Lema: Magufuli ogopa wanao kupigia makofi na mapambio wanakupoteza kuwa makini nakushauri kwa mara ya mwisho

Lema: Magufuli ogopa wanao kupigia makofi na mapambio wanakupoteza kuwa makini nakushauri kwa mara ya mwisho

Well said. Kama Hii pesa ya ndege ingepelekwa mchuchuma na Liganga nafikiri by now tungekuwa tushaanza kuona matunda yake. Mpaka Leo huwa nashindwa kuekewa sababu ya sisi kutokuinvest kwenye hiyo miradi miwili.
 
Vianzishi vya investment ni investors wakiona opportunity ya kuwekeza.Ukilala ukidhani serikali itaamka na wazo la kukupa ili uwekeze utasubirina.Dubai mwenye kampuni ya Dubai Inc aliona hiyo.opportunity akaamua kuwekeza hakuna aliyemsukuma kufanya hivyo.Ni yeye binafsi alipata Idea akaifanyia kazi
Tanzania tuna mipori kibao katafute pori moja ushushe Dubai yako serikali Wala haitakuzuia

Fahamu pia, Tanzania population ni zaidi ya 50mil+ na eneo ni zaidi ya laki tisa km za mraba kama sijakosea. Ni ujinga kuwalalamikia wananchi juu ya umasikini na kuzitetea mamlaka, kazi ya mamlaka ni kuzitumia facilities zilizopo pamoja na watu wake kama nguvu kazi kuleta maendeleo.. Unazungumzia, PLAN, ORGANISE, IMPLEMENT, hizo ni kazi za mamlaka iliyopo na mwisho wa siku ni positive results.
 
Hata mh. rais inajua wapiga makofi ni wapuuzi tu ndio sababu aliampa uwaziri mh. Bashe na kuwaacha kina Kibajaji na kina msukuma.
 
Wapiga mapambio watapinga hili ila ndio ukweli, juzi wameenda watalii zanzibar kutoka Urusi watalii 520 na wameenda kwa ndege yao, sijui hizi zetu zitaleta watalii kwa kwenda kuwakusanya kama mabasi ya mwendo kasi? Zitapark wapi labda zikikusanya hao watalii? Hili zinanikumbusha mambo ya zamani biashara ya kuokota wazungu kule Arusha walikuwa wanaita fly catcher, nadhani ndio mpango wa kigwangala huu.
 
Uzuri mmoja huu uzi ipo siku utakuja kufufuliwa hata kama ni miaka 20 ijayo
 
Maskini inauma sana, namuona mtoto wa Marehemu Mawazo akimteleta Lema kikombe cha Juice & Maji...RIP Kamanda Mawazo... Mapambano bado yanaendelea....
 
Lema wala wewe hamkutoa statistics zozote zaidi ya mashirika ma4.

Angola na nchi kibao zimefanikiwa mko aware nazo?

Ndiyo maana nasema tujifunze kuwa marafiki na tuache kuvamia mambo tusioyajua.

Naona baadhi ya watu wanatetea sana nchi za watu kukua kiuchumi, mfano umetaja Angola hakuna kitu nimeishi na raia wa Angola wanaishi nchi za watu kwa kutumia kivuli cha ukimbizi. Wanamafanikio gani? Na ndiyo maana watanzania wanazidi kufa masikini kwa ajili ya matumbo yenu na kutafuta madaraka. Kumbe hata madaraka yemyewe huyawezi. Tuangalie hiyo Angola: Ukiwauliza mbona umemaliza masomo hujarudi nyumbani Angola anasema hawezi kurudi kwa sababu ya chuki na ubinafsi uliopo nchini mwao.

Nchi nyingine Afrika ni Rwanda Burumdi Kongo n.k. Uganda wameanza kurudi sasa hivi nao walikuwa hawarudi. Wakenya wakifanya thiess yao tayari wanatiketi mkononi kurudi kwao.

Na sisi watanzania tusikubali kuiendesha nchi yetu kibinafsi kichuki kifitina kisifa kudharau kukwazana na kipambepambe. Tunaomba watu waipende nchi yao. Watu wa ccm acheni kusoma wiki media tafuteni marafiki wa nje na watu wa nchi husika.

Dhamira yangu ni kuondoa mifano inayotolewa bila kuwa na uhalisia.

Watanzania tushikamane bila chuki na tupambane mpaka watupe ile katiba yetu mpya. Waliyeificha mungu atawaumbua tu tena hadharani.

