Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
basha lenu limekiri makosa kwasasa lina criminal record.Timu gaidi watanyooka tu wasiyempenda anakuja
Keshakatwa mkia, atakuwa anaishi kama Makonda/Bashite ambaye hata nyumba alizopora wenyewe wamezichukua.Timu gaidi watanyooka tu wasiyempenda anakuja
Karma iz bitchHongera sana Sabaya Mungu ni mkubwa sana sasa upo mtaani waliokufitini wataona aibu kubwa sana
USSR
DaahAliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya, ambaye amekuwa akikabiliwa mashtaka saba ikiwemo uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka na kuongoza genge la uhalifu leo Aprili 05, 2023 ameachiliwa huru.
Taarifa zaidi zitakujia hapa hapa baadae.
Chanzo: Jambo TV
===
Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, leo April 5, 2023 ameachiliwa huru na mahakama baada ya kufutiwa mashtaka saba yaliyokuwa yakimkabili, ikiwemo uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka na kuongoza genge la uhalifu.
Mahakama imetoa uamuzi wa Lengai Ole Sabaya kulipa kiasi cha shilingi milioni 5 kama fidia kwa mwathirika na hapaswi kufanya kosa lolote la jinai kwa muda wa mwaka mmoja.
Sabaya ambaye mapema asubuhi ya leo alifika kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Moshi, kabla uamuzi wa kuachiwa haujatangazwa, kupitia Kifungu cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai namba 91 kifungu cha 1A, kesi yake ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 2022 ilifanyiwa marejeo kama upande wa mshtakiwa ulivyoomba.
Mawakili upande wa Jamhuri waliiomba mahakama kubadilisha mashtaka ya Lengai Ole Sabaya kutoka kuwa ya kesi ya Uhujumu Uchumi na kufungua kesi yenye Mashtaka ya Makosa ya Jinai baada ya Lengai Ole Sabaya kuomba kufanya mazungumzo nje ya mahakama na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Ombi hilo la Sabaya lilikubaliwa na Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Salome Mshasha baada ya Mawakili wa Lengai Ole Sabaya kuridhia na kufutwa kwa kesi yake namba 2 ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 2022.
Baada ya kuridhia hilo, kesi mpya aliyofunguliwa Sabaya ni kesi kesi ya Jinai Namba 31/2023 ambayo ndani yake kulikuwa na mashtaka mawili mapya dhidi yake, kosa la kwanza likiwa ni kuchukua madaraka ambayo siyo yake.
Imeelezwa kuwa Lengai Ole Sabaya na wenzake, Januari 19, 2021 katika eneo la Masama Mbosho wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, bila kibali walivamia duka la Alex Evarest SwaI na kuchukua mali na kuzizuia na kujipatia kaisi cha fedha shilingi milioni 50.
Kosa la pili ni kuzuia upatikanaji wa haki ambapo Januari 19, 2021 katika maeneo tofautitofauti katika Wilaya ya Hai na Tulia jijini Arusha na maeneo tofauti ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, walikula njama za kumfanya Alex Swai kuwa ametenda kosa la kukwepa kodi.
Baada ya kusomewa mashtaka, Sabaya alikiri kufanya makosa yote hayo mawili mbele ya hakimu Salome Mshasha.
Kama Yona na Mramba Enzi zileKwahiyo kumbe ni mfungwa hapo alipo
Kqbisa..jambazi limerudi tena uraiani? tukae chonjo.
Sugu alipotoka Jela alirudi bungeniKuhukumiwa kifungo si inamaanisha kakutwa na hatia. Sasa wakili wake alikuwa anaongea upuuzi gani kuwa Sabaya anaweza kugombea nafasi za uongozi ikiwa tayari ni muhaini.
Kama amekili makosa na amepewa hako kaadhabu kadogo itakuwa kuwa kiongozi?Mambo mengine tusiwe tuna ingiza kichwa kichwa.
Sabaya amekiri makosa yake yote aliyo kuwa ameshtakiwa nayo, hata lile la uhujumu uchumi na kuhoji genge la uhalifu. Maana yake Sabaya ni jambazi.
Hastahili kugombea nafasi yoyote ya kisiasa wala ya serikali.
Ana makosa ya kijinai. Huyo wakili ni mihemko tuu ..
Makosa ya Sugu na Sabaya sawa?Sugu alipotoka Jela alirudi bungeni
Selikali ya mama haitaki uonevu ndio maana Sabaya katoka njeHakuna mtu anayemiliki Serikali acheni UZWAZWA