Unajua lazima utumie akili sana kuandika heading, kinyume cha hapo unaondoa maana yote ya habari, na ujue hata mwanzo uanzaje ili umvutie msomaji. Yaani umefeli kote, ndio maana wanataka iwepo ithibati kwa ajili ya wajinga wachache kama nyie. Kwanza umeanza na ndoto, tayari ni vitu vya kusadikika na havina uhalisia. Ebu jaribu kama ungeanza na Tamko, maana nyuma yake kunautekelezaji. Ukafuatia na Scorpion akiota ndoto, eti nitakutoboa macho, sioni linganishi yako na ndoto ya Mh Lema, kwanza Scorpion anatuhuma za kumtoboa mtu macho, ambazo hazijathibitishwa na mahakama ili ziwe kweli, huenda nazenyewe zikawa uongo. Nakuomba sana, kabla haujanzisha thread uwe na akili ya kushilikisha na jua mko wengi kwenye upande wenu, usiogope kuonekana huna akili, au malipo yako yatapungua ndio uone bora ulete maada dhaifu kiasi hiki. Eti sheria ifuate mkondo, basi ungetupa hata vifungu baadhi ya hiyo sheria ili tuvijue na sisi tusije simulia ndoto zetu, kwa maana biblia inasema siku za mwisho Wazee wataota ndoto, na vijana watafasiri na kutoa maono, angalieni asema Bwana wa Majeshi ambae kwake kila goti litapigwa, nawasilisha.