Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Kama "Tuna imani na mtu fulani" inamuuma mpaka leo, tutegemee nini hasa!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkuu wa nchi amesahau kuwa yeye na wapinzani wote ni watoto wa baba mmoja,amesahau kuwa yeye ni Rais kwa sababu katiba yetu imetamka kutakuwa na cheo cha urais katika nchi yetu,amesahau kama katiba aliyoapa kuilinda inaitambua Jamhuri ya muungano wa Tanzania kama ni nchi inayofuata mfumo wa vyama vingi vya siasa.Tuzidi kumwombea tu Rais wetu maana kunatatizo la msingi hapa
Mh Rais Magufuli nakusalimu.

Nimetoka Magereza hivi karibuni ambako nilikuwa huko kwa zaidi ya miezi minne kwa kunyimwa masharti ya dhamana kwa dhamana iliyokuwa wazi.

Mh Rais, nimeona kwenye vyombo vya habari leo kuwa kwamba wale Wabunge waliokuwa wanataka kunisalimia nilipokuwa Magereza kuwa ni wasaliti wa chama cha CCM, Mh Rais wengi walinisalimia , Wachungaji , Masheikh, Wabunge na Viongozi mbali mbali , sidhani kama hatua hii ilikuwa ni usaliti isipokuwa upendo ambao ni muhimu kwa binadamu yoyote haswa wakati wa matatizo.

Mh Rais , nimeogopa sana kwa kauli hii yako , je Taifa linakwenda wapi , hivi kweli sisi Wabunge ni maadui? kama viongozi tutafikiri utengano ni moja ya njia ya kuimarisha vyama vyetu , basi bila shaka tutakuwa tunalitendea Taifa ubaya .

Dhambi hii ikikomaa basi ni hakika kwamba lugha za udini ,ukanda na ukabila hazitaacha kukomaa , ni muhimu sasa tukajenga utamaduni wa kuimiza mshikamano wa Kitaifa bila kujali itikadi kama kweli tunawapenda masikini na wanyonge wa Nchi hii .

Nawaomba Wabunge wenzangu walionijali wakati niko magereza wasijisikie vibaya kwani walifanya jambo jema na muhimu kwa wakati muhimu sana katika maisha yangu , ninatarajia kuwa Spika wa Bunge atatoa kauli juu ya kauli yako .

Mh Rais wakati wa Msiba wa Christina Lissu dada yake na Mh Tundu Lissu nilikuona katika msiba ule wewe na Mama yetu Mke wako , je Mh Rais na wewe ulikuwa unasaliti Chama chako ?

Mh Rais neno la Mungu linasema , Wapendeni maadui zenu , waombeni wanaowauzi , wabarikini wanaowaonea kwani kufanya hivi ni kuishi kwa thawabu za Mwenyezi Mungu .

Mungu akubariki sana , natumaini Mh Rais sitakamatwa leo kwa ujumbe huu mfupi .


Godbless J Lema (MB)
 
Halafu hichi ni kipindi cha kwaresma na jamaa anajiita mroman. Jaman mapdri acheni unafiki mwambieni ukwel
Mapadrii wapi hao wa kumwambia yule mtu bado sijaona atakayeweza nyanyua mdomo wamseme
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hatua ya mwisho kutoka dikteta uchwara kuwa dikteta kamili ni kulazimisha kila unachosema kiwe ndo alfa na omega hata kama ni kupandikiza chuki kwa jamii mzima.
 
Kinachowauma team wema aka ukawa ni magu kuwapa makavu live!
mambo ya kuwabembeleza kama watoto wadogo enzi za jk hakunaga, mtalialia lakini juice ikulu mtaisikia kwenye bomba!
tunataka upinzani wenye akili unafanya aina ya siasa kulingana na wakati!!
 
May God bless Godbless Lema.
Anatukana raisi na mkuu WA mkoa halafu analia kuwa apendwe nyooooooo .upendo ni Two way traffic. Yu hate the police or mahakama they will hate you. You hate the government it will hate u. Lema mind your lips
 
Sidhani kama ana Muda wa ziada kufanya mambo ya Kijinga kama hayo Urais ni kazi ngumu sana.
Tunafuatilia wanaoosha magari pale central sembuse wanaozungumza? Urais ni kazi ngumu kwenye nchi za watu si Tz.
 
Anatukana raisi no mkuu WA mkoa halafu analia kuwa apendwe nyooooooo .upendo ni Two way traffic. Yu hate the police or mahakama they will hate you. You hate the government it will hate u. Lema mind your lips
Heshima ya kiongozi inatakiwa kutokana na huduma yake kwa umma si police wala vitisho.any way this is Tz
 
hakika mwenyekiti wa CCM amejitia aibu kubwa kwa kupandikiza chuki za kichama.

