Uchaguzi 2020 Leila Sheikh: Marekani wana kizabinazabina kwa matamko yao kuhusu uchaguzi wa Tanzania

Uchaguzi 2020 Leila Sheikh: Marekani wana kizabinazabina kwa matamko yao kuhusu uchaguzi wa Tanzania

Leila Sheikh mwanahabari na mtetezi wa haki za wanawake, wakati akishiriki mjadala wa waandishi wa habari uliotayarishwa na radio DW Kiswahili leo mchana ametoa matamko ambayo hata NEC wala viongozi wa CCM hawawezi kutamka moja kwa moja kuishambulia Marekani kwa kuitaja kwa jina zaidi ya kuishia kutaja mabeberu.

Leila akichagia mjadala huo uliohusu waandishi wanavyouona uchaguzi wa Tanzania alionekana kutofautiana na waandishi wenzake kutoka mataifa ya nje kwa jinsi alivyokuwa akiitetea NEC na Rais Magufuli kwa kudai kuwa uchaguzi unaendeshwa kidemokrasia na kuongeza kuwashambulia wapinzani wanaotishia kupeleka wananchi barabarani kama watashindwa.

Alikanusha kutokuwepo uhuru wa habari kipindi hiki cha uchaguzi.
Nilimsikilza Yule mama nikazani ni me mwenyewe ndio skumuelewa nakumuuona mnafiki.kifupi nikuwa hawazezi jieleza kabsa nawala ana point,lakn nkakumbuka kunabaadhi yaredio zilfungiwa kwaajil yakulusha matangazo aya kwamuda flani kwamadai kwamba hawabalance habar.sasa naona sasaiv wameanza kuchukua makada wachama flani ili wasifungiwe tena.kwakua mnasema niteja nmeanza kuamn Sasa maana ata majbu alio kuwa anayatoa ntofauti namaswali aliyokuwa anaulzwa.Ally mutasa alikuwa smart Sana namakini kwenye oja namajbu
 
Wangesusa Ccm wangechukua kila kitu na wala hawajali chochote rejea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana.

Ccm imejimilikisha hii nchi inafanya itakalo na hakuna wakuhoji.
Sawasawa. Je, nini kifanyike kuondokana na hali hii????
 
Kwasasa hivi na haya yanayoendelea hao Wapinzania wanategemea nini?

Yaani mwenyekiti wa tume ya uchaguzi aliyteuliwa na mwenyekiti wa chama, eti amtangaze Mpinzani!

Mkurugenzi ndiye huyo anaeneza ''sera za chama'' badala ya kusikiliza kesi za wagombea na kuratibu uchaguzi

Msajili ndiye huyo anyeona Wapinzani wanaungana, alikuwa likizo CCM na TLP na Cheyo walipoungana

Kibaya zaid, Afisa wa Polisi, msimamizi wa amani anapotangaza 'matokeo kutoka jeshi la Polisi'' kabla ya kura.

Polisi anajua nani kashinda, alichokifanya ni kutamka tu kwa bahati mbaya maazimio ya vikaoni, tena kabla ya siku ya uchaguzi. ''Wewe huwezi kumshida panda gari uondok'', yes ana matokeo tayari mkononi.

Huku makao makuu dana dana za uchunguzi kana kwamba hawana uhakika kama Polisi huyo ana kinywa.

OK! tusubiri

JokaKuu tindo Pascal Mayalla
Nini kifanyike kuondoa haya?
 
Nimesikiliza huo mjadala, huyo Leila Sheikh hata kujieleza kwa ufasaha ni shida. Alikuwa ni kama kada wa CCM zaidi kuliko muandishi wa habari.
Ila angelikuwa upande mumoja wa upinzani ungelimuona bonge la intelligent. Hapo ndo munafeli upinzani.
 
Jaji Radhia mpole sana yule mama wa watu,Hamida nae ni advocate mzuri yuko vizuri ila mkorofi kinoma na umri umekwenda ila mi naipenda ile familia wako vizuri kichwani,enzi zao mtoto wa kike kusoma vile sio mchezo
Wala hufahamu hiyo familia.
Ungeifahamu ungeelewa ukweli.
Acha kuleta chuki binafsi humu.
Tabia ya udayuzz haipendezi kwa mtoto wa kiume.
 
Umekosea.
Siyo shombe la kiarabu.
Ni Mbondei na Mjeremani.

Ni shombe la kiarabu umri utakua umeenda nakumbuka alikua ile Tume ya Ukimwi miaka ya 90s mwishoni au 2000s mwanzoni alimshtaki Mwenyekiti wa Tume Major General Mbogo kwamba alimdharirisha kijinsia bila kusema kivipi
 
Shemeji yake na akina mwapachu ndio wanamuweka mjini hapa dada mmoja hivi kwao Tanga mvuta sigara mzuri,familia yao wamesoma sana kakaa Ulaya miaka kibao karudi na begi la nguo tu,aliwahi kuwa TAMWA au Tawla anakiofisi chake kinondoni kinaitwa calabash studio
Hakika wewe ni mdukuzi ....duh!
 
Ni msimamo mzuri
Leila Sheikh mwanahabari na mtetezi wa haki za wanawake, wakati akishiriki mjadala wa waandishi wa habari uliotayarishwa na radio DW Kiswahili leo mchana ametoa matamko ambayo hata NEC wala viongozi wa CCM hawawezi kutamka moja kwa moja kuishambulia Marekani kwa kuitaja kwa jina zaidi ya kuishia kutaja mabeberu.

