PreGE2025 Lema: Simba na Yanga zinanikera, namuomba Mungu aziondoe mara moja

PreGE2025 Lema: Simba na Yanga zinanikera, namuomba Mungu aziondoe mara moja

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Huyu naye kaishiwa hoja.Hayo mabadiliko anayoyaona watanzania hawaangaiki nayo nikwasababu yeye hayuko kwenye madaraka yakisiasa wakiwa wengine anaona hawafai.Sio Tz pekee ndio kwenye mashabiki wa mpira na uko kote wananchi wanaishi maisha yao ya furaha na maendeleo wanafanya.Sasa makasiriko yake hasiyalete kwenye furaha za watu,kwasababu sio watu wote wanataka hayo mabadiliiko anayoyataka yeye.Aje na hoja konki zitakazoshinda mioyo ya watu,watu wataziunga mkono kama hana atulie watu waburudike.
Tanzania hakuna mashabiki kuna wajinga wanao shabikia mpiraz haiwezekani asubuhi hadi usiku mada ziwe ni Mpira hata Barazili na Argentina hakuna huo ujinga
 
Lema hapa kazingua

ingefurahisha kwamba awashauri mpira usiwafanye wasahau mambo ya msingi kama sisi hapa ulaya
 
Lema aachane ama ajitahidi sana kutokubeza mambo ya soka, hasa hizi team mbili za simba na yanga. Mpira ni hisia na sidhani wanaopenda mpira ni kikwazo cha siasa. Aina ya siasa za hapa nchini zimeumiza sana wapinzani, hivyo kwenye soka wakawa salama. Ni sehemu inayobeba hisia zao, na wakabaki salama kuliko kwenye siasa za upinzani.

Lemw anatakiwa adhibiti hisia zakez maana hazungumzii na watu wanaopima hoja kimantiki. Anatakiwa atazame hadhira yake anayoongea nayo, na sio kuweka mbele hisia zake.
Boya huyo

Alitukana maaskofu , masheikh , leo kaingia Msimbazi na Jangwani

Hao ndio wanaitaka dola😂😂
 
Ukitaka ufokewe ziseme timu hizo na mashabiki wake
Hata upendwe kiasi gani 😄
Mpira unaweza kutumika kwenye ukombozi hapa inabidi CHADEMA tuingize counter agents ndani ya hizi timu nina imani CCM wanazitumia sana hizi timu ili kuzubaisha Watanzania.
 
Lema aachane ama ajitahidi sana kutokubeza mambo ya soka, hasa hizi team mbili za simba na yanga. Mpira ni hisia na sidhani wanaopenda mpira ni kikwazo cha siasa. Aina ya siasa za hapa nchini zimeumiza sana wapinzani, hivyo kwenye soka wakawa salama. Ni sehemu inayobeba hisia zao, na wakabaki salama kuliko kwenye siasa za upinzani.

Lemw anatakiwa adhibiti hisia zakez maana hazungumzii na watu wanaopima hoja kimantiki. Anatakiwa atazame hadhira yake anayoongea nayo, na sio kuweka mbele hisia zake.
Ana very low IQ
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema ameendelea kusema kiwa wakazi wa Dar es Salaam wamekuwa nyuma katika harakati za kudai mabadiliko na badala yake wanayapa kipaumbele mambo yasiyokuwa na maana ikiwemo ushabiki wa mpira wa miguu hususan kwa timu za Simba na Yanga.

View attachment 3307480
Huyu Lema ni mpumbavu sana, sasa nimejuwa kuwa kweli aliishia sekondari.

Michezo na muziki katika mataifa mbalimbali zilitumika kuunganisha watu wenye itikadi tofauti.

Kuna nchi zilikuwa kwenye vita lakini wakati wa michezo walisimamisha wakawa pamoja kuunga mkono timu ya taifa lao
 
Mpira unaweza kutumika kwenye ukombozi hapa inabidi CHADEMA tuingize counter agents ndani ya hizi timu nina imani CCM wanazitumia sana hizi timu ili kuzubaisha Watanzania.
Hao jamaa wana mbinu zaidi ya mia
Inawezekana kabisa
Hebu fikiria ushabiki wa mpira ulivyo na ngumu
Utajua kwa comments za watu tu

Kweli inabidi mpandikize watu huko 😄
 
Namkubali sana Lema ila hapa amekosea kiasi fulani.
Mpira umewapa ajira watu wengi tu kuanzia wachezaji coaching team, management, wajasiriamali wa kwenye matukio ya mpira na wauzaji wa bidhaa za club husika, watu wa vyombo vya habari, n.k.
Bila hamasa na huo ushabiki kusingepatikana hizo faida.
Watu wanapenda kupata furaha na ushabiki wa hizo timu huwapa furaha.
Kama unakula, unavaa, unahitaji furaha japo kwa jambo dogo.
Huwezi kuita mpira vitu vya kijinga au kitu kisicho muhimu.

