Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Usilinganishe kauli za Lema na za mkuu wa nchi. Kauli za amiri jeshi zina athari wewe !!!
Tupe nukuu ya Magu, plus haiondoi ukweli kuwa Lema hana moral authority ya kuongelea kuhusu upendo, Lema yeye alikuwa Nabii wa vifo, leo kwa nini alie lie kisa kusalimiwa ?
 
You are part of these shida, usijiweke pembeni. Una wanaokuhusu wataangukia katika maonevu haya!
Kumpenda mtu isiwe one way traffic!

Yaani kutaka wewe tu upendwe lakini hutaki wewe kuwapenda wengine.

Hata kumuombea mtu mabaya sio upendo achilia mbali kutaka watu wasisalimiane au kususa futari yao .

Mbona hatukuona huo upendo au ushauri kwenye hii habari?

LINK==> CCM wazungumzia uamuzi wa wabunge wa UKAWA kutowasalimia

LINK==> Saed Kubenea ataka wabunge wa UKAWA wenye wapenzi wao CCM wawasuse

LINK==> Wabunge wa UKAWA wasusa futari ya Waziri Mkuu

Ama kweli mkuki kwa Nguruwe ni mtamu...

It's very easy to act as victim wakati wewe ndiye aggressor.

Inanikumbusha kwenye football ambapo mchezaji anamtemea mate mchezaji mwingine ambapo yule aliyetemewa mate anapatwa na hasira na kurusha kofi au ngumi. Referee ataona mwenye makosa ni yule aliyerusha kofi au ngumi na hapohapo atampatia kadi nyekundu.
Si huwa mnasema yeye ni baba wa nyumba!
Kwahiyo mtoto mmoja akifanya kosa unahimiza na wengine kumtenga ili umkomeshe!
Nafikiri baba bora anaangalia namna bora ya kuunganisha familia yake!
ila sio kwenda kujigamba kwa majirani kama nimezuia na wenzie hakuna kumpa ushirikiano!
 
Hayo muulize Nabii Lema, yeye ndio alikuwa anasema kwa mbwembwe na kejeli kuwa Rais atakufa kabla ya 2020, leo analia lia kwa sababu ya kuto kusalimiwa tu. Unafiki utamuumiza Lema.
Jambo muhimu nililoliona kwenye andiko la lema ni kwamba anaonekana kujifunza suala la nidham dhidi ya mamlaka baada ya kutoka kisongo!.
amekuwa mpole, ama kweli jela ni noma........hongera sana kwa hilo mh lema.
 
Mh Rais Magufuli nakusalimu.

Nimetoka Magereza hivi karibuni ambako nilikuwa huko kwa zaidi ya miezi minne kwa kunyimwa masharti ya dhamana kwa dhamana iliyokuwa wazi.

Mh Rais, nimeona kwenye vyombo vya habari leo kuwa kwamba wale Wabunge waliokuwa wanataka kunisalimia nilipokuwa Magereza kuwa ni wasaliti wa chama cha CCM, Mh Rais wengi walinisalimia , Wachungaji , Masheikh, Wabunge na Viongozi mbali mbali , sidhani kama hatua hii ilikuwa ni usaliti isipokuwa upendo ambao ni muhimu kwa binadamu yoyote haswa wakati wa matatizo.

Mh Rais , nimeogopa sana kwa kauli hii yako , je Taifa linakwenda wapi , hivi kweli sisi Wabunge ni maadui? kama viongozi tutafikiri utengano ni moja ya njia ya kuimarisha vyama vyetu , basi bila shaka tutakuwa tunalitendea Taifa ubaya .

Dhambi hii ikikomaa basi ni hakika kwamba lugha za udini ,ukanda na ukabila hazitaacha kukomaa , ni muhimu sasa tukajenga utamaduni wa kuimiza mshikamano wa Kitaifa bila kujali itikadi kama kweli tunawapenda masikini na wanyonge wa Nchi hii .

Nawaomba Wabunge wenzangu walionijali wakati niko magereza wasijisikie vibaya kwani walifanya jambo jema na muhimu kwa wakati muhimu sana katika maisha yangu , ninatarajia kuwa Spika wa Bunge atatoa kauli juu ya kauli yako .

