Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Wewe ndiye unataka kumlinganisha nyerere na alhaji Ally Hasan mwinyi, hiyo haitatokea

Wewe achana na hawa watu. Wanajibishana wao kwa wao ha
Inawezekana ulipatikana baada ya babako kunywa pombe za kienyeji. Vinywaji vya kienyeji vinaendelea kukulevya mpaka leo.

Angalia kwenye list ya mafisadi watu gani waliopelekwa kwa wingi mahakamani?

Mtake msitake, Mungu akitaka mtaachia tu. Vibakwa wakubwa nyie

Nenda kaangalie "Waraka wa Panama",

Linganisha na orodha ya makwepa kodi ya yaliyoagiza malori kwa ajili ya ibada!.

Tanzania haitakuwa himaya ya mashetani. Rudi kuzimu sehemu uliyoandaliwa miele. Ibilisi!
 
Wewe achana na hawa watu. Wanajibishana wao kwa wao ha

Nenda kaangalie "Waraka wa Panama",

Linganisha na orodha ya makwepa kodi ya yaliyoagiza malori kwa ajili ya ibada!.

Tanzania haitakuwa himaya ya mashetani. Rudi kuzimu sehemu uliyoandaliwa miele. Ibilisi!

Achana na List ya Panama,
Mahakamani JoPoMa kawapeleka watu wa kutoka pande zipi? Mmejaa kibao.
Tatizo lenu nikuwa mkiwa huko nafikiri pia huwa mnafundishwa na jinsi ya kuiba badala ya kumuabudu Mungu.
Kweli mmebalikiwa mali, ila zote zimejaa damu na dhuruma. Mwendo wenu ni kwa Mwendo wa Nguvu za shetani.
 
Ni kweli hawa vijana wengi walikua waislam. Na hata jaribio la pili la kuteka ATC ambalo halikufanikiwa kwani Alikuwemo wale jamaa walibeba maembe yalopakwa rangi na kushtukiwa na Gen Kimario aliekuwemo ndani ya ndege..wale walikua vijana wa kiislam walochoka na sera za kutengwa.
Lakini nini chanzo cha haya ? Kwa ufupi baada ya uhuru ikaja policy ya afrikanazation ambayo iliwatoa wasio wafrika kazini..lakini ukweli ikawa ni chrstinazation ya kazi zote. ..then Ikaja nationalization policy walo umizwa tena ni waislam ndio walojenga mijini na nyumba zao zikataifishwa kwa wingi
Then ikaja azimio la arusha..hapa biashara zikahodhiwa na serikali ..tena waathirika ni waislam ikumbukwe waislam ndio walikua wafanya biashara wenye maduka
Sasa wakawa dhalili sana ndaniya nchi yao...kazi hawamo serikalini , nyumba zao zimetaifishwa, biashara zao zimukufa na charity zao zimepigwa mweleka na hatimae biashara nazo zikataifishwa...maisha yalikua magumu hata mabusati ya kusalia misikitini ilikua hakuna huku wenzao wakiajiriwa katika mashirika yale yalo taifishwa..

Kwa ufupi hapa ndipo ilipo anza kutoaminiana mpaka kesho ...
Hivyo legacy ni pamoja na nani alileta usawa na nani alileta ubaguzi nani aludhulumu raia wake...Mzee mwinyi alikua msafi kabisa kabisa na mwepesi kusamehe katika kujenga umoja na maelewano....
kuna wakati mwalimu aliwahi kuhojiwa kama political prisoners atawatoa jibu alotoa ni jee wameacha kuwa wahaini ? mzungu alichoka...Lakini Mzee Mwinyi wakati tunaingia Vyama vingi akasema tujenge upya nchi yetu tusameheane na akawatoa wahaini ambao walitaka kumpindua Nyerere kutokana na njaa ilozagaa nchini hawa ni kina Hans Pope na wenzake.
Kibaya zaidi matatizo hayo bado yanaendelea mpaka leo.
 
kina Memba wangeteka nyara ndege leo hii na kwenda London kusema maisha ni magumu sana na hali ni mbaya ndiyo maana wamechukua uamuzi huo wangeshangiliwa sana.

Wangeonekana wanaharakati,mashujaa,wanamapinduzi, walioandamana kueleza hisia zao wapambanaji wana uchungu na taifa letu.
 