Nawaambia wasijiamini sana kwa sababu wana Jeshi, Mahakama, Mahabusu n.k. Kuna siku mungu atawapa wananchi Mkuu wa majeshi na ataitoa hiyo katiba mpya iliyoandaliwa kwa ajili ya nyakati iliyopo iwasadie vijana wetu.

Ile ya nyakati iliyopita ya kurekebisha na mdomo na kuwa sheria siku hiyo itapelekwa uwanja wa Taifa na kuizika rasmi.
 
Mheshimiwa Lema, kwanza nikupongeze sana kwa ushauri makini unaoutoa kwa watawala na unaonyesha ni jinsi gani upinzani una watu smart wanaoweza kusaidia nchi hii kimawazo na kivitendo siku wakishika dola.

Hata hivyo,pamoja na pongezi hizi,nakushauri yale yote uyasemayo katika video, uyaweke pia katika maandishi ili kuwawezesha watu wengi zaidi kufahamu unachosema na kushauri kwani video clip zinakula MB nyingi hivyo kuna uwezekano watu wengi wakashindwa kupata kwa ukamilifu yale yote unayoyasema au kushauri.

Hongera sana kwani unaonyesha upinzani ni mkusanyiko wa watu smart sana katika nchi hii.

Umeendelea kunifanya nijivunie kuwa mshabiki wa siasa za upinzani.
Kwa kweli huwa sichoki kumsikiliza huyu mbunge. His ideas are very constructive. I don't know why other people don't see important of criticising a leader in a positive manner.
 
Kagame huwa anamlipa Tony Blair consultation fee katika maswala ya uchumi. Msionekane Rwanda inasonga mbele.
Na mkewe Tony blair ni mwanasheria naona hua anamsaidia PK na mambo yake ya kisheria huko nje.
 
Mkuu umejibu vizuri, ila naomba kwenye kuhusu bangi naomba ufute kauli yako. Una uhakika gani kwamba Lema kauli zake zinahusiana na bangi. Nani kakuambia bangi ni mbaya, naomba uache huu mmea wa Mungu usiuhusishe na mambo ya kisiasa.
Mbona wapo wasiovuta bangi wana akili mbovu sana, mnashindwa kuwalaumu walevi wanahatarisha afya zao mna kazi ya kulaumu bangi, wewe ni miongoni mwa watu wasio na akili, mmeakalilishwa kuwa bangi ina madhara, ntafutie evidence yoyote kuwa bangi ina madhara, zaidi sana mnawakamta wavuta bangi na kuwaua, mnashindwa ku verify madhara yake.
Ukinijibu usijibu kwa nyodo, jibu kama huvuti bangi.
Wazee wa kuokoteza hoja Kama kawaida yenu, mnachokiona AMBACHO hakigusi wananchi moja kwa moja Ni ndege tu?

Vipi kuhusu Treni ya kati, (Tanga-Moshi), vipi kuhusu kurudisha nidhamu utumishi wa umma, hatusemi zahanati, elimu bure inawapenga kina nani? Hivi Kuna SGR, au Mradi wa Rufiji, labda angegusia pia sekta ya madini, au upanuzi wa bandari ya dar es salaam gati 0-8.

Sasa mnajikita kwenye kuokoteza okoteza yule Mwami juzi/Jana kaja na sabotage ya bandari ya bagamoyo ooh wakenya wameshinda hakushangilia tulivyowanyang'anya Mradi wa bomba la mafuta la Hoima-Tanga, mbona husemi kwamba Tanzanite Sasa hivi haiuzwi nje ya Mererani.


Mnachojua Ni kuzua na kuzusha tu.

Kuna habari pafu moja la bangi linakaa miaka 40 kichwani sasa Lema ndio kwanza hata yeye mwenyewe ana 40+ toka azaliwe na keshakula Misumari mingapi.
 



Asante sana Mbunge Lema umenena mambo mazuri sana. Hata mimi , kama nimekuelewa vizuri, naona maendeleo ambayo yako nchini ni maendeleo ya vitu na sio maendeleo ya watu na ambayo sio future ya watanzania.

Rais Magufuli ana tuaminisha sisi kuwa analeta maendeleo ya watu. Wakati ukweli sio hivyo. Maendeleo yanayo letwa na Rais wetu naona yanaelekezwa zaidi kwenye vitu zaidi badala ya watu.

