PreGE2025 Lema: Simba na Yanga zinanikera, namuomba Mungu aziondoe mara moja

PreGE2025 Lema: Simba na Yanga zinanikera, namuomba Mungu aziondoe mara moja

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
mtu mwenye utimamu wa akili hawezi tekwa na Simba na Yanga. Waafrika ni mambumbumbu sana. wanaacha mambo ya msingi wanabaki kwenye uzwazwa !
Very subjective.
Kuna wanasheria, daktari, wahasibu, na fani zingine wameajiriwa sekta ya mpira.
Hao wote hawawezi kuwa mazuzu.
Uhuru wa mawazo au fikra ni muhimu.
 
Ukweli mchungu Ila hizi timu zinawafanya Watanzania kuzidi kuwa wajinga

Hakuna tofauti ya mtanzania mwenye degree na ambaye hajui kusoma

Kuna siku nilikuwa nabishana jamaa mmoja namwambia hizi timu CCM anazitumia kutawala bila usumbufu!!

90% ya mashabiki wa hizi timu ni wajinga

Juzi tena Kuna mfanyakazi wangu anaomba ruhusa kwa mkuu wake eti akaangalie mechi ya Simba na almasry nilicheka Sana yaani uondoke kazini muda wa kazi kisa kwenda kwenye mpira?

Huu ukweli Lema kaongea hizi timu zingefutika au kuacha kubebwa soka la Tanzania lingeenda mbali Sana!!

Uchawa wote uanzia kwenye hizi timu
Wapo wengi tu wanashabikia hizi timu na wanamchango mkubwa kwenye taifa letu, wapo madaktari, wafanyabiashara na walipa kodi wakubwa, wapo watu wakubwa wenyenafasi kwenye kuchangia shughuri za maendeleo kwenye Taifa letu na nimashabiki wa hizi timu.
Hasa unaposema penye mashibiki kumi wahizi timu basi tisa kati yao ni wajinga nakuwa sikuelewi labda km umeamuwa kuwakashifu watanzania au hujui ulichoongea nikitu gani.
 
Sijaona uwezo wenu ukaniridhisha kwamba mkipewa nchi mtalenda kombe hapa zaidi ya urafi wa madaraka tu
 
Kwenye ushabiki atuache kwanza, aende kanada atatukuta
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema ameendelea kusema kiwa wakazi wa Dar es Salaam wamekuwa nyuma katika harakati za kudai mabadiliko na badala yake wanayapa kipaumbele mambo yasiyokuwa na maana ikiwemo ushabiki wa mpira wa miguu hususan kwa timu za Simba na Yanga.

View attachment 3307480
 
Namuunga mkono simba na yanga zimeleta mental illness kwenye nchi
 
Hii ndo aina ya upinzani tulio nao nchini. Wakipewa nchi watakuwa madikteta wasioelezeka. Ninamshukuru Mungu kwa kutuepusha na hawa wahuni wanaoitwa CHADEMA. Lema hana akili kabisa. Karibu makundi muhimu yote ya kimkakati kashagombana nao.
 
Acha upotoshaji, anajaribu kuwaamsha watu kwa lugha ngumu na sio kugombana nao. Yaani anataka kura, lakini sio kwa kupitia uzito wa wananchi.
 
Ukweli mchungu Ila hizi timu zinawafanya Watanzania kuzidi kuwa wajinga

Hakuna tofauti ya mtanzania mwenye degree na ambaye hajui kusoma

Kuna siku nilikuwa nabishana jamaa mmoja namwambia hizi timu CCM anazitumia kutawala bila usumbufu!!

90% ya mashabiki wa hizi timu ni wajinga

Juzi tena Kuna mfanyakazi wangu anaomba ruhusa kwa mkuu wake eti akaangalie mechi ya Simba na almasry nilicheka Sana yaani uondoke kazini muda wa kazi kisa kwenda kwenye mpira?

Huu ukweli Lema kaongea hizi timu zingefutika au kuacha kubebwa soka la Tanzania lingeenda mbali Sana!!

Uchawa wote uanzia kwenye hizi timu
Acha kuwa nyumbu wewe. Unajua mpira wa miguu umeajiri watu wangapi? Viongozi wenu wadananda wanamlaumu kila mtu isipokuwa wenyewe. Pmbv.
 