Naona members wenzetu humu wamekasirika kweli kumuelezea Mzee Mwinyi basi nimeacha maana mpaka wasomaji wanaitwa malimbukeni.
Nini kukasirika, wakiweza hata wafe kabisa. Ukweli utabaki kuwa ukweli. Muslims ndio wakombozi wa nchi hii.
Mwinyi na JK wanaingia katika kundi moja na akina Songea Mbano, Mkwawa, Milambo, Takadir etc
 
Kisiasa, Uongozi wa Mwinyi ulifanikiwa katika mambo makuu mawili; kufunguliwa kwa milango ya demokrasia na Uhuru wa Vyombo vya Habari. Dhana ya demokrasia, japo haikutumika katika chaguzi za kipindi chake, lakini angalau miaka miwili kabla ya kuondoka madarakani nchi ilifungua mlango wa demokrasia ambapo siasa za vyama vingi zilianza wakati yeye akiwa madarakani.Kwa pamoja na Uhuru wa Vyombo vya habari, nchi ikajenga mazingira mapya kutoka yale ya utawala usiokosolewa kuja utawala uliokosolewa hadharani. Kwa mara ya kwanza ikashuhudiwa demokrasia ya Rais kuchorwa na kusemwa vibaya.

Vijana wa Chuo Kukuu cha Dar es Salaam wao walifikia hatua mbaya zaidi pale walipoifuja demokrasia hiyo kwa kuchora picha za matusi dhidi ya Rais Ali Hassan. Kama tutakavyoona katika kipengele cha elimu, Mwinyi alileta nafuu kubwa ya maisha ya Wanataaluma Chuoni hapo.

Japo wanataaluma walianza kuonesha mfano mbaya wa matumizi ya uhuru wa kujieleza ambao haukuwepo enzi za Nyerere lakini bado Mwinyi hakufunga mlango wa demokrasia.

Kwa mara kwanza tangu miaka ya 1960, Watanzania wakaanza kushuhudia majukwaa ya upinzani dhidi ya Chama tawala na serikali. Ukizungumzia mwanzo wa mageuzi ya kisiasa basi lazima utayakuta ndani ya kipindi cha Mwinyi.

Kama kuna eneo lililoung’arisha mapema utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi basi lilikuwa ni lile la Uchumi. Mwinyi aliaswa na wataalamu wa uchumi kuwa aachane kabisa na fikra zilizoshindwa na Mwalimu Nyerere kama alitaka kufanikiwa katika eneo hili.
Unapomsifia Mwinyi usisahau kuandika pia kwamba yeye kwa kushirikiana na kina marehemu Kolimba alitaka kuibadili katiba ili aendelee kuongoza. Pia usisahau Nyerere ndiye aliyewalazimisha CCM kuingia katika demokrasia ya vyama vingi wakati kamati ya Judge Nyalali ilipotoa matokeo ilisema watanzania 80% wanataka chama kimoja na 20% wanataka vyama vingi. Usisahau pia kampeni za vitisho za CCM kuwa vyama vingi vitaleta maafa. Halafu kuhusu biashara huria hili lilikua wazo la serikali iliyopita ila lilitekelezwa katika awamu ya Mwinyi aliyelianzisha alikua Marehemu Sokoine. Mwinyi atabaki katika Historia kama rais mpole lakini pia Historia itamuhukumu pia kwa kuibadilisha ikulu kuwa dangulo la wezi na ndiye aliyewapa mwanya waliomfuata kuibadili IKULU kuwa kijiwe cha uwizi.
 
KIkubwa alichofeli ni KUKUSANYA KODI na ndipo ilimbidi Mkapa alipoingia aanzishe TRA.

RUKSA RUKSA ilikuwa RUKSA kwlei kweli watu walikuwa wanahela mbaya na vitu vilipatikana kwelikweli.( Mfano w ahili ni show ya Kanda Bongo Man ndani ya Kilimanjaro Hotel Miaka hiyo ya 90 kiingilio ilikuwa 100,000/= na bado ilijaza)

Nyerere alimpiga dongo sana kuwa anashahuriwa na Mkewe au tuseme wake zake.
Watu wanang'ang'ani alibadili uchumi, mimi najiuliza kama uchumi ulibadilika kwanini bado tupo masikini? Huu ujinga wetu wa kudhani watu wakiwa na TV wameendelea ni wangapi walikua na TV huko vijijini? Kwani maendeleo ya Nchi ynaletwa na kuwa tv?
 
