DAR si LAMU
JF-Expert Member
- Mar 31, 2007
- 2,928
- 551
...Kukiwa na upungufu, bidhaa hufichwa.RTC halikuwa tena shirika la kusaidia wananchi bali lilikuwa ni shirika la kuwatesa wananchi kwani bidhaa zilifichwa kwa makusudi na zikatolewa kwa mlango wa nyuma kwenda mikononi mwa walanguzi.
...Gamba, kumlaumu, hapana. Ila, ukweli ni kuwa ilibidi kodi ikusanywe kwa kiasi hicho hicho kidogo. Mbona baada ya mambo kuwa magumu kimapato ilibidi ikusanywe.Wanaomlaumu Mwinyi kutokusanya Kodi, Ni Tax base gani iliyokuwepo baada ya Mwinyi kuingia Madarakani?, kulikuwa kuna viduka vya Wahindi tu.
...Was this the prevailing policy, then? Are we just assuming?Alichokifanya Mwinyi ni kuwawezesha wananchi wawe na kipato, ili wenye kuanzisha biashara waanze, Then unatoa Tax Incentive kwa kutowatoza kodi ili Biashara zikomae, then Ukishapata watu wa kutosha wa kuwatoza kodi Unaanza kuwatoza kodi.
...Baada ya miaka yake mitano ya mwanzo, nchi ilikuwa imeiva kukusanywa kodi. Mbona hatimae ilianza kukusanywa?Mkapa alipoingia Madarakani angalau aliwakuta watu wachache ambao ni Taxable, ambao walipata utajiri wao kipindi cha Mwinyi. Mzee Mwinyi hakuwa na Privilege hii, alikuta nchi hohehahe na wananchi hohehahe Angekusanya kodi kutoka kwa nani?
...Mchango wako ni wa muhimu.mwinyi alifanya economic reforms na kuja na open up policy kwa kufungua milango ya kiuchumi Tanzania. Hili lilifanywa na nchi nyingi kipindi hicho japo Tanzania ilichelewa sana. China kwa mfano Deng Xiaoping miaka ya 1978 alileta sera hii baada ya chairman Mao Zedong kufariki, na hii ndio inasemwa kuwa ndio Turning point ya uchumi wa China ambayo ilijenga misingi ya maendeleo waliyonayo leo.
Hivyo wakati mwinyi akifungua milango hii kwa nia njema, huwenda hakuwa na wasimamizi na watekelezaji wazuri na bobevu lakini hii ilikuwa ni turufu kubwa sana ambayo pengine Leo tungekuwa tunazungumza mengine. Wakati china ikitengeneza uchumi wa kibepari wenye sifa za kisoshalisti Tanzania sisi tuliingia katika uchumi wa kibepari moja kwa moja! Legacy ya mzee ruhusa ni kubwa sana kwa sababu aliichukua nchi ikiwa katika kipindi kigumu mno cha uchumi uliokufa kabisa kuliko raisi yoyote aliyefuatia baada yake. Ni kama vile alipewa "yatima" amlee ambae hana "nguo" wala "chakula" wala "pakulala". Alijitahidi mno. na ni kipindi hiki ndipo biashara zilianza kuibuka na bidhaa zikapatikana hasa zile bidhaa msingi ambazo wakati wa nyuma zilipangiwa foleni asubuhi mpaka jioni,kuanzia sukari ,nguo,dawa ya meno nk. Kila zama na kitabu chake, kulinganishi kipindi chake na sasa kisha eti kumkosoa kuwa hakufanya kitu ni kutokumtendea haki. Alifanya kwa nafasi yake na kutokana na changamoto za wakati wake. Na laiti waliomsaidia wangemuunga mkono na pia waliofuatia kama wangeboresha zaidi pale alipoachia kwa kuweka sera endelevu na miapango ya mda mrefu, Tanzania ingekuwa "China" ya leo! Hongera mzee mwinyi ulifanya yako kwa wakati wako.
pamoja ni habari kuwa na ukweli kwa 100% lakini imenifuhisha sana hakika nimecheka mpaka machozi yamenitokaBinafsi japo nilikuwa mdogo nimeshuhudia muuza duka akiuawa kwa ngumi moja tu katika harakati za kumpatia huduma mwananchi ambae alihisi anabaniwa kwa wiki nzima!
