Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Kuchukia serikali mara nyingi huwa ni ukosoaji wa approach ya serikali kwenye mambo mbalimbali. Na actually, kuichukia serikali au lichama fulani haiwezi kuwa sawa na himizo la kuchukiana wananchi wenyewe kwa wenyewe!
Yoyote yule anaweza kuwa na makosa iwe serikali, iwe polisi, iwe hata mwanchi wa kawaida. Hatuwezi ku control human emotional. Lakini chukulia sample hata hapa JF, utapata picha watu walivyo jijengea chuki moyoni kwaajili ya kitu kidogo kinachoitwa"siasa". Mtu anadiriki kusema yeye anaichukia CCM na wana CCM wote, na kusema haitakuja kutojea yeye kuwa na ndugu mwana CCM. Huyo kweli anaelewa maama ya siasa ya vyama vingi? Anaelewa kwamba siasa ya vyama vingi ni kipinga kwa hoja badala ya personal attack?
 
Huwezi ukamtukana, kumvunjia Heshima, Au kumdharau Rais,Mwenyekiti wa chama cha hao wabunge, Halafu
hao wabunge waje kukupongeza au kukusalimia kwa mbwembwe!!
Hii inaonyesha na wao wapo kundi moja la kumdharau Rais na Mwenyekiti wao wa chama.

Yote na yote Pongezi kwa kujua huyu ni Mh Rais
safi sana
naona sasa umeanza kujitambua.
Lema Magufuli ndiye Rais wa Tanzania kwa sasa
umpende usimpende ndiye Rais wako,
Jaribu kuwa Na Heshima kwa Mamlaka
Kwahiyo rais na yeye analipiza kisasi?
 
ukikosoa serikali unawekwa na serikali kwenye kundi la maadui wake!. wapinzani wanalo awamu hii..........
Utaratubu wa kukosowana mbona upo wazi? Mkosowe mtu bila kumtuka au kumzalilisha. Huu ni utaratubu wetu wa miaka mingi sana. Lakini watu wanataka kuchukuwa taratibu za nchi zingine za kutukanana hadhari na kuzileta kwetu. Mbona Zitto anaikosowa serikali kila siku na bado yupo uraini.
 
Kamanda pole sana na karibu. Wapinzani kwa namna Moja ama nyingine tunawaomba mshikamane sana katika kipindi hiki. Aliyoyatabiri Tundu Lissu Leo yanatimia. Nchi IPO chini ya dictatorship.Katumieni bunge lenu tukufu kufanya yaliyo mema dhidi ya kauli chafu za Rais huyu

Mkuu hizi kauli kama zitafuatwa na hao wana CCM zitamea na upande wa pili nao watajibu kwa vitendo ,na mwisho wa siku hatuna tena Taifa moja..Yale yale ya Wahutu na wa Tutsi kuuwana kwa sababu ya mbegu ya ubaguzi...

Raisi amefanya jambo la ajabu sana na la aibu dhidi yetu sisi Wananchi ,amekwenda kinyume kabisa na Katiba kinyume kabisa na hulka zetu kama Watanzania..
 
Yoyote yule anaweza kuwa na makosa iwe serikali, iwe polisi, iwe hata mwanchi wa kawaida. Hatuwezi ku control human emotional. Lakini chukulia sample hata hapa JF, utapata picha watu walivyo jijengea chuki moyoni kwaajili ya kitu kidogo kinachoitwa"siasa". Mtu anadiriki kusema yeye anaichukia CCM na wana CCM wote, na kusema haitakuja kutojea yeye kuwa na ndugu mwana CCM. Huyo kweli anaelewa maama ya siasa ya vyama vingi? Anaelewa kwamba siasa ya vyama vingi ni kipinga kwa hoja badala ya personal attack?
Mkuu unataka tuchukue sample ya watu wanaoandika hapa JF kuwa "haitatokea wawe na ndugu wana CCM" tuiingize kwenye mjadala wa hoja ya Rais kukataza wabunge wa CCM kwenda kumsalimia mbunge mwenzao wa upinzani akiwa CCM? Huoni kama sample yenyewe ni uwongo na ni rahisi kugundua kuwa anayeandika hivyo anakuwa anaandika tu kujifurahisha maana jambo lenyewe haliwezekaniki!
 