Unapomsifia Mwinyi usisahau kuandika pia kwamba yeye kwa kushirikiana na kina marehemu Kolimba alitaka kuibadili katiba ili aendelee kuongoza. Pia usisahau Nyerere ndiye aliyewalazimisha CCM kuingia katika demokrasia ya vyama vingi wakati kamati ya Judge Nyalali ilipotoa matokeo ilisema watanzania 80% wanataka chama kimoja na 20% wanataka vyama vingi. Usisahau pia kampeni za vitisho za CCM kuwa vyama vingi vitaleta maafa. Halafu kuhusu biashara huria hili lilikua wazo la serikali iliyopita ila lilitekelezwa katika awamu ya Mwinyi aliyelianzisha alikua Marehemu Sokoine. Mwinyi atabaki katika Historia kama rais mpole lakini pia Historia itamuhukumu pia kwa kuibadilisha ikulu kuwa dangulo la wezi na ndiye aliyewapa mwanya waliomfuata kuibadili IKULU kuwa kijiwe cha uwizi.
Mkuu tupe darasa lini walitaka kubadili katiba Mwinyi na Kolimba.

Japo Nyerere alijitokeza kuelezea muundo wa vyama vya siasa katika kuunda mfumo wa vyama vingi lakini hayo aliyasemea katika kipindi cha Mwenzie. Katika kipindi chake, Nyerere alipiga marufuku mfumo uliokuwepo wa vyama vingi vya siasa.

Inaposemwa mfumo wa vyama vingi ulirudi tena mwaka 1992, huenda vijana wadogo wanashindwa kuelewa. Ni kwamba Vyama vingi vilikuwepo hadi mwanzoni mwa miaka ya uhuru lakini Serikali ya Nyerere ikavifutilia mbali.

Serikali ya Mwinyi ndiyo iliyorudisha tena mfumo huo hata kama ni kwa shinikizo la Mataifa ya Magharibi. Karibu vyama vyote vikubwa vya Siasa vya Upinzani vilianza shughuli zao katika kipindi cha Mwinyi.

Mwalimu Nyerere aliikebehi serikali ya Mwinyi kuwa ilikuwa inashauriwa na mama Sitti! Kumbe basi wanawake hawana sababu ya kumuenzi Mwalimu Nyerere.
 
Akina Kolimba na Malecela walifanya chini juu kuhakikisha kuwa Mwinyi anatekeleza fikra mpya, na kuachana na zile zilizoshindwa za Nyerere. Madai ya Mwalimu kwamba wanasiasa hao walikuwa wakimshauri vibaya Rais Mwinyi yalitokana na upinzani wao dhidi ya fikra zake.

Huu ndiyo ulikuwa ugomvi wa Nyerere na Kolimba, Malecela.

Unajua Kolimba alikufa mwaka gani?
 
Ndugu yangu acha tu, enzi zile za rungwe oceanic, iliyokuwa mali ya Marehemu Mzee Mwakitange. Petty Ray Kasambula na volkswagen yake, nikiisikia tu usiku wa manane najua jamaa anatoka mbowe kupiga muziki. Alikuwepo Marehemu Choggy Sly, alikuwepo mtu anakwenda disco pale YMCA na mwamvuli mkononi akiigiza mbwembwe za wamarekani.
Alikuwepo kaka yake Jack Pemba anaitwa Chuche (nadhani ni marehemu), alikuwa fundi wa kucheza robot na baadae break dance.
Hizo zilikuwa enzi za maisha ya utotoni, marehemu Mama anatoa fedha ya disco toto jumapili mchana, halafu wakati naondoka kuelekea disco namsikia akiniambia usipite "gizani wakati wa kurudi usiku, tembea kwenye mwanga wa taa". Yaani anasema nisipite gymkhana kwenye ule mtaa wa ghana avenue kwa sababu kulikuwa na giza sana usiku. Siku zimekwenda na haziwezi tena kurudi.
Kweli days never go back..you real get enjoyed in your back to the days
 