Jibu swali nimekuuliza vita vya uganda ilikuwa mwaka gani ni ilipiganwa muda gani?Wacha kuuponda uongozi wa nyerere, nyerere alijitahidi sana kwa uwezo wake
1978 hadi 1979 mbona hujauliza madhara ya hivyo vita kiuchumi kwa nchi masikini kama tanzania kipindi hicho viliiathiri vipi?Jibu swali nimekuuliza vita vya uganda ilikuwa mwaka gani ni ilipiganwa muda gani?
...Acha kutukumbusha mambo hayo! Unatuhuzunisha!Ritz, huwa nawatazama hawa watoto wa smart phones nawaona hawana ujanja wowote. Acha tu yaani, tunaongelea enzi hizo za watoto wa Oysterbay kufanya sherehe halafu sisi watoto wa upanga mashariki tunakwenda kwa miguu kwenye nyumba ya mtu fulani. Party ikimalizika kulikuwa hakuna mambo ya boda boda au bajaji, watu wakanyaga kwa miguu taratibu kutoka mitaa ya Obay, wanavuka salender Brigde wanakunja kushoto kuitafuta Aga Khan, wakivuka Gymkhana, yanakuwepo makundi mawili, mmoja linaelekea shaaban robert na jingine linakuwa ni la watoto wa mirambo na ohio kwenye maghorofa ya Railways.
Watu walikuwa wanazifuata party za usiku kwa miguu, lakini walikuwepo wezi wa magari ya baba, wanavizia wazee wamelala, wanaenda gereji wanalisukuma gari taratibu mpaka kwenye kona ya mtaa halafu ndio linawashwa. Mwenye gari mara nyingi hana hela ya mafuta, anafanya kuwaambia marafiki zake wachange ili waweze kwenda na kurudi nyumbani bila ya baba kushtukia mchezo asubuhi ya siku inayofuata.
Vijana wengi waliopanda meli na wale waliotoroka kupitia mipaka ya nchi hii, walifanya hivyo katika miaka ya mwisho ya JKN na ya mwanzo ya AHM. Enzi hizo ndio ulikuwa wakati ambao watoto wa kishua walikuwa wapo tayari kuuza hata masinki, mafriji na magari ili mradi wapate nauli za kuondokea nchini.Kauli za vijana enzi za Nyerere
(1) Sea never Dry - wakimaanisha ipo siku watastowaway wapande meli wakimbie tabu za bongo
(2) One day yes - Wakimaanisha ipo siku watatoka tu
Misamiati ya wanasiasa kabla ya kuja mzee Ruksa
Mtu akiwa na hela au mambo safi ataitwa
Kabaila, Mnyonyaji, Bepari, Bwanyenye
Vita imepiganwa miezi 8 Nyerere katawala miaka 23 kwa faida ya JF tufahamishe athari zake.1978 hadi 1979 mbona hujauliza madhara ya hivyo vita kiuchumi kwa nchi masikini kama tanzania kipindi hicho viliiathiri vipi?
Kumbe ulivyokuwa una shadadia kwa mbwembwe hujui nini na vipi uchumi wetu uliyumba baada ya serikali ya marehemu jk nyerere kugharamia vita ya kumfunza adabu nduli Amini?Vita imepiganwa miezi 8 Nyerere katawala miaka 23 kwa faida ya JF tufahamishe athari zake.
Haya umeshinda ngoja mie nikae pembeni wengine watakujibu.Kumbe ulivyokuwa una shadadia kwa mbwembwe hujui nini na vipi uchumi wetu uliyumba baada ya serikali ya marehemu jk nyerere kugharamia vita ya kumfunza adabu nduli Amini?
Kumbe ulivyokuwa una shadadia kwa mbwembwe hujui nini na vipi uchumi wetu uliyumba baada ya serikali ya marehemu jk nyerere kugharamia vita ya kumfunza adabu nduli Amini?
Tukuulize weweYote hayo aliyataka Nyerere mwenyewe, aliwapa hifadhi waasi wa Uganda Kina Museveni tangu miaka ya Sabini, wakawa wanaleta chokochoko ndani ya Uganda, wewe unafikiri Iddi Amin dadaa kama Raisi wa Uganda angefanyaje?
Kukiri udhaifu ni uungwana piaHaya umeshinda ngoja mie nikae pembeni wengine watakujibu.
Yaani unajiuliza kuhusu legacy ya mzee wa Ruksa? Unajua kwa nini alipachikwa jina hilo ama ulikuwa hujazaliwa?