Mh. Lema umeandika vizuri, ila umemalizia kwa woga sana. Sasa kama kila mtu anaanza kumwogopa hivyo, hadi nyie wabunge, sisi wananchi tutafanyaje. Kumplease mtu pasipohitajika ni udhaifu sana.
Ndio shida ya kukimbia shule na kujifanya mnajuwa Kingereza wakati hata kiswahili hujui.

Umesoma shule gani wewe hujui hata fasihi andishi?
 
Tunaomba utuwekee hukumu ya Court of appeal na High court iliyokupa dhamana. Hizi ni kesi muhimu kwa kila mmoja. Please and please.
Serikali wajanja sana. waliondoa rufaa yao ili kuzuia hukumu isisomwe na isiingie kwenye rekodi za mahakama na kurejewa katika mashauri na kesi zingine
 
Hoja hapa sio kosa bali ni upendo. Unachanganya msingi wa hoja.

Mwenye mamlaka ya kusema kuna kosa limetendeka ni mahakama.

Mwenye mamlaka ya kupenda au kutopenda ni wewe au mimi bila kusubiri maoni/mawazo ya mtu wa pili lakini kikubwa zaidi, kupenda na kupendwa sio one way traffic

Nyie jamaa aisee mna roho mbaya sana na zimeendelea kuwa ngumu kwel kweli tangu mlipokula rambirambi zetu
 
Hivi Luwasa alienda ktk msiba bagamoyo? Maana wengine tupo chochi, network mpaka tupande juu ya miembe.
 
Utaratubu wa kukosowana mbona upo wazi? Mkosowe mtu bila kumtuka au kumzalilisha. Huu ni utaratubu wetu wa miaka mingi sana. Lakini watu wanataka kuchukuwa taratibu za nchi zingine za kutukanana hadhari na kuzileta kwetu. Mbona Zitto anaikosowa serikali kila siku na bado yupo uraini.
neno tusi ni subjective, anaye vunja sheria na ahukumiwe kwa mujibu wa sheria na si kuelekezana namna ya kukosolewa!
 
Mh Rais Magufuli nakusalimu.

Nimetoka Magereza hivi karibuni ambako nilikuwa huko kwa zaidi ya miezi minne kwa kunyimwa masharti ya dhamana kwa dhamana iliyokuwa wazi.

Mh Rais, nimeona kwenye vyombo vya habari leo kuwa kwamba wale Wabunge waliokuwa wanataka kunisalimia nilipokuwa Magereza kuwa ni wasaliti wa chama cha CCM, Mh Rais wengi walinisalimia, Wachungaji, Masheikh, Wabunge na Viongozi mbali mbali, sidhani kama hatua hii ilikuwa ni usaliti isipokuwa upendo ambao ni muhimu kwa binadamu yoyote haswa wakati wa matatizo.

Mh Rais, nimeogopa sana kwa kauli hii yako, je Taifa linakwenda wapi, hivi kweli sisi Wabunge ni maadui? Kama viongozi tutafikiri utengano ni moja ya njia ya kuimarisha vyama vyetu, basi bila shaka tutakuwa tunalitendea Taifa ubaya .

Dhambi hii ikikomaa basi ni hakika kwamba lugha za udini, ukanda na ukabila hazitaacha kukomaa, ni muhimu sasa tukajenga utamaduni wa kuhimiza mshikamano wa Kitaifa bila kujali itikadi kama kweli tunawapenda masikini na wanyonge wa nchi hii.

Nawaomba Wabunge wenzangu walionijali wakati niko magereza wasijisikie vibaya kwani walifanya jambo jema na muhimu kwa wakati muhimu sana katika maisha yangu, ninatarajia kuwa Spika wa Bunge atatoa kauli juu ya kauli yako.