Uko sahihi Kabisa!!! Nyerere anapiga kelelee Mzee Mwinyi alikuwa na adabu sana hakuwahi kumjibu ila pia hakuwahi kuyumbishwa nae!
Maigizo ya Ujamaa na Azimio la Arusha alitupa kuleee!
Tofauti kubwa ya Mzee Mwny na Marais wengine ni kutokuwa kwake na wapambe na wapishi wake wa Propaganda. Mwinyi pekee ndio Rais ambae hakuwahi kujikweza na kujifaragua kwa majivuno.
Mwinyi kaibadilisha sana hii nchi kutoka Maisha ya ki primitive ya kuamini hata kumiliki friji ya kupoza maji ya kunywa ni kuhujumu uchumi
Hahaaaaaahaaaaa..umenchekesha mkuu
 
Kisiasa, Uongozi wa Mwinyi ulifanikiwa katika mambo makuu mawili; kufunguliwa kwa milango ya demokrasia na Uhuru wa Vyombo vya Habari. Dhana ya demokrasia, japo haikutumika katika chaguzi za kipindi chake, lakini angalau miaka miwili kabla ya kuondoka madarakani nchi ilifungua mlango wa demokrasia ambapo siasa za vyama vingi zilianza wakati yeye akiwa madarakani.Kwa pamoja na Uhuru wa Vyombo vya habari, nchi ikajenga mazingira mapya kutoka yale ya utawala usiokosolewa kuja utawala uliokosolewa hadharani. Kwa mara ya kwanza ikashuhudiwa demokrasia ya Rais kuchorwa na kusemwa vibaya.

Vijana wa Chuo Kukuu cha Dar es Salaam wao walifikia hatua mbaya zaidi pale walipoifuja demokrasia hiyo kwa kuchora picha za matusi dhidi ya Rais Ali Hassan. Kama tutakavyoona katika kipengele cha elimu, Mwinyi alileta nafuu kubwa ya maisha ya Wanataaluma Chuoni hapo.

Japo wanataaluma walianza kuonesha mfano mbaya wa matumizi ya uhuru wa kujieleza ambao haukuwepo enzi za Nyerere lakini bado Mwinyi hakufunga mlango wa demokrasia.

Kwa mara kwanza tangu miaka ya 1960, Watanzania wakaanza kushuhudia majukwaa ya upinzani dhidi ya Chama tawala na serikali. Ukizungumzia mwanzo wa mageuzi ya kisiasa basi lazima utayakuta ndani ya kipindi cha Mwinyi.

Kama kuna eneo lililoung’arisha mapema utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi basi lilikuwa ni lile la Uchumi. Mwinyi aliaswa na wataalamu wa uchumi kuwa aachane kabisa na fikra zilizoshindwa na Mwalimu Nyerere kama alitaka kufanikiwa katika eneo hili.
Well said, Mwinyi alituondolea Ile adha ya kupanga foleni kutwa nzima kwa ajili ya kununua kilo moja ya sukari ambayo kwa kipindi cha mwalimu ilikuwa ikiuzwa na serikali tu,

Aidha, alituondolea usumbufu wa kukaa kituoni kutwa nzima kusubiri UDA kwani ktk zama zake wananchi waliruhusiwa kumiliki vyombo vya usafirishaji,

Nguo za kila aina zikaingia nchini, wakina mama wakapumzika kuvaa kaniki na matenge ya kaungua,

Soko huria lilichukua nafasi yake Tanzania na tukaondokana na ujima uliokuwepo awali, ukitaka kumiliki majumba 73 rukrsa, ukitaka kumiliki magari 20 rukrsa, ukitaka kumiliki mashamba heka 100 ruksa!!..... Liberal economy!!!

Mungu ambariki mzee Mwinyi!
 
Muda mfupi tu baada ya Mwinyi kuingia madarakani na kubadili mtazamo wetu wa kiuchumi, mambo yakaanza kubadilika kiasi cha kuwashangaza watu. Magenge ya ulanguzi yakatoweka baada ya bidhaa kupatikana kwa wingi.

Watanzania wakaanza kufanya biashara na nchi nyingine, waliokwenda Kenya kupeleka machungwa, na wao kurudi na sabani za kufulia na kuogea, waliokwenda Uganda, waliokwenda Uarabuni, Ulaya, Marekani, alimuradi kila mmoja alikwenda alikotaka.

