Lema: Nikimuona mtoto wa Waziri Mkuu Majaliwa au wa Rais Mwinyi anaendesha Bodaboda ndipo nitaomba radhi

Lema: Nikimuona mtoto wa Waziri Mkuu Majaliwa au wa Rais Mwinyi anaendesha Bodaboda ndipo nitaomba radhi

Happy ki ukweli amekosea...!! Nadhani hata kwenye kampeno zake alikuwa akiwatumia hawa Maafsa Usafirishaji kwenye misafara yake awaombe radhi kwa kweli....!!
Sidhani kama umeelewa na shida iko hapo
 
Hiyo sio point, hao tayari ni matawi ya juu. Tunazungumzia watu wa kipato cha chini ambao ndio wengi. Na ndio wapiga kura ndio maana JPM alikuwa makini sana na hili kundi. Huenda hao unaowasema walitumia bodaboda ndio wakafika hapo walipo.
 
Hawa ccm wangekuwa na akili na nianjema wasingeruhusu hawa bodaboda kuendesha bila kuwa na leseni na bima
 
Boda boda sio kazi nzuri

Kuchimba madini (uanaapolo )sio kazi nzuri.

Kuzibua vyoo sio kazi nzuri.

Kuosha magari sio kazi nzuri.

Kufagia barabara na kusafisha vyoo sio kazi nzuri

Lakini

Kazi zote hizi ni kazi Halali , kipato Halali japo hatarishi.

Ila ukahaba, kuuza MADAWA ya kulevya, ujambazi, wizi, ufisadi, utapelo ni KAZI HARAMU sio nzuri machoni kwa watu na Mungu.

Ni heri hao wajuu.

Lakini wanasiasa wanawatumia vibaya kuhalalisha uungwaji mkono wa madaraka yao.

Na walio wengi elimu duni hawajitambui wanatumika tu Kisha wanaendelea na tabu zao kama kawaida.

Inasikitisha
 
Lema aache ushamba. Mtoto wa PM ataendaje kuendesha boda boda? Ndiyo maana kwenye jamii kuna matabaka.

Kuna waendesha boda boda na kuna Wahandisi, kuna walimu na mama ntilie, kuna wabunge na wapiga kura, kuna watawala na watawaliwa.

Sasa mtoto wa pm ni privileged hana sababu ya kuwa boda boda, lakini hiyo haifanyi kuendesha boda kuwa siyo kazi. Atulize hicho kichwa chake au wamempa crack huko Canada?
Muulizeni kwanini Makamu Mwenyekiti wao TL haishi Tegeta kwa Ndevu Uswahilini ila anaishi Tegeta masaiti(ushuani).
 
Ikiwa takwimu hiyo huna au hujui huna basi tatizo kuanzia kwako
Anazo takwimu za vifo na majeruhi kutokana na ajali za barabarani ili tuone kati ya bodaboda na magari nani anachinja zaidi kwa mwaka?
 
Lema anakoelekea anaweza kuleta Shida Kwenye Jami iliyotulia!
Fala tu anaongea ujinga,ukute kwenye ukoo wao wapo Bodaboda wengi tu,maisha yanasonga.Ushamba unamsumbua,kukaa ukimbizini CANADA miaka miwili basi ashajiona tycoon!
 
kaendeshe bodaboda huku watoto wa majaliwana mwinyi wakifanya kaz BOT NA TRA
Kwani wanaofanya kazi TRA na BOT wote ni watoto wa viongozi?
Mbona mimi kuna Sister wangu Mtoto wa Uncle,Mkulima yupo Kijijini uko,lakini mwanae ni meneja ndani ya TRA!
Lema aache ushamba!
 
Uchumi wa canada na Tanzania unafanana Hilo pia ameliangalia.kuna level mbili za umasikini absolutely na kuna Relative Poverty sisi Africa tupo kwenye absolutely asimilia kubwa wa wananchi hawana uwezo wa kupata.

Nahitaji ya msingi ya kila siku ila wenzetu wapo kwenye Relative ambapo masikini anapimwa kwa kukosa kumeet maisha ya luxury ndio maana watoto wa viongozi wanaweza kusoma na watoto wa masikini kwasababu shule za kawaida bado zina standard nzuri ya kuweza mtu kusoma je ni the same kwa hapa bongo?

Ningemuelewa Lema asingetumia neno laana kwa bodaboda lakini pia angekuja na njia badala ya nini wafanye bodaboda badala ya hiyo kazi
Kwani hiyo umaskini ni laana ujue jua hizo standards haziko kwa bahati mbaya lazima upigane ili utoke hapo, shida inakuja hapa wale ambao wanatuongoza akili zao zimegota wanafikiri kumtoa mtu kwenye huo umaskini ni kuwapa fursa ya vijana kuwa boda boda bila kujua kwamba unazalisha matatizo mengi kwakuwa bodaboda haiwezi kuwa public transport ndiyo maana hata usipokuwa na leseni na bima wao wanaona sawa tu.
 
Mbona hajamtaja mtoto wa Samia? Anaogopa kuminyiwa mrija wa asali?
Hajataja mtoto wa Samia Kwa sababu lema kwa akili yake finyu anaona kazi za maana ni zile za kuteuliwa na rais au BOT, Samia ana mtoto wake anauza matairi pale kariakoo na kuna watu wanamuona Fala yaani wanajiuliza kakosa nini Kwa mama yake, lkn kiuhalisia jamaa anatengeneza mpunga kuliko hata walioteuliwq kuwa maRC/DC. Si ajabu hata huyu mkimbizi wa mchongo Ile kazi ya kuuza matairi anaichukulia kama biashara ya laana ndo maana hajataja watoto wa Samia.
 
