Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Acha unafiki, haujui Lema amekaa Kisongo kwa kesi ipi ?
Yeye yuko radhi kumuombea Rais afe ila analia lia hapa kuhusu kusalimiwa tu, kweli Nabii Lema ana nyumbu wengi.

Kama uliwasikia wale Waheshimiwa Majaji wenye kufahamu na kuiheshimu taaluma yao walivyosema, ndio utajua kwanini Lema aliwekwa Kisongo..

Turudi kwenye hoja ya msingi.. Huyo alieombewa kufa ni nani..? na aliombewaje..? Kama ulikaririshwa na hujui basi rudi ukawaulize, kisha urudi hapa..
 
Very sad, kama Rais wa nchi anaweza kuwa na mawazo kama hayo kwa ishu ndogo kama hiyo, sijui itakuwaje litakapokuja jambo kubwa linalohitaji muunganiko wa wabunge wote.
 
Lakini ubaguzi mlianza nyie kumbuka mlisusa futari ya majaliwa dodoma
Wanafiki sana, walikataa futari na kutoa ushirikiano wowote kwa CCM, huyu Meya wao wa Ubungo ndio alikuwa mstari wa mbele kueneza chuki, kuwaahadaa wananchi wasishirikiane na serikali yao, Lema ndio aliamua kumuombea kifo kabisa Rais wake, Magu ni mwanaume ana koromeo utaropoka ropoka huku yeye anakulia timing tu, nashangaa saivi mnabembeleza urafiki na Magu.
 
Siku zote namlaumu aliyeteua hili jina sijui alikuwa akimkomoa nani kwa kweli kwanini aliwaacha watu na busara zao ma akili zao leo hii tulitakiwa tuwe tunaongozwa na Mark Mwandosya, Akina Mzee Pinda sasa hili janga hili sijui tutalibeba mbeleko gani kwa kweli...

Mungu tunusuru tunakoelekea siko kabisa
Huyu huyu ndio chaguo sahihi kwa wakati muafaka, watu soft soft sambamba na lile fisadi kuu la side b hawakupaswa kabisa kupewa nchi.
Ukiacha huyu mwingne sahihi ni prof mhongo.
hizi ni zama za kuita nyeusi NYEUSI, nyeupe NYEUPE!
maneno meengi matamu ya kisanii tumeyachoka!
 
Toka uhuru wa nchi hii ni mara ya kwanza CCM kupata mwenyekiti wa ovyo ovyo na mara ya kwanza toka uhuru tumepata kiongozi ambaye nii dikteta uchwara na mwenye mawazo mfu
 
Umeongea vema kamanda Lema, umetumia lugha isiyoudhi, lugha tamu kwa msomaji na inayoamsha hisia za huruma, upendo na kutuacha na tafakuri murua kabisa.
 
Lema alikuwa anamuombea Rais kifo miezi michache iliyopita, tena kwa mbwembwe na kejeli unamuombea binadamu mwenzio asifikishe 2020, leo kwa unafiki anajidai kuhubiri upendo, huu unafiki Godbless J Lema unautoa wapi ?
Mnafki ni Mkatoliki anayehubiri chuki kipindi cha Kwaresma.

Uliza mafundisho ya kikatoriki ujuwe kwaresma ni nini au waulize waislamu ni kwa nini kuna mwezi wanauita ni mwezi mtukufu na ni mwezi wa haki na waislamu wanapashwa kutenda matendo gani.
 
Jamaa ana roho mbaya sana na chuki za kutisha! Halafu anajifanya ni mcha Mungu!
Wengi mnachanganya kati ya mungu na Mungu.

Hakika nakuambia Mungu wa kweli ni wa Isaka na Yakobo tu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
NINA WASIWASI NA URAIA WAKE KWELI NI MTANZANIA HUYU SASA MBONA ANALIGAWA TAIFA AMBOLO MW.JKR AMELIJENGA KWA SHIDA SANA MUNGU ATUSAIDIE MAOMBI NI MUHIMU SANA KIPINDI HIKI KWA TAIFA LETU
 
Mnafki ni Mkatoliki anayehubiri chuki kipindi cha Kwaresma.

Uliza mafundisho ya kikatoriki ujuwe kwaresma ni nini au waulize waislamu ni kwa nini kuna mwezi wanauita ni mwezi mtukufu na ni mwezi wa haki na waislamu wanapashwa kutenda matendo gani.
Mwambie Lema aache kulia lia, yeye alikuwa tayari kumuombea binadamu mwenzie kifo tena kwa mbwembwe na kejeli, yeye alikuwa Nabii kazi kutabiria kifo wenzie ila leo analia lia kisa kutokusalimiwa, ajitakaze ana koromeo yeye kama wenzio wanavyompotezea anavyo watabiria kifo.
 
Hivi wabunge wa upinzani huwa hawana kumbukumbu ama nini? Kuna siku walitoka nje ya bunge wakawatangazia watu wao kwamba wasishitikiane na wale wa ccm.
 
hawa walikwenda pemba wakamsema sana maalim sefu .eti anawazuia watu wasiende msibani mara anawazuia watu kukinga maji mara sijui nini .leo ndio hayo
 
Na upinzani munawajibu wa kuhubiri haya uliyoyasema kwa wanachama wa wapenzi wenu, Chadema mna wanachama na wapenzi wenye chuki kwa serikali na dola kwaujumla. Kila mmoja anamuhitaji wenzake kwa njia moja au nyingine.
Hiyo chuki dhidi ya serikali na dola raia hazaliwi nayo bali serikali na dola humfundisha. Serikali ndio ya kwanza kupenda na kutenda haki kwa raia then raia love back the government.
 
Lema alikuwa anamuombea Rais kifo miezi michache iliyopita, tena kwa mbwembwe na kejeli unamuombea binadamu mwenzio asifikishe 2020, leo kwa unafiki anajidai kuhubiri upendo, huu unafiki Godbless J Lema unautoa wapi ?
Usilinganishe kauli za Lema na za mkuu wa nchi. Kauli za amiri jeshi zina athari wewe !!!
 
JpM nahisi anamatatizo makubwa yanayosababishwa na kukosa furaha tangu akiwa mdogo....
hivyo amekua ni mtu mwenye hasira zisizokwisha na zinamuondolea ubinadamu, furaha na busara.

iko shida
 
Kumpenda mtu isiwe one way traffic!

Yaani kutaka wewe tu upendwe lakini hutaki wewe kuwapenda wengine.

Hata kumuombea mtu mabaya sio upendo achilia mbali kutaka watu wasisalimiane au kususa futari yao .

Mbona hatukuona huo upendo au ushauri kwenye hii habari?

LINK==> CCM wazungumzia uamuzi wa wabunge wa UKAWA kutowasalimia

LINK==> Saed Kubenea ataka wabunge wa UKAWA wenye wapenzi wao CCM wawasuse

LINK==> Wabunge wa UKAWA wasusa futari ya Waziri Mkuu

Ama kweli mkuki kwa Nguruwe ni mtamu...

It's very easy to act as victim wakati wewe ndiye aggressor.

Inanikumbusha kwenye football ambapo mchezaji anamtemea mate mchezaji mwingine ambapo yule aliyetemewa mate anapatwa na hasira na kurusha kofi au ngumi. Referee ataona mwenye makosa ni yule aliyerusha kofi au ngumi na hapohapo atampatia kadi nyekundu.
what the issue behind? unajua adhabu ya kosa la kuota la Lema?
 
Back
Top Bottom