Earthmover
JF-Expert Member
- Sep 28, 2012
- 24,977
- 23,799
......Godbless umefika muda wa wewe mwenyewe kujitathmini. Siasa haijawahi kuwa uadui katika nchi hii mpaka pale wewe ulipoziumba na kuziimarisha siasa za namna hiyo kwa maneno yako. Godbless jiulize kwani wewe ndio mbunge wa kwanza wa upinzani nchi hii?Jiulize pia kama kweli ktk jimbo lako kuna matatizo yanayokufanya wewe ufanye siasa zinazofanana na za kimapinduzi. Godbless haujawa muangalifu ktk kauli zako, huwafikirii Waka huwahurumii wananchi wako wala wa taifa kiujumla unapotoa kauli zako. Unafahamu frustrations zao, badala y'all kuwapoza na kuwabadili mtazamo ili watumie changamoto zilizopo Kama fursa wewe sasa unazitumia hizo kama silaha yako ya kujiimarisha kisiasa, kujiimarisha katika ajira yako bila kujali athari zinazoweza kutokea kwa wewe kufanya hivyo. Nasema bila kupepesa macho ya kuwa nilikuwa mfuasi wako kipindi kile cha mama Batilda Buriani. Baadae siasa zako zikaanza kunikifu, MA ukweli kuwa kuna watu wengi ndani ya chama chako siasa zako zimewakinai. Kuna mmoja yeye aliipenda katiba ya wananchi kwa kitu kimoja kikubwa, ukomo wa ubunge. Ukomo wa ubunge kwake ungefanya jambo moja kubwa, kumuondoa Lema Arusha, kuondoa image mbaya ya chama. Yakupasa Godbless ufahamu kuwa hakuna namna moja ya uongozi inafaa nyakati zote, namna kadhaa za uongozi zinaweza kufaa nyakati tofauti kulingana na mahitaji. Kiongozi anayeangalia maslahi makubwa ya nchi itamlazimu wakati fulani kutumia staili ya Machiavelli kulinda ustawi wa watu wengi dhidi ya kijana mmoja mjinga na mbinafsi asiyetosheka na kikubwa alichopata ukilinganisha na uwezo wake. Taswira y'all siasa unayoijenga Godbless si tu italeta uadui kati ya chama tawala na upinzani, italeta pia uadui kati ya wenye kujishughulisha na kupata na wale wanaoaminishwa matatizo yao na kukosa kwao kumetokana na wao kuonewa. Waambie ukweli Godbless, hakuna anayewaonea, wanajionea wenyewe. Juzi alikuwa Mkapa, jana Kikwete na leo Magufuli. Mbeya wanaonewa na manispaa, arusha nao manispaa, ubungo wataonewa na manispaa, ilala halikadhalika. Kigoma ujiji malalamiko hayaishi. Serikali yenye kuleta maendeleo inahitaji watu wafanye kazi ili walipe kodi hakuna uongo mwingine unless udanganye watu, utukane system ya Machiavelli ifanye kazi
......ukiongea na LEMA unaongea na Watanzania