Lema anatakiwa aelezwe Simba na Yanga ni zaidi ya CHADEMA

Lema anatakiwa aelezwe Simba na Yanga ni zaidi ya CHADEMA

Wakoloni walikuwa ni wastaarabu. Nakuhakikishia wakoloni wangekuwa jeuri kama hawa viongozi wetu basi wangekuwa na uwezo wa kututawala mpaka sasa. Lema kuji-organize? Hili ni rahisi kulisema kuliko kutenda, ila sisemi umekosea japo linahitaji uwezo na coordination ya hali ya juu. Kwa mfano njia moja ambayo huwa naifikiria ni kupenyeza sleeper cells ndani ya serikali, vyombo vya usalama, tume ya uchaguzi na chama tawala. Hii njia inahitaji usiri na utulivu wa hali ya juu sana na pia muda mrefu.
Lema kusema vibaya Simba na Yanga hivyo tu ni strategic mistake.

Unajua unaweza ukatoa kauli ambayo hata kama ni factually right, bado ikawa strategic mistake.

Kwa sababu michezo ni sehemu muhinu ya kila nchi. Michezo inaingia mpaka kwenye uchumi kuna nchi zinaingiza pesa nyingi za kigeni kwenye michezo. Michezo ina "soft power" mpaka katika siasa za kimataifa. Sasa hivi tunaona Saudi Arabia inafanya jitihada kubwa sana ya kuji rebrand kwa kupitia michezo.

Wiki hii Wakenya wametisha Boston Marathon, dunia nzima inajua Wakenya wanaongoza kwenye marathon. Mkenya akienda popote duniani nchi yake inajulikana kwa sababu ya marathon.

Michezo inatumika mpaka katika diplomasia za kimataifa kuna wakati US na China walikuwa hawaelewani, kukawa na mashindano ya kimataifa Japan, mchezaji wa US akachelewa kupanda basi, wachezaji wa China wakampa lift, ilivyoonekana wachezaji wa US na China wameweza kuelewana na kusaidiana ikapelekea mpaka rais Nixon wa Marekani kufikiria upya Foreign Policy ya Marekani kuhusu China, akafungua mlango wa mazungumzo. Tumeona mambo mengi ya kubadilika siasa na uchumi yametokea hapo.

Kwenye vita baridi mchezo wa Chess ulisaidia sana kuongeza maelewano kati ya Urusi na Marekani.

Namuelewa sana Lema anachosema. Mimi nasoma historia sana. Mshairi wa Roma ya kale Juvenal aliandika kwamba ukitaka kuwatawala watu wa kawaida ambao hawafikirii mambo mengi, wape mkate (chakula) na michezo, circuses (bread and circuses). Naelewa Lema anaongelea kuhusu kupumbazwa kwa watu kwa kuwapiga dozi ya michezo wasijielewe kwenye mambo ya msingi ya nchi.

Lakini pia, tunaweza kushikilia michezo na mambo mengine pia, na si lazima kila mtu adai katiba mpya. Kuna watu hawana interest na mambo ya siasa na wao ni haki yao kupenda michezo bila kunyanyapaliwa. Kulikuwa hakuna haja ya kuzinyanyapaa Simba na Yanga in a false dichotomy fallacy as if watu wakishabikia Simba na Yanga mambo mengine hayawezekani kufanyika, na wasiposhabikia matatizo yetu yataisha. Kuna watu hata wakiacha kufuatilia Simba na Yanga hawataongeza lolote kwenyw siasa, sasa hao kwa nini unataka kuwanyima raha yao ya kushabikia mpira?

We can chew gum and walk.

Watu wanaweza kushabikia Simba na Yanga halafu hapo hapo mambo ya msingi mengine yakazingatiwa.

Lema ni kama ana dude kubwa la kupigana nalo, CCM, anakuwa kalishindwa hilo dude CCM, sasa anatafuta scapegoat wa kummalizia hasira zake, Simba na Yanga.
 
Lema kusema vibaya Simba na Yanga hivyo tu ni strategic mistake.

Unajua unaweza ukatoa kauki ambayo hata kama ni factually right, bado ikawa strategic mistake.

Kwa sababu michezo ni sehemu muhinu ya kila nchi. Michezo inaingia mpaka kwenye uchuni kuna nchi zinaingiza pesa nyingi za kigeni kwenye michezo. Michezo ina "soft power" mpaka katika siasa za kimataifa. Sasa hivi tunaona Saudi Arabia inafanya jitihada kubwa sana ya kuji rebrand kwa kupitia michezo.

Wiki hii Wakenya wametisha Boston Marathon, dunia nzima inajua Wakenya wanaongoza kwenye marathon. Mkenya akienda popote duniani nchi yake inajulikana kwa sababu ya marathon.

