Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Mh Rais Magufuli nakusalimu.

Nimetoka Magereza hivi karibuni ambako nilikuwa huko kwa zaidi ya miezi minne kwa kunyimwa masharti ya dhamana kwa dhamana iliyokuwa wazi.

Mh Rais, nimeona kwenye vyombo vya habari leo kuwa kwamba wale Wabunge waliokuwa wanataka kunisalimia nilipokuwa Magereza kuwa ni wasaliti wa chama cha CCM, Mh Rais wengi walinisalimia, Wachungaji, Masheikh, Wabunge na Viongozi mbali mbali, sidhani kama hatua hii ilikuwa ni usaliti isipokuwa upendo ambao ni muhimu kwa binadamu yoyote haswa wakati wa matatizo.

Mh Rais, nimeogopa sana kwa kauli hii yako, je Taifa linakwenda wapi, hivi kweli sisi Wabunge ni maadui? Kama viongozi tutafikiri utengano ni moja ya njia ya kuimarisha vyama vyetu, basi bila shaka tutakuwa tunalitendea Taifa ubaya .

Dhambi hii ikikomaa basi ni hakika kwamba lugha za udini, ukanda na ukabila hazitaacha kukomaa, ni muhimu sasa tukajenga utamaduni wa kuhimiza mshikamano wa Kitaifa bila kujali itikadi kama kweli tunawapenda masikini na wanyonge wa nchi hii.

Nawaomba Wabunge wenzangu walionijali wakati niko magereza wasijisikie vibaya kwani walifanya jambo jema na muhimu kwa wakati muhimu sana katika maisha yangu, ninatarajia kuwa Spika wa Bunge atatoa kauli juu ya kauli yako.

Mh Rais wakati wa Msiba wa Christina Lissu dada yake na Mh Tundu Lissu nilikuona katika msiba ule wewe na Mama yetu Mke wako, je Mh Rais na wewe ulikuwa unasaliti Chama chako?

Mh Rais neno la Mungu linasema, Wapendeni maadui zenu, waombeni wanaowauzi , wabarikini wanaowaonea kwani kufanya hivi ni kuishi kwa thawabu za Mwenyezi Mungu.

Mungu akubariki sana, natumaini Mh Rais sitakamatwa leo kwa ujumbe huu mfupi.

Godbless J Lema (MB)
Mkuu hebu tukumbushe haya..
Nani walisema adui namba moja wa watanzania ni ccm?
Nani walisema wapinzani wasishirikiane na ccm?
Nani walisusia futari ya waziri mkuu?
Ni mbunge gani wachadema alishawai kumpa muda wake wakuongea mwana ccm?
 
Binafsi namfuatiliaga sana Rais kiukweli ni mbaguzi sana. Issue ya kitaifa yeye huweka uchama. Mfano wakati tumetoka kwenye uchaguzi wa marudio ambapo pamoja na figisu zilizofanywa kwa wapinzani ili CCM ishinde, kweli ikashinda ajabu siku moja akiwa anampokea sikumbuki Rais wa nchi gani, Mimi nilidhani ni ya kitaifa zaidi kumbe bado akasimama na kwenda kwa Waandishi na kusema CCM hoyee. Eti tumewachapa (wapinzani) kwangu japo yeye ni mwenyekiti wa CCM lkn pale akili yangu inaniambia ilikuwa ya kitaifa sio chama, again alichomdanyia Yule Mbunge wa CUF akiwa njiani kuelekea Mtwara haikuwa fair. Ila uchonganishi wa Rais kwa Mbunge na wapiga Kura wake kwa faida ya Chama chake,
Alichomfanyia Lema maana kwa confession japo indirectly kwa kudai wabunge waliopanga kwnda kumsalimia Lema eti wasaliti,
Again Leo alipopiga simu Clouds TV akasema Safi sana Diamond kwa kuwa ni CCM.
Nikikumbuka alivyompeleka Tulia kwa Zengwe na yote na hata haya yanayofanyika kwa wapinzani kila anapokalia kiti Tulia.
Anahubiri umoja lakini ndio kiongozi wa kuwagawa wananchi kwa misingi ya Chama. Ina maana kutokuwa mwanaccm ni dhambi kubwa saaana.
 
