Jotojiwe
JF-Expert Member
- Mar 24, 2012
- 335
- 130
Wala nisiende mbali, chuki sio kupigana makonde tuu, chuki ipo hata kwenye matamshi ya mtu. Lema aliposema utapata baraka kwa Mungu ukimzomea Lowassa. Wewe kwa mtazamoa wako yale maneno yalikuwa ni chuki, kejeli, utovu wa nidhamu au labda kwa mtazamo wa upinzani ule ulikuwa ni ujasiri? kauli nyingi za upinzani zimejazwa chuki ambazo ukiwauliza ni za nini, wanakosa majibu. Hivi, mtu mwenye akili timamu anaweza kusimama hadharani ukasema nimeota mtu fulani atakufa?, unaweza kutumia kauli hiyo kwa mtoto aliye mzaa? au unaweza kuwaambia wanafamilia nimeota baba yetu atakufa? kama sio chuki ni nini?
Sina hakika na kile unachowaza kama kina uhalisia, pia sina hakika kama unajua maana ya chuki? Labda nikuelezee kilichomtokea Lema, LEMA HAKUOTA NDOTONI WALA HAKUTUMIWA SMS BALI ALIPATA "MAONO" YENYE MAAGIZO FULANI NA HAKUA NA BUDI KUYAFIKISHA KWA MHUSIKA. RAIS WAKO ANAJUA MAONO NI KITU GANI NA ANAMJUA MUNGU KAMA UNAVYOMSIKIA KILA MARA AKISEMA YEYE NI MPENZI WA MUNGU PALE ANAPO SEMA KWELI HIVYO ANAJUA NJIA ZA MUNGU KUWASILIANA NASI NA MOJA WAPO NI HIYO YA MAONO. ENDAPO ANGESEMA HATA MIMI NILIONGEA NA MUNGU AJANIAMBIA JUU YA MAONO YAKO TUNGEAMINI KWELI LEMA KATUCHANGANYA LAKINI YEYE KAMFUNGA KWA SABABU ZAKE BINAFSI HATA WEWE HUZIJUI,.
MWISHO WA SIKU TUSEME MJUMBE KAFUNGWA, HUKU KWETU TUNASEMAGA MJUMBE HAUWAWI LAKINI HUYU ALMANUSURAH AUWAWE.
NIMALIZIE TU KUSEMA HAINA HAJA YA NGUVU KUBWA SANA KUJUA NANI MWENYE CHUKI, KAMA HATA KUJULIANA HALI KAMA WATU WA TAIFA MOJA NI USALITI BASI HIYO NDIYO CHUKI NA SIO KINGINE.