May God bless Godbless Lema.




Mh.Rais wa ccm(nitatolea maelezo kwa nini namuita rais wa ccm)yupo sahihi kuwaita waliopanga kwenda kumuona Lema gerezani kuwa ni wasaliti.Kama kitendo cha Mh.Lema kunyimwa dhamana na kupelekea kusota mahabusu kwa miezi minne kulitokana na agizo lake,ni sahihi kabisa kwa yeye kuwaita wasaliti wale wote waliotaka kwenda kinyume na agizo lake la kuhakikisha Lema ananyimwa haki yake ya kupata dhamana.

Ndiyo,kukiuka maagizo halali ya kiongozi wako ni usaliti,na dawa ya msaliti ni kumpa adhabu inayolingana na usaliti wake.Ikiwa Mh.Lema alishikiliwa kwa maelekezo toka juu kama ilivyojulikana tangu awali,kitendo cha wabunge wa ccm kujipanga kwenda kumuona mtu ambaye kiongozi wa chama na serikali ameelekeza anyimwe dhamana huo ni usaliti wa dhahiri.

Sasa ni dhahiri Taifa lipo njia panda,ikiwa kiongozi mkubwa wa nchi(rais)anawaona kuwa watu waliopanga kwenda kumjulia hali mwenzao aliyepo matatizoni kuwa ni wasaliti,anatoa fundisho gani kwa wananchi wake?Kwangu mimi huyu si kiongozi wangu,kumuita kiongozi ni usaliti kwa nafsi na dhamiri yangu iliyomkataa tangu awali,huyo ni rais wa wale waliomchagua tu,tusiomchagua tukimuita rais tutakuwa tunazisaliti dhamiri zetu zilizomkataa kama ambavyo yeye anaona kitendo cha mwanaccm kumpa pole mwanaChadema kuwa ni usaliti.

Sasa naanza kuwa na mashaka makubwa sana juu ya miili ile iliyozikwa pale mto Ruvu kwenye makaburi ya Sandarusi.Yawezekana maiti wale hawakuwa wahamiaji haramu,bali walikuwa ni wasaliti wa mtawala wetu na ndiyo maana hawakuwa na namna yoyote ya kuulipa usaliti wao zaidi ya kifo.

Viongozi wetu wa kiroho wanapaswa watufundishe sala mpya za kuuombea utawala huu na mtawala wetu,siku zote huwa anasisitiza na kuomba aombewe bila kuweka wazi aombewe ili apate nini kupitia sala zetu,kama hitaji lake ni kupata roho ya chuki,hasira na visasi ili aweze kuwaona wanaolia pamoja na waliao ni wasaliti,basi suala/dua hiyo ni mpya na viongozi wetu wa kiroho wanapaswa kutufundisha namna ya kuiomba dua hii tukufu inayomuwezesha mtawala wetu kuuona mshikamano wa kijamii na hali ya kujali utu wa mwenzako kuwa ni usaliti.

Twaaaaafa!
 
Unapenda sana shari.Jifunze kuutawala mdomo wako na si mdomo ukutawale wewe.Utarudi kisongo.
 
Kama kawaida yetu chadema kuendeshwa kwa matukio...la baishite limewatoa sasa mmepata kauli ya Rais mmepata pa kutokea...

Suala la kuhubiri upendo ni la kila mtu....sio la Magufuli peke yake. Huwezi kujifanya bingwa wa kutabiri kwa kumsemea kifo Rais halafu acheke kwa kufurahi kuwa 2020 atakuwa amekufa...hii kauli mbona machademaa hamkuipinga?

Ni wazi chadema na wanachama wenu mmekuwa mkionesha chuki ya dhahiri kwa viongozi wa CCM kiasi cha kuingilia faragha zao kuwa Makonda kwanini hajapata mtoto na kumkejeli kwa kukosa mtoto wakati ni kazi ya Mungu kukupa mtoto au la....huu ni upendo?

Kuna watu wenye chuki kama nyie? Mtu akirudisha mapigo kwa njia ileile mnatoa mapovu.

Halafu kuna anaye wazidi kwa kauli mbovu hasa Lemaa....mtu unaongea kama sio kiongozi bana. Okey, nashukuru naona umetoka getezani walau ukiwa umejifunza kitu. Basi uendelee hivyohivyo na kuhubiri upendo na sio chuki.

Wananchi tusiwahubiri kana kwamba tunaishi jahanamu wakati hio Serikali unayotukana ni watu kama wewe....wanakasirika na uwepo wa demokrasia hauwazuii kukasirika.

Tuhubiri upendo, mshikamano na umoja. Masuala ya watu wanayonena ndani ya vikao vyao hayatuhusu. Labda kama statement hio Rais angeizungumza hadharani....
 
