Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui


Sina hakika na kile unachowaza kama kina uhalisia, pia sina hakika kama unajua maana ya chuki? Labda nikuelezee kilichomtokea Lema, LEMA HAKUOTA NDOTONI WALA HAKUTUMIWA SMS BALI ALIPATA "MAONO" YENYE MAAGIZO FULANI NA HAKUA NA BUDI KUYAFIKISHA KWA MHUSIKA. RAIS WAKO ANAJUA MAONO NI KITU GANI NA ANAMJUA MUNGU KAMA UNAVYOMSIKIA KILA MARA AKISEMA YEYE NI MPENZI WA MUNGU PALE ANAPO SEMA KWELI HIVYO ANAJUA NJIA ZA MUNGU KUWASILIANA NASI NA MOJA WAPO NI HIYO YA MAONO. ENDAPO ANGESEMA HATA MIMI NILIONGEA NA MUNGU AJANIAMBIA JUU YA MAONO YAKO TUNGEAMINI KWELI LEMA KATUCHANGANYA LAKINI YEYE KAMFUNGA KWA SABABU ZAKE BINAFSI HATA WEWE HUZIJUI,.

MWISHO WA SIKU TUSEME MJUMBE KAFUNGWA, HUKU KWETU TUNASEMAGA MJUMBE HAUWAWI LAKINI HUYU ALMANUSURAH AUWAWE.

NIMALIZIE TU KUSEMA HAINA HAJA YA NGUVU KUBWA SANA KUJUA NANI MWENYE CHUKI, KAMA HATA KUJULIANA HALI KAMA WATU WA TAIFA MOJA NI USALITI BASI HIYO NDIYO CHUKI NA SIO KINGINE.
 

Hivi umesha pitia nyuzi za wana chadeama kwenye mitandao ya kijamii, na kujionea kauli zinazo toka huko ikiwa zingine ni vitisho na kebehi kwa wana CCM? Ni dhahiri unajarubi kumtetea Lema, mimi hilo sina pingamizi nalo ni haki yako. Lakini uliona wapi mtu anamtabiria kifo rafiki yake? mara nyingi watu humtabiria kifo adui yake ili wapate nafasi ya kufanye yale wanayo yataka pindi adui yao anapo toweka. Sasa kama wewe unaona Lema ni mtu msafi kiasi cha kuwa karibu na Mungu na Mungu huyo huyo akaamuwa kutowa ujumbe kupitia Lema, hapo napata picha nina ongea na mtu wa aina gani.
 
duh yaani kusalimiwa ndo watu mnalalamika hivi...
acheni basi wakuu...
 

Lema hajawai kuwa mtabiri, lema alipata maono na ndio maana hajajiItaja kuwa yeye ni nabii. Kumbuka maono anaweza kupata mtu yeyote yule kulingana na Mungu anavyotaka.. Tangu lini dola ikatishiwa na upinzani? haiwezekani labda waasi ndio wanaweza kuitisha dola.
 
It does not help you can still make an application for the Court of appeal to make a review of the same!
Aiseee!!! nawashauri wanasheria wa Lema wafanye hiyo kitu haraka ili tupate hiyo hukumu! Ahsante sana kwa kunihabarisha!!
 
Hawa ni yule mnyama asiye na kumbukumbu husahau baada ya sekunde tu. Kwani yeye Lema mwenyewe anahubiri upendo na amani? Akwende zake amuache Rais wetu kipenzi afanye kazi. Hamna jipya nyie.
 
Kwani wewe unahubiri upendo toka lini hata utake Rais ahubiri upendo? Kazi ni moja tu hadi muwe na adabu na heshima kwa Mkuu wa nchi. Mlizoea kumtukana Kikwete sasa mmekutana na mwamba. Sifa zote mlizotaka kwa Rais ajae zipo kwa Mr. President JPM
 
Kama ungekuwa unatumia lugha za kistaarabu kiasi hiki tangu awali basi unge epuka kadhia iliyokukuta. Mwanzo mzuri Kamanda na ujumbe utafika. Bila shaka hautakamatwa there is nothing wrong in it, hakuna kuombeana vifo humu. Kweli Jela yastahili kuitwa chuo cha mafunzo a.k.a The Correction Centre.
 
Nyerere alitoa mfano mfupi tu akasema.. Kwa nchi changa kama hii tukikumbatia ukabila tutaangamia, alikuwa na maana ya vitu kama ukabila (wakati huo wa chama kimoja ) usitutenganishe... Mzaramo aende kuoa kule chato. Mtukufu Tafadhali njoo urekebishe kauli yako...
 
Ukabila haufai!..aache upendeleo na chuki kwa wasio wa upande wake
 
nadhani sasa ataelewa nini mana ya upendo. kudharau mamlaka hata kama zinamapungufu. si upendo huo.
 
Wabunge wa UKAWA walipozuiliwa kuwa na mahusiano na wa CCM ulikuwa umezaliwa?
 
Jameni pa moja na kujadili mambo ya siasa,mkumbuke Yesu yu karibu kurudi.Msipoteze muda mwingi kwenye mambo ya kupita,wengine pressure ziko juu.Yesu ndiyo kimbilio pekee,wanadamu wanaweza kubadilika lakini Yesu habadiliki.Wanadamu wanaweza wakakuahidi wasitende lakini ahadi za Mungu ni hakika na kweli.
Je leo umemshukuru Mungu walau umeamka mzima?
 
Siasa kweli si uadui ila kwa Watanzania ni uadui maana ukiona jinsi mifumo ya nchi inavyofanya kazi katika utekelezaji wa majukumu yao ni dhahiri 'SIASA TANZANIA NI UADUI' Mfano; Mkuu kusema waliokwenda kumpa Lema hi! akiwa lupango eti ni usaliti. Jamani kivipi inakuwa usaliti kisa vyama tofauti.
 

Mkuu Karibu uwatumikie wapiga kura wako kwa kasi sasa.

Ujumbe wako umefika.

My Take;

Twende mbele turudi nyuma me bado na mashaka na viongozi walio chini yake na wanao mletea hizo Informations zote kwa imani yangu wanampoteza Rais kabisa nahisi kunawatu bado wanamakundi makubwa ndani ya CCM na wanachomeana sana kwa JPM uhasama ndani ya serikali mpaka kupakaziana nyie ni viongozi wa nchi hii mjitambueni Jamani hii ni Tanzania yetu sote. Mmekuja na slogan KAZI KWANZA matokeo yake mnatuvuruga ni are?

Mkianza zambi ya kubaguana ati wao ni CCM sie ni CUF,CDM, ACT itawakula mpaka mjute na hizo ndimi zenu za kuchonganisha nyie kwa wenyewe. Kumbukeni wabunge nyie ni Taasisi na mhimili mwingine sasa vuruganeni mtashangaaa
 
Vyama vya upinzani havina budi kuungana na kuwa na tamko moja juu ya haya yanayofanywa na mzee
 
Lema fanya yako..Jimboni hakuna maji ya uhakika wala umeme!Miundo mbinu ya shida na vijana wengi hawana ajira!Ila kila siku una deal unarukia yasiyokuhusu..Fanya yako na shughulikia kero za wananchi wako!Period

Ukisha kuwa kiongozi wa mahali na umechaguliwa na wananchi wako iwe ni CCM CUF ACT NCCR we ni kiongozi wa wote sasa Kama kiongozi wa nchi ananza kuwavuruga hao viongozi itakuwaje so me ni CCM we ni CUF huyu kiongozi atatuongoza vipi,hili nalo ni tatizo pia

POLITICS IS BATTLE OF IDEAS
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…