Lema: Nikimuona mtoto wa Waziri Mkuu Majaliwa au wa Rais Mwinyi anaendesha Bodaboda ndipo nitaomba radhi

Lema: Nikimuona mtoto wa Waziri Mkuu Majaliwa au wa Rais Mwinyi anaendesha Bodaboda ndipo nitaomba radhi

Brother jibu kwa fact maana lema hoja yake iko wazi,
Mkuu nchi ina Mazezeta hii, yaani tuna furahia kuona raia wengine wanaajirwa Benki kuu, wengine Bandaranini kwa Vimemo, na raia wengine wao wanaambiwa nendeni mkasomee Ualimu au kaendesheni toyo.

Kama ni Ualimu hata watoto wa Raia wakasomee pia na wakafundishe, hakuna raia firs class na raia daraja la mwisho, shida nchi imejaa wajinga
 
Tukitoka kwa bodaboda tuje kwa
Walimu
Manesi
Watunza rekodi
Askari
Madereva
Na wengine wengi na pia tujue watoto wa mbowe lisu lema
Rais wangu Spunda Rungwe
Raisi Samia
Raisi kikwete wanafanya kazi zipi
Kabisa kunapaswa kuwa na haki sawa hakuna raia First class na raia daraja la mwisho, whay wengine waajiriwe Umoja wa Mataifa huko, Benki kuu na wengine wakawe walimu?
.
 
Hiyo hoja kama kweli ameitoa basi amedhihirisha yeye Lema ana upeo mdogo sana wa kufikiri. Lakini sishangai maana hata mwezake John Heche niliyesoma nae Shahada ya Elimu na mkewe ambaye ni Mwalimu pale Nyabulogoya Sekondari Kata ya Nyegezi Jijini Mwanza eti nae anauponda Ualimu kisa tu aliwahi kuwa Mbunge! Watu Hawa ni washamba kweri kweri!!
mpwayungu village njoo hapa umjibu Mtoto wa Shule
 
Sidhani kama amekuja kwa lengo la kukijenga chama chao huenda kuna ajenda ya kukidumaza hicho chama.
Je, yeye Lema amewahi muona mtoto wa Waziri mkuu anashona viatu?
Je anaweza kutuonesha mtoto wa Rais Mwinyi ambaye ni Mwl.wa S/Msingi ?
Kwa mantiki yake ni kuwa kazi zote zinazofanywa na watu wa kipato cha chini ni laana kwa kuwa hakuna watoto wa viongozi wakuu wa Nchi wanaozifanya.
Kama sio laana whay watoto wa vigogo wasizifanye? Kwa hio ulivyo mjinga unafurahia raia wengine kuajiriwa kwa vimemo kazi za maana kama za Umoja wa Mataifa huko New york, na raia wengine wao wanapaswa kuendesha toyo?

Unafurahia kuona hakuna usawa? Nyie ni watu wa aina gani? Yaani kuwa ba ubaguzi wa wazi kwenu ni furaha?
 
Anazo takwimu za vifo na majeruhi kutokana na ajali za barabarani ili tuone kati ya bodaboda na magari nani anachinja zaidi kwa mwaka?
 
Angeshauri sasa kazi gani ndio inayofaa au ni namna gani ya kuifanya hii ifae. Maana bodaboda wamekuwa msaada mkubwa sana hasa sisi tunaoishi uswahilini wamekuwa wakipeleka wagonjwa wetu mahospitali hata usiku wa manane na pia wamekuwa wakituwahisha kwenye mishe mishe zetu. Sasa kama mtu anasema hii kazi haifai kufanywa na watu anataka ifanywe na nani? Sidhani kama yeye huwa anatumia huu usafiri. Kazi yeyote mtu anayoifanya kwa furaha na hakuombi ugali wako muheshimu kwa hiyo omba omba ndio kazi ya heshima?
Tunapaswa kuwaona hata watoto wa viongozi wakisotea kazi, wakiwa mtaani, kwani wao wana nini? How come ni rai wa choka mbaya pekeee ndio waendeshe toyo?

Usawa uko wapi? Yaani raia wengine waajiriwe kwa vimemo na wengine wakasotee kazi?
 
Je !!Lema anataka wafanye kazi zipi za maana?Au nao waanze kutumia domo kaya kupiga kelele ili wawe wabunge?Au wakawe wezi wa magari?Tunaomba jibu Lema.
Kazi za Viwandani na kazi za kilimo na kama ni shida ya ajira hata watoto wa viongozi wawe na shida hioz haiwezekani wao wajairiqe kwa Vimemo huku sisi tukisota, na mbaya nyie mnashingilia mtaani kuona watoto wa viongozi wakila meme ya nchi hii, ina maana Nyerere aliwatafutia wao Uhuru?
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Lema amesema endapo atamuona mtoto wa Waziri mkuu mh Majaliwa au mtoto wa Rais Mwinyi anaendesha Bodaboda ndipo ataomba radhi.

Lema amesisitiza Kuwa Bodaboda ni Kazi isiyofaa inayouwa na kuwapa ulemavu Vijana Wengi.

Lema amenena haya kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Mlale Unono!