Rais hajiamini bado Kwamba ndiye Rais, Kauli ya msukuma yule mbunge wa Geita ina maana kubwa sana,Tulishauri huyu mtu CCM Msimpe uenyekiti wa Chama mkatuona wajinga,Mkakubali Tulishauri mtu asiwe na kofia mbili mbona yeye ni Rais,Amir jeshi mkuu na ni mwenyekiti wa CCM.Ilitosha awe Rais na Amir Jeshi mkuu Mbona USA inawezekana?

Kikwete Aliliona hili,Baada ya Askofu Gwajima kutumwa kuwatisha ule upande wa pili wakanywea ila mpango ulikuwepo,

Mnakumbuka Kikwete alipoombwa asalimie wajumbe wa mkutano mkuu,Alisema ahaaaaa sisi ni wazee kama hivi mkitualika tutakuja lakini haya mambo mengine ni yenu,jua hapo kuna shida.
 
Hakuna hata upande wenye afadhali sio CCM wala Chadema wote ni yaleyale tu bado tuna safari ndefu sana kwenye ukomavu wa kisiasa.
 
Mh Rais Magufuli nakusalimu.

Nimetoka Magereza hivi karibuni ambako nilikuwa huko kwa zaidi ya miezi minne kwa kunyimwa masharti ya dhamana kwa dhamana iliyokuwa wazi.

Mh Rais, nimeona kwenye vyombo vya habari leo kuwa kwamba wale Wabunge waliokuwa wanataka kunisalimia nilipokuwa Magereza kuwa ni wasaliti wa chama cha CCM, Mh Rais wengi walinisalimia, Wachungaji, Masheikh, Wabunge na Viongozi mbali mbali, sidhani kama hatua hii ilikuwa ni usaliti isipokuwa upendo ambao ni muhimu kwa binadamu yoyote haswa wakati wa matatizo.

Mh Rais, nimeogopa sana kwa kauli hii yako, je Taifa linakwenda wapi, hivi kweli sisi Wabunge ni maadui? Kama viongozi tutafikiri utengano ni moja ya njia ya kuimarisha vyama vyetu, basi bila shaka tutakuwa tunalitendea Taifa ubaya .

Dhambi hii ikikomaa basi ni hakika kwamba lugha za udini, ukanda na ukabila hazitaacha kukomaa, ni muhimu sasa tukajenga utamaduni wa kuhimiza mshikamano wa Kitaifa bila kujali itikadi kama kweli tunawapenda masikini na wanyonge wa nchi hii.

Nawaomba Wabunge wenzangu walionijali wakati niko magereza wasijisikie vibaya kwani walifanya jambo jema na muhimu kwa wakati muhimu sana katika maisha yangu, ninatarajia kuwa Spika wa Bunge atatoa kauli juu ya kauli yako.

Mh Rais wakati wa Msiba wa Christina Lissu dada yake na Mh Tundu Lissu nilikuona katika msiba ule wewe na Mama yetu Mke wako, je Mh Rais na wewe ulikuwa unasaliti Chama chako?

Mh Rais neno la Mungu linasema, Wapendeni maadui zenu, waombeni wanaowauzi , wabarikini wanaowaonea kwani kufanya hivi ni kuishi kwa thawabu za Mwenyezi Mungu.

Mungu akubariki sana, natumaini Mh Rais sitakamatwa leo kwa ujumbe huu mfupi.


Godbless J Lema (MB)
Nice job,unakua sasa.Siasa siyo uadui,siyo kutukanana wala kuombeana kifo.Ni kujenga hoja,big up Lema. Jela haiongopi.
 
Heshima ya kiongozi inatakiwa kutokana na huduma yake kwa umma si police wala vitisho.any way this is Tz
Umma tunamtambua nyie watu gani ambao kutwa mnatukana serikali,bunge,mahakama na sasa mumehamia kutukana TLS kuwa toka iundwe no tawi LA CCM haijafanya chochote. Hamieni Somalia basi
 
Kuna siku mwanajukwaa alisema mtakatifu yuko kwenye kwaresma. Sasa nashindwa kuelewa kwa ile kauli yake ya mtu kumtembelea mfungwa ni msaliti. Ndiyo maana nasema siwezi kumwombea maana mungu wake siyo mwenye huruma. Mungu ninayemtegemea haendekezi chuki. Huyu anajidai ni mkatoliki! Hahahaaa labda katoliki zimegawanyika
 
Kweli viongozi wa dini zote wakikaa kimya hapa nitashangaa!!!!!!

Baba mtakatifu alimtembelea mtu aliyempiga risasi jela na kumsamehe.

Looo nimeshangazwa leo
 
Back
Top Bottom