Michezo inatumika mpaka katika diplomasia za kimataifa kuna wakati US na China walikuwa hawaelewani, kukawa na mashindano ya kimataifa Japan, mchezaji wa US akachelewa kupanda basi, wachezaji wa China wakampa lift, ilivyoonekana wachezaji wa US na China wameweza kuelewana na kusaidiana ikapelekea mpaka rais Nixon wa Marekani kufikiria upya Foreign Policy ya Marekani kuhusu China, akafungua mlango wa mazungumzo. Tumeona mambo mengi ya kubadilika siasa na uchumi yametokea hapo.

Kwenye vita baridi mchezo wa Chess ulisaidia sana kuongeza maelewano kati ya Urusi na Marekani.

Namuelewa sana Lema anachosema. Mimi nasoma historia sana. Mshairi wa Roma ya kale Juvenal aliandika kwamba ukitaka kuwatawala watu wa kawaida ambao hawafikirii mambo mengi, wape mkate (chakula) na michezo, circuses (bread and circuses). Naelewa Lema anaongelea kuhusu kupumbazwa kwa watu kwa kuwapiga dozi ya michezo wasijielewe kwenye mambo ya msingi ya nchi.

Lakini pia, tunaweza kushikilia michezo na mambo mengine pia, na si lazima kila mtu adai katiba mpya. Kuna watu hawana interest na mambo ya siasa na wao ni haki yao kupenda michezo bila kunyanyapaliwa. Kulikuwa hakuna haja ya kuzinyanyapaa Simba na Yanga in a false dichotomy fallacy as if watu wakishabikia Simba na Yanga mambo mengine hayawezekani kufanyika, na wasiposhabikia matatizo yetu yataisha. Kuna watu hata wakiacha kufuatilia Simba na Yanga hawataongeza lolote kwenyw siasa, sasa hao kwa nini unataka kuwanyima raha yao ya kushabikia mpira?

We can chew gum and walk.

Watu wanaweza kushabikia Simba na Yanga halafu hapo hapo mambo ya msingi mengine yakazingatiwa.

Lema ni kama ana dude kubwa la kupigana nalo, CCM, anakuwa kalishindwa hilo dude CCM, sasa anatafuta scapegoat wa kummalizia hasira zake, Simba na Yanga.
Umedadavua vizuri sana kuhusu diplomasia ya kwenye michezo iran na USA baada ya misuguano na maneno kutishiana kwa muda mrefu hatimaye walikutana kwenye fainal za kombe la dunia 1998 france mpira ukachezwa wamekuja kutana tena 2022 qatar hivyo michezo isidharauliwe kabisa..nani angemjua iddi azan...abassi tarimba ..na wengineo upo sahihi mkuu asilimia zote endelea kutoa darasa maridhawa unarelimisha bila kutumia nguvu...
 
Lema akitaka kuhakikisha Simba na Yanga ni zaidi ya CHADEMA aombe polisi wamchukue Hersi au Mo dewji kama wataweza si kama viongozi wa CHADEMA wanachukuliwa kindezi mbele ya wafuasi wao..

Soma Pia: Lema: Simba na Yanga zinanikera, namuomba Mungu aziondoe mara moja

Wajaribu kuchukua kiongozi wa Simba au Yanga kama atatoka mtu...Chadema ina wapiga soga mitandaoni hawana watu wa kweli ni heri walivyojiondoa uchaguzi kura ilikuwa hakuna.
Ndugu yangu usipoteze muda kumjibu mjinga na mpumbavu kwenye hilo. Achana naye maana ameishajimaliza yeye na chama chake cha Chadema!
 
Nimekusoma vyema nimeheshimu mchango wako ni kweli usemacho ni lazima sheria ziheshimiwe lakini ninachokwazika mimi ni pale wanapo ahidi kuwa watakinukisha na kumjaza upepo muhusika ukifika wakati wa ukweli wote wanabaki kuwa maripota wa kujitegemea...
Hivi brother hadi sasa hujagundua kuwa WAMESHAKINUKISHA?
Yale ya Kariakoo leo ndio hivyo tena kukinukisha! Na wasipojielewa hao watawala, nchi hii isiyo kuwa na ajira thabiti ya vijana basi mambo yanaanza hivihivi kidogo kidogo mwisho ni taabu.
General El Bashir wa Sudan hakuondolewa na jeshi bali raia tena wakiongozwa na mwahaharakati mdogo wa kike Alla Salah aliyekuwa anasomea Uhandisi.
Kuna kitu cha kutisha kinakuja brother, ila kwa vile JF never die kumbuka post hii na utakuja kuniuliza ulikuwa ni UTABIRI au NILIJUA?
 
Kwenye vitabu vya Shivji na wenzake kuna sehemu wameandika jinsi Nyerere alivyopewa ushauri na washauri wake wa siasa kwamba maduka yote yataifishwe, hata maduka madogo ya Uswahilini. Huo ulikuwa ushauri wa wasomi wa uchumi. Lakini Nyerere akautafakari ushauri huo, akaona apate mawazo zaidi. Akamtafuta Mzee mmoja wa Yanga aliyekuwa CCM anaitwa Tabu Mangala. Nyerere akamuuliza Mzee Tabu Mangala, vipi, tutaifishe maduka ya watu ya Uswahilini? Mzee Tabu Mangala akasema chonde chonde Baba usifanye hivyo, hao wasomi hawajui tunavyoishi Uswahilini, sisi ndio tunajua.