Kazi zenye maslahi ni nyingi hao watoto wa majaliwa na mwinyi wataweza kufanya kazi zote zenye maslahi? Je wewe unafanya kila chenye maslahi? Kila mtu afanye anachokimudu msipangie watu cha kufanya.
Kwa Nini Huwezi kukuta Mtoto wa Kiongozi ni dereva Bajaj au bodaboda?.
 
Kwa Nini Huwezi kukuta Mtoto wa Kiongozi ni dereva Bajaj au bodaboda?.
Jibu ni simple tu Wana nafasi ya kupata kazi zenye maslahi makubwa kuliko ya uboda boda! So kutofanya uboda boda haimanishi hiyo kazi ni mbaya na ya laana.
 
G. Lema yuko sahihi 100% tatizo dunia ya sasa haitaki ukweli. Pia Lema bodaboda ni vigumu kumuelewa uwezo mdogo
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Lema amesema endapo atamuona mtoto wa Waziri mkuu mh Majaliwa au mtoto wa Rais Mwinyi anaendesha Bodaboda ndipo ataomba radhi.

Lema amesisitiza Kuwa Bodaboda ni Kazi isiyofaa inayouwa na kuwapa ulemavu Vijana Wengi.

Lema amenena haya kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Mlale Unono!

======

"Nikimuona mtoto wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa au Mtoto wa Rais Mwinyi anaendesha bodaboda na kudai ni kazi ya heri nitaomba radhi. Bodaboda ni kazi ya mateso,imeumiza watu na kujeruhi watu wengi.Acheni kudanganywa na Serikali iliyo kosa mbinu za kuokoa maisha yenu. Umasikini sio sifa."

View attachment 2539929
Ujinga mtupu. Wewe jiulize BABA YAKE Waziri Mkuu alikuwa na cheo gani hadi kamsomesha mwanaye hadi kuwa Waziri Mkuu. Baba yake Waziri Ng'wigulu alikuwa mtu wa kaeaida, kwa ujumla karibu mawaziri wote CCM ni watoto wa maskini. Wacha ya kina Mbowe wala hakusoma nadhani ni Form 3, lakini bilionea mali za kurithi. Iweje umlinganishe mbowe leo na bodaboda au udharau bodaboda? Watanzania si wote ni matajiri wa kurithi kama CHADEMA.
 
Kama nchi unadhani kuwaingiza vijana hawa wa miaka 15 hadi 30 kwenye kazi ya uboda boda itaisaidia nchi kupiga hatua
Watakula wapi? Wanaingizwa au wanaingia wenyewe.


Hao vijana ni wanaona Bora waende huko ili mkono uende kinywani
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Lema amesema endapo atamuona mtoto wa Waziri mkuu mh Majaliwa au mtoto wa Rais Mwinyi anaendesha Bodaboda ndipo ataomba radhi.

Lema amesisitiza Kuwa Bodaboda ni Kazi isiyofaa inayouwa na kuwapa ulemavu Vijana Wengi.

Lema amenena haya kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Mlale Unono!

======

"Nikimuona mtoto wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa au Mtoto wa Rais Mwinyi anaendesha bodaboda na kudai ni kazi ya heri nitaomba radhi. Bodaboda ni kazi ya mateso,imeumiza watu na kujeruhi watu wengi.Acheni kudanganywa na Serikali iliyo kosa mbinu za kuokoa maisha yenu. Umasikini sio sifa."

View attachment 2539929
Huyu kachanganyikiwa, na amekwenda mbali kuwataja watoto wa Majaliwa na Mwinyi aanze na watoto wake kwanza.

Ni hali ya dunia nzima, hakuna uwezekano wa serikali kuwa mwajiri mkuu katika nchi inayojivunia kuongezeka kwa watu kila kukicha. Ni changamoto inayokwenda na uhalisia wa utakatifu wa maisha ya binadamu.

Nigeria ina changamoto ya watu kuwa wengi sana lakini ni hao hao wanaomtajirisha Dangote na mabilionea wengineo.

India ina changamoto ya watu wengi lakini ni hao hao wanaochukuliwa na makampuni makubwa ya Marekani na Uingereza wakiwa wataalamu wa kompyuta na masuala ya mawasiliano kwa ujumla.
 
Kwani hiyo umaskini ni laana ujue jua hizo standards haziko kwa bahati mbaya lazima upigane ili utoke hapo, shida inakuja hapa wale ambao wanatuongoza akili zao zimegota wanafikiri kumtoa mtu kwenye huo umaskini ni kuwapa fursa ya vijana kuwa boda boda bila kujua kwamba unazalisha matatizo mengi kwakuwa bodaboda haiwezi kuwa public transport ndiyo maana hata usipokuwa na leseni na bima wao wanaona sawa tu.
Kazi nyingi hazina maana sijui kwanini lema kaganda kwenye bodaboda unajua cashier wa pale Mlimani city analipwa kwa mwezi Laki 1.5 wakati bodaboda wastani kwa siku anaingia elfu 30 ambayo ukizidisha kwa mwezi unakuta ni laki 3 ni zaidi ya huyo cashier
 
Una uhakika kuwa viongozi wote wa CCM Wana vipato vikubwa!

..Ndio.

..viongozi wa Ccm wanatembelea ma-V8 yaliyonunuliwa kwa fedha za umma.

..Na tuache kudanganyana kwamba bodaboda ni kazi yenye tija na future nzuri.

..Tujitahidi uchumi wetu uzalishe ajira za kudumu, zenye vipato vizuri, na pensheni.
 
Back
Top Bottom