The Resident Magistrate Court in Moshi, Kilimanjaro has found former Hai District Commissioner, Lengai Ole Sabaya, guilty of the criminal charges, and sentenced him to one-year in community service with the condition that - #TheGuardian
 
Hii nchi Wenyenchi ndiyo wanaoijua,siyo Wananchi! Tusishangae akiteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa.
 
Amekomeshwa hatarudia tena mpumbavu huyo na namshauri awe anasikiliza ushauri wa lema akiendelea na kibri chake atafia gerezani.
 
Hongera sana Sabaya Mungu ni mkubwa sana sasa upo mtaani waliokufitini wataona aibu kubwa sana


USSR
Karma iz bitch
Kijana sabaya alikua anajimwambafy sana
For sure sabaya alikua anajitapa na kuumiza sana watu ...
 
Ilibid atolewe muda mrefu tu, kesi imepigwa sana tar ili kusubiri report ya CAG, Moto bungeni na mtaani umeanza kuwaka ndo wameona wamtoe ili tusahau report, kesho vyombo vyote vya habari ni kuhusu jamaa

Ametolewa leo ili kuficha madudu report ya CAG
 
Aliyewahi Kuwa mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya amehukumiwa Kifungo cha Nje cha Mwaka mmoja baada ya kukiri makosa na kuomba mahakama imwangalie kwa jicho la huruma.

=======
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, imemtia hatiani aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya mara baada ya kukiri kosa na kumfunga kifungo cha mwaka mmoja nje bila kufanya kosa lolote la jinai.

Sabaya amekiri kosa hilo kwa njia ya ‘Plea Bargaining, ambao ni mchakato wa makubaliano / maridhiano maalumu katika kesi ya jinai kati ya Mkurugenzi wa Mashtaka kupitia Mwendesha mashtaka na mshtakiwa ambapo mshatikiwa anaweza kukiri kosa moja au zaidi ili aweze kupata nafuu katika kesi inayomkabili.

Sabaya ambaye alisalia kwenye kesi namba 2 ya mwaka 2022 baada ya wenzake Sylvester Nyegu, Nathan Msuya, John Aweyo na Antero Asey ambao septemba 7, 2022 waliachiwa baada ya kufanya makubaliano mahakama na mwendesha mashtaka Mkuu wa serikali.

Msingi wa kesi hiyo kwa Mujibu ya hati ya mashtaka inadaiwa Mnamo Februari 21. 2021 Sabaya na waliokuwa wenzake hao walijipatia kitita cha Tsh Milioni 50 Kutoka kwa mfanyabiashara Alex Swai wakimtisha kutoa taarifa zake za ukwepaji kodi.

Ikumbukwe pia tangu kesi hiyo kuanza kwake Juni Mosi, 2022 haikuwai kusikilizwa kutokana na sababu mbalimbali za kisheria.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Salome Mshasha leo Aprili 05, 2023 ilifika Mahakamani kwa ajili ya kutajwa lakini upande wa mashtaka kupitia kwa Wakili Mwandamizi wa Serikali Verediana Mlenza akadai mshtakiwa ameomba makubaliano nje ya Mahakama na Mwendesha mashtaka Mkuu wa serikali.

Maombi ambayo Mahakama iliyaridhia na kumuachia huru Mshtakiwa huyo Lengai ole Sabaya kwa shart la kifungo cha nje kwa muda wa mwaka Mmoja, na kumtaka amlipe fidia ya Tsh Milioni Tano mfanyabiashara Elbariki Swai ambaye ni Muathirika wa tukio hilo.


Source: ITV Habari

Pia soma: Lengai Ole Sabaya aachiwa Huru
 
Daah
Kama binadamu tunatakiwa kuwa tunajifunza sana kwa Mambo kama haya tunapokuwa tunayasikia, tunayaona na kuyapitia.
Linganisha nguvu kubwa sana iliyotumika/rasilimali zetu zilivyotumika kwa ajili ya jambo lenye kutia watu aidha upofu au kwa namna ya pekee kuwafundisha watanzania jinsi mamlaka husika zilivyo aidha imara au dhaifu,
Mambo haya yote ni elimu kubwa kwetu kuendelea kutambua umuhimu /uhitaji wa katiba na sheria zenye kukidhi matakwa ya wananchi kwa wakati mahsusi wa sasa.
 
Kwa Kweli mama ameutendea haki mwezi mtukufu wa ramadhani kwa kumuachia sabaya.
 
Kama amekili makosa na amepewa hako kaadhabu kadogo itakuwa kuwa kiongozi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…