Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Halafu mtu anasimama na kusema Magufuli anafata nyayo za Mwl.Nyerere. Mwl. Nyerere alituunganisha watanzania wote,hakukua na ukabila,udini wala utengano wa kiitikadi wa kivyama. Ila zile juhudi zote za Mwl.Nyerere uyu anaziharibu.
 
Ujumbe Muhimu sana. Ni na uhakika watu wake wameuso na kumfikishikia. Binafsi niliogopa sana niliposikia hii kauli kutoka kwa Mh. Rais wa Jamhuri.

Kwetu sisi Roman Catholic,kuwatembelea wafungwa/mahabusu kunaongeza rehema na baraka zaidi. Hapo naona Rais anataka kuwafundisha watu matendo gani ya huruma wafaanye. Mbinguni kila mtu ataenda peke yake. Asitake kuwafanya watu watende dhambi ya chuki kwa maslahi yake binafsi.
Hapo kwenye red mkuu umenena vyema kabisa, na wakati huu wa mfungo wa kwaresma tunahimizwa sana kutenda matendo ya huruma kama hayo ya kutembelea wafungwa, wagonjwa, yatima n.k pamoja na kusali bila kuchoka. Sasa najiuliza huyu mtu huwa anasoma Biblia gani hiyo inayomwelekeza kulipiza kisasi? Biblia gani inasema jino kwa jino? Naomba nihitimishe kwamba mtu huyu ni mgonjwa wa akili na anapaswa kupimwa kabla hazija-crack zaidi akiwa hapo jumba kubwa anaweza kujikuta ameagiza majeshi yetu yaende kumpiga Uhuru Kenyatta huyu! Tafadhari wataalam wa psychiatry wafanye kazi yao haraka sana bila kuchelewa. Hivi anasali wapi huyu? Na hapa napenda niwape makavu Maaskofu wangu wa Katoliki, hivi hamwoni kwamba mtu huyu anaenda kinyume na mafundisho ya Bwana Yesu Kristo pamoja na yale mnayotuhimiza makanisani kila siku za misa takatifu? Kwa nini mmepigwa ganzi kumhubiria mtu wenu mnamwacha anaangamia hivi hivi? Hizi double standards mnazitoa wapi? Hivi kuna uwezekano kwa matendo haya na nyie mkaiona mbingu kweli?

Hebu tuache unafiki, mtu huyu aambiwe kwamba anaenda kinyume na Ukristo na ikiwezekana azuiliwe kukomunika kabisa. Kila wakati mnatuhimiza tutubu na kuhubiri upendo wa Kristo mbona mnaogopa kumkemea mtu huyu? Hamwoni kwamba Yesu wa Earisti anawekwa kwenye Tabernacle iliyochafuka? Naamini kama angekuwa Mkristo wa kawaida akawa anayatenda haya hadharani namna hii angekuwa ameshafungiwa kukomunika! Tutafakari kwa pamoja Wakatoliki wenzangu!! Na mtu huyu namwomba "ATUBU NA KUIAMINI INJILI!!" Injili inahubiri upendo ambayo ni amri kuu aliyoiweka Bwana wetu Yesu Kristo. Kama yeye mwenyewe alivyosema amri kuu ni "Upendo" (mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa akili zako zote na nguvu zako zote) na ya pili yafanana na hiyo nayo ni "mpende jirani yako kama nafsi yako mwenyewe". Utasemaje kwamba unampenda Mungu wakati huo una kinyongo na majirani zako? JIRANI YAKO NI NANI?
 
Imarisha chama chako peke yako, hakuna mshikamano wa kitaifa wenye itikadi moja .kilichokupeleka mahabusu ni shutuma za kisiasa si vingine. vinginevyo hata me ningekuja kukuona sio mbaya kichaa wangu unajua naboeka sana ninapoiicheki ile movie yako ya homosex.
 
Mkuu wa nchi amesahau kuwa yeye na wapinzani wote ni watoto wa baba mmoja,amesahau kuwa yeye ni Rais kwa sababu katiba yetu imetamka kutakuwa na cheo cha urais katika nchi yetu,amesahau kama katiba aliyoapa kuilinda inaitambua Jamhuri ya muungano wa Tanzania kama ni nchi inayofuata mfumo wa vyama vingi vya siasa.Tuzidi kumwombea tu Rais wetu maana kunatatizo la msingi hapa
Unaiombea akili au mtu mwenyewe.. Ref mithali 26...
 
Mh Rais neno la Mungu linasema, Wapendeni maadui zenu, waombeni wanaowauzi , wabarikini wanaowaonea kwani kufanya hivi ni kuishi kwa thawabu za Mwenyezi Mungu.

Mungu akubariki sana, natumaini Mh Rais sitakamatwa leo kwa ujumbe huu mfupi.


Godbless J Lema (MB)

Sijui Mtukufu, Shabiki wetu mkuu sana Gwajima anapitaga JF? hili ni funzo zito
 
Kauli anazotoa raisi wa tz kwakweli zinafanya raia wajue kwamba huyu ni raisi wa ccm zaidi kuliko tz
 
Ujumbe Muhimu sana. Ni na uhakika watu wake wameuso na kumfikishikia. Binafsi niliogopa sana niliposikia hii kauli kutoka kwa Mh. Rais wa Jamhuri.

