa tv?
 
Mkuu tupe darasa lini walitaka kubadili katiba Mwinyi na Kolimba.

Japo Nyerere alijitokeza kuelezea muundo wa vyama vya siasa katika kuunda mfumo wa vyama vingi lakini hayo aliyasemea katika kipindi cha Mwenzie. Katika kipindi chake, Nyerere alipiga marufuku mfumo uliokuwepo wa vyama vingi vya siasa.

Inaposemwa mfumo wa vyama vingi ulirudi tena mwaka 1992, huenda vijana wadogo wanashindwa kuelewa. Ni kwamba Vyama vingi vilikuwepo hadi mwanzoni mwa miaka ya uhuru lakini Serikali ya Nyerere ikavifutilia mbali.

Serikali ya Mwinyi ndiyo iliyorudisha tena mfumo huo hata kama ni kwa shinikizo la Mataifa ya Magharibi. Karibu vyama vyote vikubwa vya Siasa vya Upinzani vilianza shughuli zao katika kipindi cha Mwinyi.

Mwalimu Nyerere aliikebehi serikali ya Mwinyi kuwa ilikuwa inashauriwa na mama Sitti! Kumbe basi wanawake hawana sababu ya kumuenzi Mwalimu Nyerere.
 
Akina Kolimba na Malecela walifanya chini juu kuhakikisha kuwa Mwinyi anatekeleza fikra mpya, na kuachana na zile zilizoshindwa za Nyerere. Madai ya Mwalimu kwamba wanasiasa hao walikuwa wakimshauri vibaya Rais Mwinyi yalitokana na upinzani wao dhidi ya fikra zake.

Huu ndiyo ulikuwa ugomvi wa Nyerere na Kolimba, Malecela.

Unajua Kolimba alikufa mwaka gani?
 
Kweli days never go back..you real get enjoyed in your back to the days
 
Hahaaaaaahaaaaa..umenchekesha mkuu
 
Well said, Mwinyi alituondolea Ile adha ya kupanga foleni kutwa nzima kwa ajili ya kununua kilo moja ya sukari ambayo kwa kipindi cha mwalimu ilikuwa ikiuzwa na serikali tu,

Aidha, alituondolea usumbufu wa kukaa kituoni kutwa nzima kusubiri UDA kwani ktk zama zake wananchi waliruhusiwa kumiliki vyombo vya usafirishaji,

Nguo za kila aina zikaingia nchini, wakina mama wakapumzika kuvaa kaniki na matenge ya kaungua,

Soko huria lilichukua nafasi yake Tanzania na tukaondokana na ujima uliokuwepo awali, ukitaka kumiliki majumba 73 rukrsa, ukitaka kumiliki magari 20 rukrsa, ukitaka kumiliki mashamba heka 100 ruksa!!..... Liberal economy!!!

Mungu ambariki mzee Mwinyi!
 
Well said, upo sahihi kabisa
 
hakusimamia vizuri swala la demokrasia ndio maana hakutaka kubadili katiba ili iendane na mfumo wa vyama vingi!hadi leo katiba ni ya chama kimoja inatoa mwanya wa udanganyifu kwenye chaguzi nyingi
Mwinyi alitakiwa ahakikishe uwepo wa katiba inayoakisi vyama vingi na ushindani sawa wa kisiasa kwa kuwa ndio aliasisi mfumo huo! Pia alitakiwa mali zote zilizokuwa za TANU na baadae kurithiwa na CCM zinarudishwa kuwa za umma na sio kuzibakiza kuwa CCM wakati zilipatikana kwa jasho la watanzania wote bila kujali itikadi zao
Mwinyi alijenga msingi mbaya wa demokrasia ya vyama vingi ambao hadi leo unakinufaisha CCM! Kwa hili simuungi mkono hata kidogo
 
Yeye alikuwa anashauriwa na nani kuwapangisha watu foleni kutwa nzima kusubiri kununua kilo moja ya sukari na unga wa yanga ?
 
Ww Ni muongo kuliko wote kama historia huijui kaa kimya ufunzwe nyerere hakupenda kung'atuka ila alilazimika kutokana nanchi kuwa kwenye hali mbaya kuwahi kutokea watanzania waliteseka sana uchumi ulikuwa negative ukikutwa na kilo zaidi ya moja ya bidhaa ww ni muhujumu uchumi heal ya kuendeshea nchi mwinyi alitoa nje
 
Hakuna historia huo ndiyo ukweli, ila wewe ndo hujui maana unasema Nyerere alizazimishwa kung'atuka, halafu hujajibu hoja yangu kuwa Mwinyi alitaka kubadilisha katibu kwa kumtumia Kolimba. Usibishe kwa jazba na matusi watu hawatakuelewa. Ulichoandika ni hasira zako za kutokumpenda Nyerere. Tunapotaka kujadili tuache mapenzi ya watu wetu ama vyama vyetu tuongelee ukweli....Tanzania ready for multiparty – Mwalimu
Mwalimu Nyerere has stated that Tanzania is ripe for political pluralism and has urged CCM Party leaders to initiate peaceful transition. He told journalists at his Msasani residence in Dar es Salaam that, although the majority of Tanzanians supported the CCM, there was a substantial minority which wanted the constitution changed to allow pluralism. He believed there were serious, patriotic people, some of them inside the CCM, who could form a viable opposition party once permission had been given. However, a sound opposition leadership was yet to emerge, he added Sunday News.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…