Mamlaka imeamua kunsamehe tu.....ashukuru Sana connection zake za kifamilia huko Ccm.
 
Lilikuwa n swala la muda tu Sabaya kuachiwa, ukiachana na kelele za wasiojua namna siasa za Tz zinakwenda.


Huyu jamaa, Bashiru na mwenzao Makonda ni watu waliojilimbikizia pesa nyingi wakati wa JPM, nadhani sasa ataenda kutulia ale mema ya nchi kutokana na pesa alizochuma.
 
Jamani kiswahili chetu mara nyengine kinaleta matatizo kwa sababu hatuna maneno sahihi ya kutumia katika situation fulani fulani. