Ndiyo, ushahidi wa kimazingira unaonyesha wazi mhusika wa shambulizi ni JPM! (wanaoweza kubisha ni wasio na akili ya kufikiria tu)
1. Press ya JPM akipokea ripoti ya akina Mruma na Osoro, ilikuwa clear kabisa, ilimlenga Lissu na alitamka wazi wazi hatua za kuchukua dhidi yake...
2. Eneo aliloshambuliwa ni lenye ulinzi mkali wakati wote, mwenye uwezo wa kuwaondoa walinzi siku ya tukio kwa vyovyote vile inahusu Amri kutoka "juu"
3. Baada ya kumshambulia hakuna namna yoyote iliyofanyika kuwakamata wahusika,wala kufunguliwa kesi inayohusiana na tukio lile, (yaani ilichukuliwa kana kwamba aliyepigwa risasi ni mbuzi tu, tena asiye na mwenyewe), kisingizio kikawa "wanamsubiri aliyrshambuliwa aje atoe ushahidi wake, (sababu ya kipumbavu kabisa) kamanda Barrow aliuawa Mwanza, nani aliyetoa ushahidi hata kukamatwa kwa wahusika maeneo mbali mbali ya nchi?
4. Kuna CCTV camera mahususi kwa ajili ya kulinda maeneo lilipotokea shambulizi, nani alizitoa? na kwa nini hazikutumika kama kielelezo cha kwanza kubaini waliohusika na shambulio?
5. Baada ya jaribio la mauaji kushindikana, iliamuriwa avuliwe ubunge, huku pesa yake ya matibabu ikizuiwa (ili afe tu), nani aliyekuwa na mamlaka ya kufanya yote hayo?
Mwenye akili timamu anafahamu, tukio zima la kupigwa risasi kwa Tundu Lissu, lilikuwa na muunganiko wa karibu kabisa na JPM, na alishindwa kuficha chuki yake dhidi ya Lissu akaionyesha wazi wazi kwa matendo baada ya tukio, angekuwa na akili angejitutumua walau kwa kumlipia matibabu na kumlipa stahiki zake kama mbunge,lakini kwa kuwa alikuwa na chuki za kipumbavu akaishia kujichoresha wazi wazi uhusika wake kwenye tukio!
Tuseme yoote, lakini ukweli unabaki kwamba JPM alikuwa na roho mbaya sana kwa "political opponents" wake, na Mungu ametoa fundisho, aliyetaka kuua amekufa yeye na sasa analiwa na funza huko chato,na aliyekusudia kumuua anaishi...
JPM alikuwa muuaji asiye na huruma kabisa, mbaya zaidi aliwalenga wapunzani wake kisiasa tu, wala hata sio wahaini au majambazi kama Sabaya!