KERO Lemara Kati, Kata ya Lemara Kati - Arusha na maeneo ya Njiro barabara ni mbaya kama tupo kijijini

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
Barabara ya Lemara Kati, Kata ya Lemara Kati, Jiji la Arusha pamoja na maeneo ya Njiro karibu na Fiber Board imekuwa katika hali mbaya kwa muda mrefu ya barabara, inaonekana kama tupo kijijini.

Usafiri wetu ni mkubwa Bajaj kutokana na ubovu wa barabara hiyo. Wakati maeneo mengine kama Engosheraton, Olasiti na Ngareno yakiwa tayari yana barabara za lami, wakazi wa Lemara bado tunaishi kwa matumaini ya ahadi za viongozi kwamba barabara hiyo itawekwa lami.

Jambo lingine ni kuwa ikifika Saa 12 jioni nauli huwa karibu Sh 1,000, lakini kuanzia saa 1 usiku inaweza kufikia Sh 1,500 hadi Sh 2,000 kutokana na uhaba wa daladala na hali ya barabara.

Tunavumilia vumbi, mashimo na usumbufu wa usafiri, huku viongozi wakitoa ahadi za mara kwa mara bila utekelezaji wa kudumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…