Katika utalii naona Waziri Kigwangala bado hajajua strategy ya kuiwezesha nchi yetu kuwa na watalii wengi. Ndege peke yake sio solution. Brain wash ndiyo solution. Nisameheni kwa kulitumia hili neno kwa makusudi.

Nimesha wahi sema mara nyingi sana kuwa kuwatumia ma Stars kama Willy Smith na Prominent persons kama Rais Obama na Prince William wanao kuja likizo na familia zao, kama njia ya kuwa vutia watalii, hiyo haita work hata mara moja.

Kama tunataka kuwatumia prominents ili kuutangaza utalii wetu, basi hatuna budi kuwa wabunifu. Kwa mfano; tunaweza mtumia Willy Smithy, akiwa kama agent anayezuia biashara ya meno ya tembo, katika filam ambayo tumeibuni sisi wenyewe inayo husu kuuawa kwa Tembo wetu na majangili kwa ajili ya biashara ya meno ya tembo, tuseme nchini China, na Rais Obama akawa kama Rais wa Amerika anaye shirikiana na Willy Smith kutokomeza biashara hiyo ambayo ina athiri wanyama na Mbuga zetu.

Filim hiyo ikiwa na mafanikio na ikionyeshwa kwenye cimemas zao na kwenye Videos na Media nyingine kama Youtube, hapo ndipo watu wengi watataka kuja kwetu.

Niwape mfano, ile filim ya King Lion, ime wafanya wazungu wengi wajue kuwa kuna nchi anaitwa Madasca na lugha ya kiswahili kwa upande mwingine kujulokana.

Njiani nyingine ambayo ni muhimu sana, ni njia ya kiwatwanga wazungu kwa matangazo ya mbuga zetu kwenye Media zao kama BBC, CNN, CNBC, Al Jazeera na kadhalika.

Tofauti tuliyo nayo ukilinganisha na maendeleo ya wachina ni kwamba wachina wana produce manufactured goods zilizo kuwa designed na wenyewe na nyingine kuwa designed nje, wakati sisi bado tunategemea agricultural products na madini yetu ambayo bado hayajaanza kutuingizia faida tunayostahili.

Hayo madege anayo yanunu na mabasi ya mwendo kasi akiondoka walakini wa kufa ni mkubwa sana. Labda tumpate kiongozi mwingine ambaye atakuwa kama yeye ili kuendeleza aliyo pacha

 
Wazee wa kuokoteza hoja Kama kawaida yenu, mnachokiona AMBACHO hakigusi wananchi moja kwa moja Ni ndege tu?

Vipi kuhusu Treni ya kati, (Tanga-Moshi), vipi kuhusu kurudisha nidhamu utumishi wa umma, hatusemi zahanati, elimu bure inawapenga kina nani? Hivi Kuna SGR, au Mradi wa Rufiji, labda angegusia pia sekta ya madini, au upanuzi wa bandari ya dar es salaam gati 0-8.

Sasa mnajikita kwenye kuokoteza okoteza yule Mwami juzi/Jana kaja na sabotage ya bandari ya bagamoyo ooh wakenya wameshinda hakushangilia tulivyowanyang'anya Mradi wa bomba la mafuta la Hoima-Tanga, mbona husemi kwamba Tanzanite Sasa hivi haiuzwi nje ya Mererani.


Mnachojua Ni kuzua na kuzusha tu.

Kuna habari pafu moja la bangi linakaa miaka 40 kichwani sasa Lema ndio kwanza hata yeye mwenyewe ana 40+ toka azaliwe na keshakula Misumari mingapi.
Mzee baba je na pama lake kala pafu ngapi? Msanii wa gazeti la sani aliona mbali kumtengeneza Pimbi kama one of the characters.
 
Kenya wako active Sana sababu kampuni zao za utalii ziko active Zina branches ulaya na Marekani kusaka watalii .Sisi kampuni zetu za utalii hata ukiuliza mwanachuo wa chuo kikuu au afisa wa serikali hata hazijui.Na ukimuuliza ukitaka kwenda Mfano kutalii mbugani utatumia kampuni gani hajui .Kampuni zetu za utalii zipo zipo tu

Issue sio waziri au serikali ni ujinga wa kampuni zetu za utalii na kutokuwa active
Uko sahii mkuu. It is just a matter of Generation. Watanzania hatutaweza kwa sababu ya tradion yetu. Rais wetu anafikiri watanzania wana uwezo wa kuwaza beyond their limit, kitu ambacho hajui ni kwamba watanzania peke yao hawata weza. Na pia hawawezi kubadilika mara moja itachukua muda mrefu sana mpaka wao kuja kujitambua.