Kwa upande wa pili wanaona siasa inawanufaisha moja kwa moja watu wachache ambao ni wanasiasa.
Siasa ukiweka sana hamasa kuna uwezekano wa kujikuta jela, kupata ulemavu, kuuwawa, kupotea au kufilisika. Mfano Ben Saa8, Soka, Mawazo, na wengineo.

Sasa mtu anaona ajiweke kwenye hatari yote hiyo kwa manufaa ya nani?
Si bora aende kwenye furaha kwenye mpira?
Lakini ukiangalia kwa undani kwenye siasa unaweza kuhamsika au kuhamasisha ukaleta maendeleo makubwa kwa jamii yako na uzao wako ujao. Sema siasa unahitaji Martyrdom (kujitoa muhanga) au sacrifice (kujitoa sadaka).
Mfano anayopitia Lissu au yaliyo wakuta akina Patrice Lumumba, Martin Luther King Jr, Che Guavara, Malcolm X, au akina Ben na Soka.
Lema ni bwege tu! Bado tabia za wizi wa magari hazijamtoka.
 
Mkuu umezunguuka sana..kifupi siasa ni utapeli!
 
Ukweli mchungu Ila hizi timu zinawafanya Watanzania kuzidi kuwa wajinga

Hakuna tofauti ya mtanzania mwenye degree na ambaye hajui kusoma

Kuna siku nilikuwa nabishana jamaa mmoja namwambia hizi timu CCM anazitumia kutawala bila usumbufu!!

90% ya mashabiki wa hizi timu ni wajinga

Juzi tena Kuna mfanyakazi wangu anaomba ruhusa kwa mkuu wake eti akaangalie mechi ya Simba na almasry nilicheka Sana yaani uondoke kazini muda wa kazi kisa kwenda kwenye mpira?

Huu ukweli Lema kaongea hizi timu zingefutika au kuacha kubebwa soka la Tanzania lingeenda mbali Sana!!

Uchawa wote uanzia kwenye hizi timu
Mzee kwenye suala la maendeleo ya soka simba na yanga zinaplay part kubwa sana.

Kwenye suala la mapato na kodi, simba na yanga kila mmoja kwa nafasi yake wamekuzidi kwenye uchangiaji.

Hata kwenye namna ya kuendesha biashara pia, they are best than you.

Mjinga ni wewe tu.

Sijui nataka kusemaje ila jaribu kufikiria nawe utanufaika vipi na tomu moja wapo au zote kwenye biashara zako.

Think positively.
 
Huyu siasa zimemshinda

Siku akiwq raisi hajui kuwa atatakiwa kuimarisha sekta ya michezo yeye anawaza kuhomoa

Kama ccm wamemzidi akili na power akazitafute sio kuwa mjinga kiasi hiki
badala yake wanayapa kipaumbele mambo yasiyokuwa na maana ikiwemo ushabiki wa mpira wa miguu hususan kwa timu za Simba na Yanga
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema ameendelea kusema kiwa wakazi wa Dar es Salaam wamekuwa nyuma katika harakati za kudai mabadiliko na badala yake wanayapa kipaumbele mambo yasiyokuwa na maana ikiwemo ushabiki wa mpira wa miguu hususan kwa timu za Simba na Yanga.

View attachment 3307480
Ni kweli ila Yanga tu ndiyo inabidi ife maana haina mafanikio yoyote kimataifa, wao kazi yao ni kupambana na timu za mchangani tu kuaminisha mashabiki wao kuwa wao ni timu kubwa wakati hawana lolote la kujivunia.
 
Kila siku mnasema watanzania wote wanafurahia na kutekeleza NR NE, Sasa watanzania gani ambao hawafuatilii Mambo ya chadema?
Yanafuatiliwa mtandaoni tu, mtaani ni habari za Simba na Yanga huwezi enda maeneo yenye population km sokoni, au sehemu yyte inakusanya ukakutn na upuuzi wa NR
 
Back
Top Bottom