Soko la bidhaa mbalimbali likashamiri. Badala ya watu kutafuta bidhaa, bidhaa zikatafuta watu. Nguo mpya za dukani bwerere, mitumba bwerere, sabuni kibao, fegi hahahah teletele, magari makubwa na madogo kibao, Televisheni kibao, Radio kibao.
Well said, upo sahihi kabisa
 
hakusimamia vizuri swala la demokrasia ndio maana hakutaka kubadili katiba ili iendane na mfumo wa vyama vingi!hadi leo katiba ni ya chama kimoja inatoa mwanya wa udanganyifu kwenye chaguzi nyingi
Mwinyi alitakiwa ahakikishe uwepo wa katiba inayoakisi vyama vingi na ushindani sawa wa kisiasa kwa kuwa ndio aliasisi mfumo huo! Pia alitakiwa mali zote zilizokuwa za TANU na baadae kurithiwa na CCM zinarudishwa kuwa za umma na sio kuzibakiza kuwa CCM wakati zilipatikana kwa jasho la watanzania wote bila kujali itikadi zao
Mwinyi alijenga msingi mbaya wa demokrasia ya vyama vingi ambao hadi leo unakinufaisha CCM! Kwa hili simuungi mkono hata kidogo
 
KIkubwa alichofeli ni KUKUSANYA KODI na ndipo ilimbidi Mkapa alipoingia aanzishe TRA.

RUKSA RUKSA ilikuwa RUKSA kwlei kweli watu walikuwa wanahela mbaya na vitu vilipatikana kwelikweli.( Mfano w ahili ni show ya Kanda Bongo Man ndani ya Kilimanjaro Hotel Miaka hiyo ya 90 kiingilio ilikuwa 100,000/= na bado ilijaza)

Nyerere alimpiga dongo sana kuwa anashahuriwa na Mkewe au tuseme wake zake.
Yeye alikuwa anashauriwa na nani kuwapangisha watu foleni kutwa nzima kusubiri kununua kilo moja ya sukari na unga wa yanga ?
 
Unapomsifia Mwinyi usisahau kuandika pia kwamba yeye kwa kushirikiana na kina marehemu Kolimba alitaka kuibadili katiba ili aendelee kuongoza. Pia usisahau Nyerere ndiye aliyewalazimisha CCM kuingia katika demokrasia ya vyama vingi wakati kamati ya Judge Nyalali ilipotoa matokeo ilisema watanzania 80% wanataka chama kimoja na 20% wanataka vyama vingi. Usisahau pia kampeni za vitisho za CCM kuwa vyama vingi vitaleta maafa. Halafu kuhusu biashara huria hili lilikua wazo la serikali iliyopita ila lilitekelezwa katika awamu ya Mwinyi aliyelianzisha alikua Marehemu Sokoine. Mwinyi atabaki katika Historia kama rais mpole lakini pia Historia itamuhukumu pia kwa kuibadilisha ikulu kuwa dangulo la wezi na ndiye aliyewapa mwanya waliomfuata kuibadili IKULU kuwa kijiwe cha uwizi.
Ww Ni muongo kuliko wote kama historia huijui kaa kimya ufunzwe nyerere hakupenda kung'atuka ila alilazimika kutokana nanchi kuwa kwenye hali mbaya kuwahi kutokea watanzania waliteseka sana uchumi ulikuwa negative ukikutwa na kilo zaidi ya moja ya bidhaa ww ni muhujumu uchumi heal ya kuendeshea nchi mwinyi alitoa nje
 
Hakuna historia huo ndiyo ukweli, ila wewe ndo hujui maana unasema Nyerere alizazimishwa kung'atuka, halafu hujajibu hoja yangu kuwa Mwinyi alitaka kubadilisha katibu kwa kumtumia Kolimba. Usibishe kwa jazba na matusi watu hawatakuelewa. Ulichoandika ni hasira zako za kutokumpenda Nyerere. Tunapotaka kujadili tuache mapenzi ya watu wetu ama vyama vyetu tuongelee ukweli....Tanzania ready for multiparty – Mwalimu
Mwalimu Nyerere has stated that Tanzania is ripe for political pluralism and has urged CCM Party leaders to initiate peaceful transition. He told journalists at his Msasani residence in Dar es Salaam that, although the majority of Tanzanians supported the CCM, there was a substantial minority which wanted the constitution changed to allow pluralism. He believed there were serious, patriotic people, some of them inside the CCM, who could form a viable opposition party once permission had been given. However, a sound opposition leadership was yet to emerge, he added Sunday News.
 
Back
Top Bottom