Anachokisema ni kweli,japo wengi comments naona wanampinga,hizi timu zinatumika mara nyingi kubadilisha upepo wa mijadala mingi ya msingi............unatoka mfano kimara unaacha mjadala Yanga, Simba......unafika Riverside....unakatisha mabibo hadi Karume pale kijiweni,mijadala ni hiyo hiyo tu...... Mtu huyo huyo anatoka kwenye mabishano akiugua au kwenda hospital unakuta anaonja joto la jiwe na kuaanza kulia lia........kwa hili Lema yuko sahihi
 
Hii ndo aina ya upinzani tulio nao nchini. Wakipewa nchi watakuwa madikteta wasioelezeka. Ninamshukuru Mungu kwa kutuepusha na hawa wahuni wanaoitwa CHADEMA. Lema hana akili kabisa. Karibu makundi muhimu yote ya kimkakati kashagombana nao.
Hawa ni wahuni tu walianza na bodaboda, polisi, mahakama, machinga, vikoba, walimu, wazanzibari, sasa Simba na Yanga. Eti hawa ndio wapinzani na kuna nyumbu wanawaunga mkono.
 
Lema sasa anaingilia vitu vya watu ,sasa unavyosema mpira ufutwe je ajira hizo zilizotokana na mpira zitasaidiwa na Chadema? Kuna wengin nao siasa hawazipendi wanaomba vyama vyote vifutiliwe mbali.

Tuheshimu haki za watu ,kila mtu ana haki ya kupenda atakacho ili mradi asivunje sheria.

Tatizo la kujiona uko sahihi, na wengine siyo sahihi. Mpira ni ajira kama vile ilivyo kwa bongo flavour, ngumi, riadha nk
 
Namkubali sana Lema ila hapa amekosea kiasi fulani.
Mpira umewapa ajira watu wengi tu kuanzia wachezaji coaching team, management, wajasiriamali wa kwenye matukio ya mpira na wauzaji wa bidhaa za club husika, watu wa vyombo vya habari, n.k.
Bila hamasa na huo ushabiki kusingepatikana hizo faida.
Watu wanapenda kupata furaha na ushabiki wa hizo timu huwapa furaha.
Kama unakula, unavaa, unahitaji furaha japo kwa jambo dogo.
Huwezi kuita mpira vitu vya kijinga au kitu kisicho muhimu.

Kwa upande wa pili wanaona siasa inawanufaisha moja kwa moja watu wachache ambao ni wanasiasa.
Siasa ukiweka sana hamasa kuna uwezekano wa kujikuta jela, kupata ulemavu, kuuwawa, kupotea au kufilisika. Mfano Ben Saa8, Soka, Mawazo, na wengineo.

Sasa mtu anaona ajiweke kwenye hatari yote hiyo kwa manufaa ya nani?
Si bora aende kwenye furaha kwenye mpira?
Lakini ukiangalia kwa undani kwenye siasa unaweza kuhamasika au kuhamasisha ukaleta maendeleo makubwa kwa jamii yako na uzao wako ujao. Sema siasa unahitaji Martyrdom (kujitoa muhanga) au sacrifice (kujitoa sadaka).
Mfano anayopitia Lissu au yaliyo wakuta akina Patrice Lumumba, Martin Luther King Jr, Che Guavara, Malcolm X, au akina Ben na Soka.
Lema anatabia ya kuwasilisha hoja zake kwa kutumia kauli tata na Kali zaidi..lkn ukifikiria kwa umakini...yupo sahihi..tatizo ni kwamba watanzania...akili zao ni ndogo.
(Sio kosa lao)..kuelewa ujumbe anaotoa Lema.
 
Acha upotoshaji, anajaribu kuwaamsha watu kwa lugha ngumu na sio kugombana nao. Yaani anataka kura, lakini sio kwa kupitia uzito wa wananchi.
Atajibiwa kwa lugha ngumu kwenye sanduku la kura
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema ameendelea kusema kiwa wakazi wa Dar es Salaam wamekuwa nyuma katika harakati za kudai mabadiliko na badala yake wanayapa kipaumbele mambo yasiyokuwa na maana ikiwemo ushabiki wa mpira wa miguu hususan kwa timu za Simba na Yanga.

View attachment 3307480
Binafsi nashauri Wana Chadema WOTE waache kushabikia Simba na Yanga. Na mwana Chadema yeyote akayebainika anaishabikia Simba au Yanga afukuzwe kwenye chama maana atakuwa amepewa fedha na Abduli akidhoofishe chama! Ahahahahaha!!!
 
Back
Top Bottom