Nitofautiane na Lema, Mange haamasishi maandamano bali anawaelekeza watanzania njia mojawapo ya kudai haki ni pamoja na maandamano hasa kwa trajectory ya siasa za sasa za kitanzania kila mtu kabanwa kooni njia pekee ni maandamano tu.
Watanzania wamejitahidi kufanya cancelling culture kwa wasanii , Simba na Yanga na wengine walioshirikiana na wauaji ila wameshindwa hivyo maandamano na migomo ndio njia sahihi hii tumeona hata enzi za chama kimoja kule Kenya , KANU baada ya Moi kuvifuta vyama vingine na kubadili sheria wananchi kupigania haki walibaki na majukwaa mawili ambayo ni midahalo ya chuo kikuu na maandamano ambapo watu kadhaa walikamatwa na kufukuzwa chuo na wengine tuliwapokea hapo Tanzania UDSM wakamalizia masomo yao kama Prof Makau Mutua na wengine wakiwemo wakufunzi na wanataaluma kama Ngungi wa Thiong'o , Willy Mutunga, Prof Anyang Nyon'go ,Elisha Atieno Odhiambo, na wanafunzi wengine kama Miguna Miguna ambao waliomba hifadhi ya muda mfupi Tanzania kabla ya kupokelewa nchi nyingine na kwenda kumalizia masomo yao.
Sasa Tanzania midahalo ya kisiasa vyuo vikuu naambiwa imefutwa kwa sasa kauli ni moja uchawa kwanza ukiwa CHADEMA wewe ni mhaini /gaidi.
Media ziko hoi, mashirika ya haki za binadamu yanaitwa yanafadhiliwa na mabeberu kuchfaua nchi hivyo maandamano ndio karata ya mwisho kufanya madikteta wasikie tumeona hili katika nchi nyingi tu duniani.
Mange yuko sawa kuwakumbusha watanzania kwa kuwapa civic education njia zipi ni sahihi kwa sasa kudai haki yao na ukitaka kuamini maandamano yana nguvu ya mabadiliko ndio maana yakitangazwa policcm wanajaa na mabunduki mitaani na hiyo ndio indicator wananchi wanatakiwa watambue nguvu yao kwamba wao wana nguvu kuliko madikteta na si vinginevyo.