Nimesha toa mifano mingi sana humu kiasi kwamba nimechoka, Rais wetu hataki kuamini kuwa watanzania peke yaobila ushirikiano na Diaspora, hawataweza kuleta mabadiliko ambayo Rais anayategemea kutoka kwao. Serikali inatakiwa iweke mikakati kabambambe ya kuwawezesha Diaspora kuleta utaalam wao nyumbani. Njia ni nyingi. Ni kiasi tu cha kuwauliza wenzetu walio pata maendeleo ya haraka hivi punde kama china, wamefanyaje kuleta maendeleo yao kupitia diaspora?

Rais wetu ana ona ufahari jinsi anavyo uonyesha ulimwengu jinsi gani Tanzania ni Tajiri. Utajiri sawa, lakini unatakiwa tujue jinsi ya kuutumia kwa manufaa yetu na kizazi cha baadae.
 
Wazee wa kuokoteza hoja Kama kawaida yenu, mnachokiona AMBACHO hakigusi wananchi moja kwa moja Ni ndege tu?

Vipi kuhusu Treni ya kati, (Tanga-Moshi), vipi kuhusu kurudisha nidhamu utumishi wa umma, hatusemi zahanati, elimu bure inawapenga kina nani? Hivi Kuna SGR, au Mradi wa Rufiji, labda angegusia pia sekta ya madini, au upanuzi wa bandari ya dar es salaam gati 0-8.

Sasa mnajikita kwenye kuokoteza okoteza yule Mwami juzi/Jana kaja na sabotage ya bandari ya bagamoyo ooh wakenya wameshinda hakushangilia tulivyowanyang'anya Mradi wa bomba la mafuta la Hoima-Tanga, mbona husemi kwamba Tanzanite Sasa hivi haiuzwi nje ya Mererani.


Mnachojua Ni kuzua na kuzusha tu.

Kuna habari pafu moja la bangi linakaa miaka 40 kichwani sasa Lema ndio kwanza hata yeye mwenyewe ana 40+ toka azaliwe na keshakula Misumari mingapi.
mataga mnasifu, mnaimba mapambio, na kupiga makofi. Mbona Lissu alipigwa risasi mkashangilia na kufurahi na mkamtukana mkidhani angekufa..? Mbona wabunge na madiwani wa upinzani waliunga mkono juhudi mpaka mkaweka muda maalumu wa kuunga mkono juhudi? Mbona mlikataa kuwa ruge na seth ni wezi na mkaimba mapambio sana enzi zile na sasa nyienyie mnasifu na kupiga makofi.....
 
Hiyo sector ya utalii inahitaji watu smart kwenye Brain sio aina ya Kigwangale,

wa Kenya bado watatawala kwenye hiyo sector paka pale tutakapo pata kiongozi ambaye is bussiness oriented......
Business oriented kama Lazaro Nyalandu mzee wa kutorosha Twiga wetu siyo?
 
Sikatai alichokisema mtaalamu wa masuala ya utalii, kitu ambacho yeye hajamwelewa Lema ni kuwa je, lazima iwe Dreamliner ya US $ 262 milioni katika kuboresha sekta ya anga? Je, isingetosha ndege ndogo za abira 50 mpaka 70 kwa safari zetu za ndani na majirani zetu? Kwa bei hiyo ya Dreamliner mbili tungeweza pata ndege ndogo ngapi?

Kama unayajua mahesbu vizuri gharama za manunuzi ya hizo ndege mbili ukijumlisha na gharama za uendeshaji wake, sidhani kama faida za ajira zitakazo patikana na mafanikio ya hizo sekta alizo zitaja zitaweza leta kipato kikubwa kwa taifa. Kama faida ambayo imepatikana mpaka sasa ni kiasi cha US$ 14 milion itachukua miaka mingapi mpaka hiyo Air line iweze kujiendesha yenyewe na kutuletea mapato.

Usafiri wa anga humu ndani kama kwenye mbuga zetu za wanyama na tourist attractions nyingine nchini na labda nchi jirani kama Zambia, Zimbabwe, Burundi, Malawi na DRC, ni sawa kabisa tuna uhitaji usafiri wa anga, lakini sio kwa ndege kubwa za masafa marefu kama Boeing 787. Za nini?