Hapo utaona klabu ya Yanga ilitumika kama sehemu ya CCM na serikali kupata habari za chini kabisa kwa wananchi. Na Nyerere alikuwa na washauri wake rasmi wa uchuni, lakini pia alitumia wazee wa CCM waliokuwa kwenye hizi klabu kujua wananchi wanataka nini.

Mwishowe Nyerere aliuacha ushauri wa washauri wake wasomi, akaufuata ushauri wa Mzee Tabu Mangala.

Sasa kama Lema hajaona kuwa Simba na Yanga ni sehemu za kupata pulse ya wananchi, anakuwa hajajua siasa za Tanzania bado.
Mzee Kiranga Hayo yalikuwa ya kale not now! Usidanganywe na hawa wa Kariakoo ya sasa!
 
Ukiachilia mbali siasa,mimi.natamani ningefuta kabisa ligi ni mipira wa miguu apa bongo.imagine watu wanaanza kudiscuss mpira asubuh ata kazi hawafanyi???watu hasa wanaume wanashindwa kudiscuss ni jinsi gani watajiletea maendeleo wanadiscuss mamipira masaa yote???naamini mabadiliko yanakuja na uyo Daudi aliechaguliwa na Mungu atafutilia mbali ligi na mpira
 
Upuuzi mpira ni ajira kama nyingine kama yeyel ema ni mlevi na mzinifu wengine ulevi wao ni mpira..
Mkuu hata Kujamiana ni chanzo cha uzazi na kuongeza familia na dunia, lakini ikitumika vibaya inakua Uasherati na uzinzi na ni dhambi!
Mpira ukiendeshwa kwa namna hii ya Yanga na Simba inageuka kuwa ufala na kama kujamiana kunavyo geuzwa uzinzi na ukahaba!
 
Lema akitaka kuhakikisha Simba na Yanga ni zaidi ya CHADEMA aombe polisi wamchukue Hersi au Mo dewji kama wataweza si kama viongozi wa CHADEMA wanachukuliwa kindezi mbele ya wafuasi wao..

Soma Pia: Lema: Simba na Yanga zinanikera, namuomba Mungu aziondoe mara moja

Wajaribu kuchukua kiongozi wa Simba au Yanga kama atatoka mtu...Chadema ina wapiga soga mitandaoni hawana watu wa kweli ni heri walivyojiondoa uchaguzi kura ilikuwa hakuna.
Mmmh hapo umechapia Mo Dewji alipotea karibu mwezi mzima kipindi cha Jiwe hakuna mshabiki aliefurukuta wala kua na habari nae 😃😀
 
Mmmh hapo umechapia Mo Dewji alipotea karibu mwezi mzima kipindi cha Jiwe hakuna mshabiki aliefurukuta wala kua na habari nae 😃😀
Elewa nilichoandikwa Mo allitekwa kwa kuviziwa akiwa peke yake..Heche na lissu wamechukuliwa kweupe kwenye mikononi mwa wafuasi wa chadema...
 
Mkuu hata Kujamiana ni chanzo cha uzazi na kuongeza familia na dunia, lakini ikitumika vibaya inakua Uasherati na uzinzi na ni dhambi!
Mpira ukiendeshwa kwa namna hii ya Yanga na Simba inageuka kuwa ufala na kama kujamiana kunavyo geuzwa uzinzi na ukahaba!
Sikuwahi kukusikia hata siku moja ukiponda simba na yanga naamini busara zako mshauri mjumbe wa kamati kuu kachemka...
 
Lema akitaka kuhakikisha Simba na Yanga ni zaidi ya CHADEMA aombe polisi wamchukue Hersi au Mo dewji kama wataweza si kama viongozi wa CHADEMA wanachukuliwa kindezi mbele ya wafuasi wao..

Soma Pia: Lema: Simba na Yanga zinanikera, namuomba Mungu aziondoe mara moja

Wajaribu kuchukua kiongozi wa Simba au Yanga kama atatoka mtu...Chadema ina wapiga soga mitandaoni hawana watu wa kweli ni heri walivyojiondoa uchaguzi kura ilikuwa

Mbwa wewe kwahiyo yanga na Simba zitatoa rais na kuundaa serikali?
Daaah kweli watu wanajizima data,hata MWEZI haujaisha Alikomwe si alikamatwa akakaa ndani Singida?
Hao wa makolo si walikatwa mwanza?
Achana nayo Kanjibhai si alitekwa wanathimba walifanya nini?
Na vipi kuhusu manji aliyewekwaga rumande akaja akatoka kama mtu wa kale wanajangwani walikuwa hawajafika nchini?,kuna namna akili yako inawaza makandokando 'bothi '
 
Back
Top Bottom