Najua wanaccm mnafurahia hili lakini kumbukeni Tanzania ni mhimu zaidi ya CCM, Chadema na CUF na kadhalika. Yanahubiriwa maendeleo hakika watu Milioni Nane hamtafanikisha kwa ajili ya watu Milioni 50, Akimaliza hapo ataingia kwenye Dini, kisha Ukanda, then Kabila so hakuna aliyesalama, please Watanzania ni wamoja bila kujali vyama. Vyama kwa ujumla wenu mnafika kama 15milioni tusio na chama Tupo zaidi ya 35milioni. Ingekuwa uwezo wangu ningefutilia Mbali mavyama tubaki na Tanzania
 
Alichokisema Rais sikukipenda kabisa.Niliumia roho ila nimeshamsamehe.Pengine hajui alitendalo ila wazungu wana Msemo wao "ONLY TIME WILL TELL",Lets keep on waiting.

Mungu hapendi.
 
Mh Rais Magufuli nakusalimu.

Nimetoka Magereza hivi karibuni ambako nilikuwa huko kwa zaidi ya miezi minne kwa kunyimwa masharti ya dhamana kwa dhamana iliyokuwa wazi.

Mh Rais, nimeona kwenye vyombo vya habari leo kuwa kwamba wale Wabunge waliokuwa wanataka kunisalimia nilipokuwa Magereza kuwa ni wasaliti wa chama cha CCM, Mh Rais wengi walinisalimia, Wachungaji, Masheikh, Wabunge na Viongozi mbali mbali, sidhani kama hatua hii ilikuwa ni usaliti isipokuwa upendo ambao ni muhimu kwa binadamu yoyote haswa wakati wa matatizo.

Mh Rais, nimeogopa sana kwa kauli hii yako, je Taifa linakwenda wapi, hivi kweli sisi Wabunge ni maadui? Kama viongozi tutafikiri utengano ni moja ya njia ya kuimarisha vyama vyetu, basi bila shaka tutakuwa tunalitendea Taifa ubaya .

Dhambi hii ikikomaa basi ni hakika kwamba lugha za udini, ukanda na ukabila hazitaacha kukomaa, ni muhimu sasa tukajenga utamaduni wa kuhimiza mshikamano wa Kitaifa bila kujali itikadi kama kweli tunawapenda masikini na wanyonge wa nchi hii.

Nawaomba Wabunge wenzangu walionijali wakati niko magereza wasijisikie vibaya kwani walifanya jambo jema na muhimu kwa wakati muhimu sana katika maisha yangu, ninatarajia kuwa Spika wa Bunge atatoa kauli juu ya kauli yako.

Mh Rais wakati wa Msiba wa Christina Lissu dada yake na Mh Tundu Lissu nilikuona katika msiba ule wewe na Mama yetu Mke wako, je Mh Rais na wewe ulikuwa unasaliti Chama chako?

Mh Rais neno la Mungu linasema, Wapendeni maadui zenu, waombeni wanaowauzi , wabarikini wanaowaonea kwani kufanya hivi ni kuishi kwa thawabu za Mwenyezi Mungu.

Mungu akubariki sana, natumaini Mh Rais sitakamatwa leo kwa ujumbe huu mfupi.

Godbless J Lema (MB)
Mh Lema Rais Magufuli kama ametoa statement hiyo kwa wana CCM wenzako wala hajakosea ni kweli kabisa ilikuwa ni usaliti na wala si utengano.

Kumbuka sababu zilizo kufanya wewe uwe Gerezani ni issue inayomuhusu Mwenyekiti wao wa CCM sasa inapotokea kiongozi akaenda kukujulia hali kwa namna yoyote ile wa CCM inaonekana amehudhunishwa na wewe kuwa Gerezani na yuko against na waliokuweka ndani kiitikadi hata kama ni marafiki zako huo tunaita Usaliti na baadhi ya nchi anawezwa hata akapotezwa kabisa.

Lakini issue ya Rais Magufuli na Mke wake kuhudhuria msiba wa Dada yake na Tundu Lissu wala haifanani na wewe kuwa Gerezani mahabusu kwa kesi ya kisiasa/kiitikadi

Wala sio kuwa sasa Rais ndiyo umekuwa kimara wa ubaguzi ila umekuwa na misimamo yake ktk serikali kisiasa na kila siku anasisitiza amani,umoja na ushirikiano kwa watanzania wote.
 
Kila jambo lina nyakati na majira yake wakati wakuzaliwa na wakati wa kufa wakati wa kulia na wakati wa kucheka wakati wa kupanda na wakuvuna sijui sizonje yupo wakati gani hili nalo lita pita watanzania watapita lakini ardhi aliyo iumba Mungu inayoitwa Tanzania itakuwepo milele watu wanajisahau kwa vyeo mali uongozi..... nawaapia kwa jina la Mungu anaye ishi ukipanda chuki utavuna hiyo chuki na atendaye ya mwili atavuna hayo serikali hii itaumiza wengi makabila ukanda na dini mbalimbali lakini yote hayo nayo yatapita mtu akijiona Mungu mtu nae atapita Mungu si mjomba wa mtu Mungu ibariki Tanzania amen!
 