======

"Nikimuona mtoto wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa au Mtoto wa Rais Mwinyi anaendesha bodaboda na kudai ni kazi ya heri nitaomba radhi. Bodaboda ni kazi ya mateso,imeumiza watu na kujeruhi watu wengi.Acheni kudanganywa na Serikali iliyo kosa mbinu za kuokoa maisha yenu. Umasikini sio sifa."

View attachment 2539929
Wametoka kwa wamachinga
 
Hajadharau

Sisi kama Bodaboda tumemuelewa na huo ni ukweli, hakuna mtu aliyekuwa na malengo yakuja kuwa Bodaboda

Ni kazi yenye msoto sana na kuishi katika risk, hao mamwela wa CCM wamekuwa kero tukiwa road

Bado uhai wetu upo rehani kwa manyemela wanaotuwinda kuja kutuibia pikipiki zetu.

Ni kazi ambayo wengi tunafanya ili tufanikiwe tuje kuachana nayo.
Mkuu nchi ina watu wajinga haijawahi tokea sijui kama kuna Taifa jingine lina raia wajinga.

Yaani tuna furahia kuona watoto wa Vigogo wao wanafanya kazi huko New york Umoja wa Mataifa, wako BOT, ila watoto wa choka mbaya wao ni kozi za Ualimu na Unesi na kuendesha toyo.

Ina maana basi Nyerere uhuru alio tafuta aliwatafutia Viongozi na sio raia, na mbaya Raia wamekuwa mazezeta tupu wanaona ni sawa
 
Lema aache ushamba. Mtoto wa PM ataendaje kuendesha boda boda? Ndiyo maana kwenye jamii kuna matabaka. Kuna waendesha boda boda na kuna Wahandisi, kuna walimu na mama ntilie, kuna wabunge na wapiga kura, kuna watawala na watawaliwa. Sasa mtoto wa pm ni privileged hana sababu ya kuwa boda boda, lakini hiyo haifanyi kuendesha boda kuwa siyo kazi. Atulize hicho kichwa chake au wamempa crack huko Canada?
Kwa nini asiende? Kwa sababu yeye Baba yake ana tamka tu anapata kazi kokote? Nyie ni wajinga na wapumbavu sana, so unachekelea watoto wako kuja kuwa wamachinga baadae huku watoto wa sasa wa wakina Nape na Mwigulu waki viongozi?

Kwa nini mnakuwa wajinga kiasi hiki? Yaani mnashangilia ubaguzi wa kazi? Kwenye kodi pia wanabagua?
 
..Mzee Mwinyi mwanae ni Raisi kule Znz.

..Mzee Mkapa mwanae ni Katibu Mkuu wa wizara.

..Mzee Kikwete mwanae ni Naibu Waziri.

..Mama Samia mwanae ni Mbunge.

..Sasa viongozi wa aina hiyo ndio wanatushauri wenetu wawe bodaboda.
Na sisi tuna shangilia tulivyo vilaza, Mkuu shida ni Ujinga wa Raia, nchi ina Raia wajinga sijawahi ona
 
kaendeshe bodabofa jinga wewe huku watoto wa majaliwa na mwinyi wakifanya kaz BOT NA TRA.
Mkuu nchi ina wajinga sana, wao watotobwao wako hadi Umoja wa Matifa huko New York, tena wameajiriwa kwa Vimemo, huku watoto wa Choka mbaya wakiambiwa waende Ualimu na TOYO
 
Ndio maana wenye akili tumemuelewa kwanin hao viongoz wa ccm wanazunguka kudanganya kuwa bodaboda ni kaz nzuri wakati watoto wao hawaendeshi bodaboda badala yake wanaganya kaz BOT.NA TRA.
Mkuu shida nchi ina wajinga nazani asilimia 90 kutwa nzima ni wanadanganywa tu
 
Ni mfano usio sahihi wala hauna mantiki hii ni duni vipato ni tofauti kila mtu na riziki yake na utaftaji wake ...Atambue kwamba hata ambao Wana vipato vya juu ni wachache sana mno .

Yeye ni mwanasiasa na wenzio wanasiasa wanajua kuanzia kupiga dili na kuiba , sio lazima kwani hapo unagusia wananchi wa hali ya chini kabisa.. wanasiasa wote sijui lema na wenzio CCM wote akili sawa wao ndo wanufaika na pesa za wananchi ...je hao bodaboda waache kazi then waende wapi?

Kuna watu wamekaa nje miaka mpaka 20 ila wanaporudi bongo wanajua Kuna tofauti ya kule na huku ...wale wenzetu wameendelea sana unaweza kutoka kule baada ya kukaa sana ukaja bongo ukapaona kama pananuka ila ukiwa na akili unalow matarajio ukirudi bongo kwamba hapawezi kuwa kama ughaibuni

.Wenzetu miaka miwili basi kila kitu anaona kinyaa ni ushamba mtupu ..
Kwa nini viwe tofauti? Kwa nini wao wafanye kazi BOT, kazi za Umoja wa Mataifa na kwingineko? kama ni shida ya kazi hata watoto wa Waziri wawe na shida na kazi.

Watoto wao wanafanya kazi New York theb wanakuja kuwahadaaa wajinga nyie kwamba kaendesheni toyo na kasomeni Ualimu
 
Back
Top Bottom