Mh Rais wakati wa Msiba wa Christina Lissu dada yake na Mh Tundu Lissu nilikuona katika msiba ule wewe na Mama yetu Mke wako , je Mh Rais na wewe ulikuwa unasaliti Chama chako ?

Mh Rais neno la Mungu linasema , Wapendeni maadui zenu , waombeni wanaowauzi , wabarikini wanaowaonea kwani kufanya hivi ni kuishi kwa thawabu za Mwenyezi Mungu .

Mungu akubariki sana , natumaini Mh Rais sitakamatwa leo kwa ujumbe huu mfupi .


Godbless J Lema (MB)

Uwe na kumbukumbu timamu. Soma hapa: Kamati Kuu CHADEMA yawavua Uanachama Madiwani 5 walioingia muafaka Arusha
 
RAIS WETU WA ARUSHA MANDELA WA A,TOWN PAMOJAH CHARII ANGU.
Lema-Boy.png



Swissme
 
what the issue behind? unajua adhabu ya kosa la kuota la Lema?
Hoja hapa sio kosa bali ni upendo. Unachanganya msingi wa hoja.

Mwenye mamlaka ya kusema kuna kosa limetendeka ni mahakama.

Mwenye mamlaka ya kupenda au kutopenda ni wewe au mimi bila kusubiri maoni/mawazo ya mtu wa pili lakini kikubwa zaidi, kupenda na kupendwa sio one way traffic
 
Si huwa mnasema yeye ni baba wa nyumba!
Kwahiyo mtoto mmoja akifanya kosa unahimiza na wengine kumtenga ili umkomeshe!
Nafikiri baba bora anaangalia namna bora ya kuunganisha familia yake!
ila sio kwenda kujigamba kwa majirani kama nimezuia na wenzie hakuna kumpa ushirikiano!
Kwanza hakuna nukuu yoyote iliyosema hivyo kuhusu Magu, pili kuna njia nyingi za kumfunza mjinga, si lazima umubembeleze kila wakati, somo limefika kwa wahusika.
 
Naona akili sasa zinaanza kumrudia baada ya kukaa kisongo , aki angalia Huko mbele kuna kesi ya mashoga na ndoto sasa anataka huruma
 
Chadema ni wasahaulifu sana.Lema alishawahi kutangazia dunia kuwa adui namba moja wa chadema ni CCM au mmesahau tupekue thread humu?Kitendo cha wabunge wa ccm kumtembelea Lema kingekuwa ni usaliti mkubwa kwa ccm,viongozi wa ngapi wa ccm wanapata matatizo ikiwemo kuugua zaidi ya kuweka msemo wenu "waache wafu wazikane".Mlianza na dhambi ya ubaguzi itwamaliza
 
Lema fanya yako..Jimboni hakuna maji ya uhakika wala umeme!Miundo mbinu ya shida na vijana wengi hawana ajira!Ila kila siku una deal unarukia yasiyokuhusu..Fanya yako na shughulikia kero za wananchi wako!Period
Iki anachokifanya pia anashughulikia wananch wake.. Acha kukaririri maitaji ya wananch sio maji wala umeme pekee bali na utawala bora.
 
Acha unafiki, haujui Lema amekaa Kisongo kwa kesi ipi ?
Yeye yuko radhi kumuombea Rais afe ila analia lia hapa kuhusu kusalimiwa tu, kweli Nabii Lema ana nyumbu wengi.


Kubali tu jamaa ana roho mbaya , hata kitendo cha kabinti Wema Sepetu kuhama chama yaani kimemuuma kashindwa kuvumilia, Lowasa ndo kabisaaaa siku akifa ataweka sherehe
 
Tunaomba utuwekee hukumu ya Court of appeal na High court iliyokupa dhamana. Hizi ni kesi muhimu kwa kila mmoja. Please and please.
Na wewe fanya Kama alivyofanya Lema ili upitie aliyopitia live na upate hukumu live Lema usimfanye test tube
 
Back
Top Bottom