Binafsi sijafurahishwa na kauli za mtukufu JPM dhidi ya wabunge wa CCM walio kwenda kumtembelea lema kipindi yupo Kisongo. Mtukufu JPM amewaita wabunge hao 'wasaliti'. Hii ni kauli ya kulipasua taifa.

Lakini tujiulize je hii ndio mara ya kwanza kwa Mtukufu kuongea wazi wazi kauli za chuki dhidi ya wapinzani? La hasha, nakumbuka mwaka 2016 septemba Rais JPM akiwahutubia wananchi wa Zanzibar alitamka wazi wazi kuwa Anamshangaa sana Rais wa ZNZ anasaini makaratasi ya mtu aliyekataa kumpa mkono siku ya mazishi ya Jumbe, na kusema kwake isingekua rahisi hivyo.

Kwa kutizama kauli hizi unaweza ukajiuliza je Rais anafikiria nini kichwani kuhusu watu walio na Kabila au Dini tofauti na yake?

Kwa sasa tunaweza tukaona ni kauli za kisiasa na kupita tu, lakini naamini ipo siku Mtukufu anaweza kusema jambo juu ya Wasukuma dhidi ya makabila mengine au wakristo dhidi ya dini zingine, Jambo ambalo litadumu katika vichwa vyetu Milele yote na kuvuruga Maana ya Utanzania wetu.

Inasikitisha Rais anaposhindwa kutambua kua yeye kama Mtanzania Namba moja hapaswi kututizama wananchi wake katika mizania ya U Ccm na U pinzani, Raisi anapaswa kuelewa/kukumbushwa kuwa Kabla ya U ccm au U pinzani wetu sisi ni WATANZANIA, kabla ya kumtizama lema kama mwana chadema unapaswa kumtizama kama mtanzania.
Unapoomba kuombewa na wananchi huwa husema naomba wana Ccm mniombee, bali huwa unaomba watanzania wote

Mtukufu JPM unapaswa kuzitafakari sana kauli zako kabla hujalitenganisha Taifa.

Mapenzi ya Chama yasizidi mapenzi ya Taifa.
 
  • Thanks
Reactions: SIM
Kwa kauli za mkulu kwa kweli lema yabidi aombwe radhi manake sio kwa kauli hii.Lema alipokuwa gerezani aliitaji faraja ya kila alieona anaweza kumfariji bila kujali itikadi udini ukabila au hata umri so watu kutishiwa na kuitwa usaliti hii si sawa nitaipinga daima nikiwa na pumzi.
Alihitaji faraja.....!! Wewe ulikwenda kufarijiana?
 
Hapa duniani kila nchi ina kiongozi wake mkuu. Hapa kwetu Tanzania tunaye Rais wetu.

Mara kadhaa Rais wetu ametuomba tumuombee. Kauli hii tumekuwa tunaiona kama kauli nyepesi lakini ni nzito sana.
Watanzania miaka yote tumekuwa wamoja. Na kazi kubwa ya Rais ni kujenga umoja na mshikamano kwa watu anaowaongoza.

Rais wetu amefikia hatua ya kusema kwamba wabunge wa CCM kwenda kumpa pole mbunge mwenzao aliyewekwa kifungoni ni usaliti?

Basi hii inamaana Rais wetu analo tatizo flani ambalo kwa ajili ya faragha hawezi litaja, ndo maana anatuomba tumuombee.
Nashauri tumuombee.
 
ki ukweli si jambo jema na watanzania hatujalelewa hivi mi si shabiki wa upinzani lakini siasa ama Imani zinazojaza Chuki watanzania ni lazima sote kwa pamoja tuseme hadhrani kuwa NO . Mi mkereketwa wa Mkuu Ila sikubaliani na msimamo wake huo . Tanzania ni zaidi ya kila kitu
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Lakini baadhi ya Watanzania wanadhani Lema na Tundu Lissu na CHADEMA ndio wachochezi. Wanashindwa kuona kauli zote hizi kuwa zina hatari kubwa kwa taifa letu. Tuache unafiki na ushabiki, yamkini tutapona. Ama sivyo tutageuka Taifa la kijinga sana kwa hayo yatakayojiri muda si mrefu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom