Ila kajifunza
Sio kwamba waliamua kumtunza kwa muda huko ili kukidhi shauku ya raia wengi waliotaka kuona Sabaya akiwajibishwa kwa makosa yake baada ya MZEE kufariki?

Hasa ukiangalia namna walivyolimaliza hili swala.
 
Wadau nawasabahi.HATIMAYE DC MSTAAFU wa Hai GEN.SABAYA yupo HURU pamoja na Kesi zote 3 kumkabili na AMEZIMALIZA kwa KUKIRI MAKOSA kwa DPP na KUACHIWA HURU kwa STAILI ya PLEA BARGAINING.
Sasa nimeamini UKIFUNGWA TANZANIA ni UZEMBE wako.Moja ya Makosa ya GEN SABAYA ni KUONGOZA GENGE la UHALIFU kwa kutumia SILAHA kosa ambalo ni KUBWA lakini AMEKIRI na kuachiwa HURU.Watanzania Tutarajie MAJAMBAZI Mafisadi Wahujumu Uchumi Wauza Madawa hakuna ATAKAYEFUNGEA kwa Mtindo huu wa "PLEA BARGAINING"
Narudia tena UKIFUNGWA TANZANIA ni UZEMBE WAKO kwani PLEA BARGAINING ni OFFER kwa WAHALIFU
 
Hatimae haki imetendeka,njia zote haramu za kukukomoa zimeshindikana!
"Kweka" na Baba mkwe Gang wa Hai,leo ni siku mbaya kwenu!
Walamba Asali mjifunze kwamba kuna siku moja pia itatokea!

Tunaomba ripoti ya CAG ijadiliwe kwa Uhuru kabisaa!

Mungu ni ni Mwema...
Karibu Uraiani Jemedari Sabaya!
Future yako bado ipo kubwa kabisa kwenye siasa,Achana na CCM ya asali Boyz kwa sasa!

Utumishi na uhusika wa kweka kwenye hili unapaswa kuchunguzwa,hata kama si leo,jinai huwa haiozi.
 
Sheria ni za watu masikini?

Ukate watu masikio na miguu, upige watu, upore mali za watu na bado unaambiwa upo huru....
Hapo hata mm sijaridhika. Lkn nadhani kesi bado inaendelea kaachiwa kwa maana ya kupewa dhamana baada ya makosa ya uhujumu uchumi kufutwa ambayo kisheria hayana dhamana. Kinyume na hapo itakuwa ni dhuluma kwa waathirika.
 
aise hii Nchi mbona tamu sana ?

unakula milioni 50 unalipa faini ya milioni 5 ?

Wazee tuingie mzigoni mambo iko huku
 


God is good all the time
 
Uko sahihi mkuu. Kesi bado inaendelea kaachiwa kwa maana ya kupewa dhamana baada ya makosa ya uhujumu uchumi kufutwa ambayo kisheria hayana dhamana.

Sasa wasioujua kusoma na wakrupukaji wanapotosha.
 
MAANA PANA YA HUKUMU YA LEO
Nini maana ya hukumu hii ya kihistoria dhidi ya aliyekuwa mkuu wa wilaya Lengai Ole Sabaya baada ya kukiri kosa, kutiwa hatiani na kupewa adhabu ya kulipa faini na kuachiwa toka magereza kwa masharti.

Sasa mkuu huyu wa wilaya wa zamani hataweza kuteuliwa kushika nafasi ktk ofisi ya umma wala kugombea nafasi ya kisiasa kutokana na kupatikana na hatia kesi yake ilipokuwa inasikilizwa.

5 Apr2023
#BREAKING: SABAYA AACHIWA HURU BAADA ya KUSOTA MAHABUSU MIAKA 2...


Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, leo April 5, 2023 ameachiliwa huru na mahakama baada ya kufutiwa mashtaka saba yaliyokuwa yakimkabili, ikiwemo uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka na kuongoza genge la uhalifu. Mahakama imetoa uamuzi wa Lengai Ole Sabaya kulipa kiasi cha shilingi milioni 5 kama fidia kwa mwathirika na hapaswi kufanya kosa lolote la jinai kwa muda wa mwaka mmoja
 
Una maanisha mbowe nae hataweza kugombea nafasi yoyote? Maana alikutwa na hatia
 
Inamaana gani kupigwa faini ya 5mn Tano kama hakukutwa na hatia alafu achiwe Tena kwa masharti
SABAYA hajapatikana na hatia wala hajaombewa msamaha na walamba asali akina ZITTO au Askofu Shoo. Mwana ume ni kushina kesi sio kulamaba asali ikulu. Ok
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…