Leila akichagia mjadala huo uliohusu waandishi wanavyouona uchaguzi wa Tanzania alionekana kutofautiana na waandishi wenzake kutoka mataifa ya nje kwa jinsi alivyokuwa akiitetea NEC na Rais Magufuli kwa kudai kuwa uchaguzi unaendeshwa kidemokrasia na kuongeza kuwashambulia wapinzani wanaotishia kupeleka wananchi barabarani kama watashindwa.

Alikanusha kutokuwepo uhuru wa habari kipindi hiki cha uchaguzi.

View attachment 1596645

=======
Msimamo wa Leila:

Tunapoelekea Uchaguzi Mkuu 2020: Madai ya Wanawake kuboresha maisha

TUMESIKIZA Ilani za Uchaguzi za vyama kadha vya siasa kwa ajili ya kuomba kura zetu ili tuamue ni Timu ipi tuamue kuikabidhi dhima na dhamana juu ya nchi yetu; rasilimali zetu; mustakabala wa Taifa letu; na ndoto zetu za kuwa na Taifa lenye furaha, amani, maendeleo na maisha bora kwa wote.

Hapa, kura zetu sisi wenye nchi yetu, ndiyo turufu kuu ili tuweze kufanya maamuzi yenye busara ni Timu ipi tuikabidhi nchi yetu.

Sisi wanawake tumeshuhudia gurudumu la maendeleo likisukumwa kwenye mrengo wa Haki Jinsia kwenye hii miaka 5, hapo hapo, tunakumbushia yafuatayo ili tuweze kufikia Malengo ya Taifa ya 2030, yakiwemo:

■ Tunadai kwenye Mpango wa kuinua hali ya uchumi kwa wanawake, pawekwe Dirisha makhsus la wajasiriamali wanawake wa ngazi ya jamii ili wapate mikopo yenye riba ya kiwango cha chini iwezekanavyo, waweze kuwekeza kwenye biashara zao bila kuwa na vikwazo.

■ Tunataka Mafunzo na Stadi za kuendesha biashara na kufanya promosheni ili wawe na stadi za kunadi bidhaa na huduma wanazotoa.

■ Tunataka Masoko na fursa za Masoko ndani na nje ya nchi.

■ Tunataka kuwepo na Dawati la Jinsia kwenye maeneo ya biashara kama kwenye Gulio ili wanawake waweze kutoa taarifa iwapo wananyanyaswa kijinsia.

■ Tunataka elimu jamii juu ya kurasimisha biashara za ngazi ya jamii ambayo ni rafiki kwa wanawake wa ngazi ya jamii.
Kwa sasa, tumeona mrengo unao urasimu, na mafomu ya kujaza mfano TRA ya kulipa kodi ni kwa lugha ambayo wengi wetu hatuielewi vizuri.

Wanawake wafanya biashara wakienda kuulizia jinsi ya kujaza mafomu, wanaambiwa wapate mseja/consultant ambaye wamlipe ili awajazie fomu. Hii haina tija kwa mfanya biashara wa ngazi ya jamii.

Pawekwe Wasaidizi kuwapa msaada wafanyabiashara wa ngazi ya jamii.
Aidha, elimu jamii kupitia redio iongezewe wigo kuweza kufikia wakulima na wavuvi nk.

■ Tunataka Sheria ya Kusimamia Ukatili wa Majumbani/Domestic Violence Act.
Hadi sasa, hatujapata Sheria hii ambayo ni muhimu kuzuia ukatili unaofanyika ndani ya familia, siyo tu miongoni mwa wanandoa au wapenzi, bali hata ukatili dhidi ya wazazi/wazee.

■ Tunahitaji Sera ya Afya ya Uzazi SRH Policy ambayo itatoa Muongozo kwenye mitala juu ya mafunzo ya mabadiliko ya kimwili, ili mabinti na vijana wajitambue. Itaweza pia kuzuia mimba hatarishi za utotoni.

■ Tunataka Rasilimali zetu zinufaishe wananchi hususan, kwenye ugawaji wa:
> Maeneo ya kulima
> Vitalu vya machimbo ya Madini
> Sekta ya uvuvi- wanawake wasiwe wapaaji samaki tu, bali wamiliki mashua za uvuvi, na wasikatazwe kwa kisingizio kuwa wanawake wanaleta 'mkosi' kwenye uvuvi, na kubakushwa kuwa wapaaji samaki. Tuondoe fikra finyu zilizopitwa na wakati.

■ Kiwanda cha kutengeneza taulo za kike za kujihifadhi wakati wa hedhi huko Simiyu kipewe kipaumbele. Tutengeneze pedi kwa pamba yetu; kwa gharama nafuu; na ziuzwe kwa bei ya chini kabisa, kwa mabinti wa shule na wasichana wa vyuo.

■ Ulinzi uongezwe kwenye sehemu za ajira kwa wanawake dhidi ya ngono lazimishi.

■ Elimu jamii juu ya stadi za ukulima na ufugaji kuongeza ufanisi.

Leila Sheikh
Mwanaharakati wa Haki Jamii
Agosti 31, 2020


Leila Sheikh is an award winning author and a documentary film maker.
 
Ulitegemea kasichana, mwanafunzi wa chuo kikuu arudi na mbaula, Cantor, Suzuki?
Karudi na begi moja lenye Jeans 2, t Sheti 3, sketi moja, dera na mtandio wa kusali, na vitabu.
Karudi na B. A. Politics and Government
Karudi na M. A. African Studies.
Karudi na Higher Diploma in Journalism and Film Making.
Na maadili yake na uzalendo wake.
Hakika wewe ni mdukuzi ....duh!,
 
Back
Top Bottom