kipara kipya
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 20,141
- 24,449
- Thread starter
- #101
Miaka yote waliingia kwa tume hii hii endeleeni kumsikiliza kiongozi mkuu mariah sarungi mtafanikiwa..Wewe ni mboga mboga na una chuki zisizo na msingi. Hivi madai ya Chadema kutaka uwanja sawa wa kufanya siasa nalo huoni kama ni la msingi? Hivi kwa mtu mwenye akili timamu anakubaliana na kilichofanyika 2019,2020 na November 2024? Kama kweli Samia anapendwa na amefanya mengi kwa nini anaogopa uchaguzi huru na wa haki? Madai ya Chadema siyo kwa manufaa yao pekee bali kwa hatima ya siasa za nchi kuwe na uchaguzi unaoaminika na kuheshimika. Inapendeza uchaguzi huru na haki anayeshindwa anakubali kiroho safi watu wanapeana mikono kusubiri miaka mitano tena.