Mh Rais wakati wa Msiba wa Christina Lissu dada yake na Mh Tundu Lissu nilikuona katika msiba ule wewe na Mama yetu Mke wako, je Mh Rais na wewe ulikuwa unasaliti Chama chako?

Mh Rais neno la Mungu linasema, Wapendeni maadui zenu, waombeni wanaowauzi , wabarikini wanaowaonea kwani kufanya hivi ni kuishi kwa thawabu za Mwenyezi Mungu.

Mungu akubariki sana, natumaini Mh Rais sitakamatwa leo kwa ujumbe huu mfupi.


Godbless J Lema (MB)

Godbless umefika muda wa wewe mwenyewe kujitathmini. Siasa haijawahi kuwa uadui katika nchi hii mpaka pale wewe ulipoziumba na kuziimarisha siasa za namna hiyo kwa maneno yako. Godbless jiulize kwani wewe ndio mbunge wa kwanza wa upinzani nchi hii?Jiulize pia kama kweli ktk jimbo lako kuna matatizo yanayokufanya wewe ufanye siasa zinazofanana na za kimapinduzi. Godbless haujawa muangalifu ktk kauli zako, huwafikirii Waka huwahurumii wananchi wako wala wa taifa kiujumla unapotoa kauli zako. Unafahamu frustrations zao, badala y'all kuwapoza na kuwabadili mtazamo ili watumie changamoto zilizopo Kama fursa wewe sasa unazitumia hizo kama silaha yako ya kujiimarisha kisiasa, kujiimarisha katika ajira yako bila kujali athari zinazoweza kutokea kwa wewe kufanya hivyo. Nasema bila kupepesa macho ya kuwa nilikuwa mfuasi wako kipindi kile cha mama Batilda Buriani. Baadae siasa zako zikaanza kunikifu, MA ukweli kuwa kuna watu wengi ndani ya chama chako siasa zako zimewakinai. Kuna mmoja yeye aliipenda katiba ya wananchi kwa kitu kimoja kikubwa, ukomo wa ubunge. Ukomo wa ubunge kwake ungefanya jambo moja kubwa, kumuondoa Lema Arusha, kuondoa image mbaya ya chama. Yakupasa Godbless ufahamu kuwa hakuna namna moja ya uongozi inafaa nyakati zote, namna kadhaa za uongozi zinaweza kufaa nyakati tofauti kulingana na mahitaji. Kiongozi anayeangalia maslahi makubwa ya nchi itamlazimu wakati fulani kutumia staili ya Machiavelli kulinda ustawi wa watu wengi dhidi ya kijana mmoja mjinga na mbinafsi asiyetosheka na kikubwa alichopata ukilinganisha na uwezo wake. Taswira y'all siasa unayoijenga Godbless si tu italeta uadui kati ya chama tawala na upinzani, italeta pia uadui kati ya wenye kujishughulisha na kupata na wale wanaoaminishwa matatizo yao na kukosa kwao kumetokana na wao kuonewa. Waambie ukweli Godbless, hakuna anayewaonea, wanajionea wenyewe. Juzi alikuwa Mkapa, jana Kikwete na leo Magufuli. Mbeya wanaonewa na manispaa, arusha nao manispaa, ubungo wataonewa na manispaa, ilala halikadhalika. Kigoma ujiji malalamiko hayaishi. Serikali yenye kuleta maendeleo inahitaji watu wafanye kazi ili walipe kodi hakuna uongo mwingine unless udanganye watu, utukane system ya Machiavelli ifanye kazi
 
Huku Mhe. Rais anapotupeleka tulishatoka huko enzi za ukoloni za divide and rule.


Hata wabunge wa CCM wana uhuru wa kuamua kumtembelea mgonjwa, au aliyeko mahabusu ambaye sio wa chama chao, kama hawavunji katiba ya nchi wala chama chao. Isifike wakati mkashindwa hata kuzikana kisa tofauti za kiitikadi.
Waliotangulia hawakutufundisha hivyo.

Mungu yuko nawe Mhe. Godbless J Lema .
.....
.....Mkuu za siku salimia Makamanda wote Arusha Preta kapotea sana Salute Mingi sana
 
Back
Top Bottom