Kwetu sisi Roman Catholic,kuwatembelea wafungwa/mahabusu kunaongeza rehema na baraka zaidi. Hapo naona Rais anataka kuwafundisha watu matendo gani ya huruma wafaanye. Mbinguni kila mtu ataenda peke yake. Asitake kuwafanya watu watende dhambi ya chuki kwa maslahi yake binafsi.
Tena mbaya zaidi iki ni kipindi cha Kwaresma, kipindi ambacho haya matendo ya huruma yanatakiwa kuonyeshwa kwa vitendo na mbaya zaidi nilimwona Mh. Rais amefunga mikono akiomba siku ya Majivu, siku ya kuanza rasmi mfungo wa Kwaresma. Sasa sijui alipakwa majivu na kufunga na kusali ili apigwe picha au yote yalitoka moyoni. Mh. Rais kama Mkatoliki mwenzangu nimejisikia vibaya kuona anahubiri uadui kipindi hiki ambacho Mwokozi Yesu alikufa msalabani ili nasi tukombolewe
 
Tuhubiri amani na upendo muda wote hata kama kuna watu wametoa kauli zinazoonesha tofauti.
 
Karibu sana kamanda. Nimefurahi kukuona tena hapa . Mungu azidi kukulinda
 
Naiunga mkono kauli ya Mh Rais kwani si busara kwa mbunge wa ccm kwenda kumfariji mbunge wa upinzani aliyewekwa ndani kwa uchochezi dhidi ya serikali ya CCM. Huo ni usaliti mkubwa na akibainika hatua kali zichukuliwe. Hivi huyu mbunge wa CCM akifika anakuambia koma uchochezi au pole umeonewa.

Muktadha wa kuhudhulia msiba au sherehe ya arusi ni tofauti na ilivyo kwenye kesi ya Lema. Mfano Lema awe na kesi ya kujeruhi iliyotokana na misuguano ya kijamii na kukosa dhamana hapo hata mwanaccm akienda kumfariji akuna shida kabisa.

Mh Rais kafanya vizuri kuwaeleza wabunge wa ccm kuwa imara kukitetea chama chao kwa hali na mali wala wasijirahisi kwa sifa za kijinga mitandaoni. Mbunge wa ccm anatoa muda wa kuchangia bungeni kwa mtu wa chadema wakati mle bungeni silaha kubwa ni kutoa hoja. Wabunge wangapi wa ccm Mara walitaka kuongea halafu yeye kwa kunogewa mahaba anatoa muda.
 
Yani umuombee mwenzio kifo then unahitaji upendo kutoka kwake!sio bure utakua umechanganyikiwa.
 
Anaandika Mkurugenzi Mtendaji LHRC Helen Kijo-Bisimba.

Nimesoma ukurasa wa mbele gazeti la Mwananchi la leo. Siamini Rais Amesema haya kama ni kweli tuko pabaya .

Upinzani si uadui.Kwa hiyo wabunge wasijuliane hali. wakiugua wasitembeleane wakifiwa wasifarijiane? Kama tumefika huko hatuhitaji kuwa na mfumo wa vyama vingi. nilidhani mfumo huu ni wakutuwezesha kuwa na uwajibikaji zaidi si wakuleta uadui. Ninajua Wabunge akiwemo Rais alipokuwa mbunge wamekua wanapingana kwa hoja ndani ya Bunge, wakitoka ni wamoja. Kauli hii kama ni kweli haikupaswa kutoka kwa Rais aliye baba wa wote. Ninaamini wabunge hawataipokea hii.

My take ==Raisi amewaonya wabunge wa CCM waliokuwa wamepanga kumtembelea mbunge mwenzao Godbless Lema gerezani na ameita kitendo hicho kama usaliti mkubwa kwa CCM.
Raisi mara nyingi husema yeye ni wa wote ,maendeleo hayana chama,tudumishe amani na upendo maana Tanzania ni moja,lakini Tanzania itakuwa moja kwa mtindo huu wa kupandikiziana chuki??

Tuzidi kuliombea Taifa.Na wengine tunazidi kukata tamaa.Mungu saidia.
 
Katika kile kinachoonesha sasa siasa ya bongo ni vita na uadui, Rais na mwenyekiti wa chama aliwaonya wajumbe kwa kumwambia mbunge aliyetaka kwenda kumuona Lema gerezani kwamba huo ni sawa na usaliti.
 
Ni active member lakini sio verified user, na hawezi kuwa verified kwani hana uwezo kujenga hoja kwenye uwanja huru. Anaweza kujenge hoja na kejeli anapokuwa mbele ya polisi na vyombo vingine vya dola. Umewahi kumuona kwenye midahalo zaidi ya kuhutubia kama kasisi?
Taratibu kaka... Bado nakihitaji sana tu
 
Kumbe jamaa ana roHo mbaya kiasi hiki?.
Nadhani atakuwa anajutia hayo maneno yake,ninaomba tumsamehe jamani uwe mpinzani ama mwana CCM.
 
Back
Top Bottom