Biashara ya usafiri wa anga duniani imekuwa na ushindani mkubwa sana kiasi kwamba mashirika ambayo zamani yalikuwa yakitamba kama Swiss Air na Air Italia yamebidi yasalim amri na kuform Synegy na Lufthansa, sembuse sisi na vindege vyetu viwili?

Off course, hata mimi ninampongeza Rais Magufuli kwa kulifufua shirika letu la ndege na tunatambua how important it is, katika sector ya utalii nchini kuwa na ndege zetu wenyewe, lakini kwa maoni yangu, angeweka mkazo katika kudumisha usafiri wa anga wa ndani kwanza kabla ya kupapatikia nje.

Unajua kitu ambacho nyie watanzania wengi msio wajua wazungu walivyo, hamwelewi, ni kwamba mnafikiri wazungu wako kama sisi, isipokuwa ni rangi tu, wakati ambapo ukweli wa mambo ni kwamba wazungu hawako kama sisi kifikra hata kidogo.

Naomba hapa niweke wazi kidogo kwa watanzania msio wajua vizuri wazungu, mzungu generally anamwoogopa sana mtu mweusi kuliko kuliko hata mnyama mkali. Hiyo iko kwenye genes zao! Sielewi sababu ni nini? Mtake msitake wako hivyo. Na ndiyo maana hawataki sisi tuwe na maendeleo kama wao. Hawataki sisi tuwaongoze wao.

Nawaomba sana watanzania wenzangu tusi weweseke na wazungu tunao waona Afrika aidha kwa kuishi au kwa kuja kuzuru, hao wachache wao watakuwa wamesha jitambua, lakini wengi wao wanajilazimisha au wanakuja kwa madhumuni fulani. Sasa unategema mzungu kama huyu apande ndege ya Air Tanzania ambayo hajawahi kuisikia maishani mwake hata mara moja kwa hiari? Endeleeni tu kucheza na kufanya masihala na wazungu. Sooner or later mtapata majawabu yake.

Air Malaysia yenyewe ina wawia vigumu kuipanda sembuse Air Tanzania? Mimi nimesha panda mara kadhaa Oma Air kutoka Berlin kuja Afrika, kutoka Berlin mpaka Muscat ndege zilikuwa mara zote karibu tupu pamoja na bei poa. Kwa nini?

Ningependa kumshauri Rais Magufulih hizo hela kuzitumia katika miradi ambayo ingekuwa na direct impact kwa vijana wetu wasio na ajira ambao wanahangaika na biashara za umachinga mijini na kublock barabara za waenda kwa miguu.

Fly overs, mahospitali, viwanja vya ndege na mabarabara ajenge tu, lakini asisahahu kuwa weka watanzania fit kwa maisha ya kesho katika teknolojia za kisasa. SGR, STIEGLERS GORGE na pia upanuzi wa bandari yetu sio vitu vibaya, ni mawazo mapana sana ambayo sina budi kumpongeza sana, lakini tunahitaji zaidi, kwani challenges ambazo zinatukabili in the near fueture ni kubwa sana kuliko hizo projects mbili kubwa.

Watanzania wengi wanahitaji, wajerumani wanasema; "Beschäftigung"=employment! Au tuseme shughuli za kufanya ili watu waweze kujiingizia kipato cha kuwawezesha kuishi na kufanya mambo mengine. Nasikitika kusema uchuuzi peke yake wa umachinga hauta leta employment kubwa sana na kuwafanya watanzania kuwa mabilionea kama Rais mwenyewe anavyo sema. Hata akina Mo na wafanya biashara wengi wakubwa Tanzania wana watu walio soma. Hawafanyi biashara zao bila know how! Mo mwenyewe amesomea uchumi.

Tuna hitaji projects kubwa kama SGR kumi na ziwe sustainable.

Zaidi ya hayo ningetaka kudokeza kitu kidogo, hili Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira au kitengo cha mazingira NEMC kingepata wizara yake. Kwa wenzetu walio endelea wizara hii ina watu waziri sana katika mambo ya kutafiti wa mazingira kwa ujumla.

Kama wizara ingeweza kufanya utafiti kabambe na ku initiate projects ambazo kwa upande mmoja kuleta matokeo ya kweli ya utafiti wa mazingira na upande mwingine kutoa ajira nyingi kwa watanzania.

Watu wengi ambao wamebobea katika meteorology, Ardhi, misitu, maji safi na maji taka wangekuwa kwenye hii wizara na kuwa na ubora wa kuleta mabadiliko ya kweli na ku preserve mazingira kwa ufanisi zaidi.
 
Back
Top Bottom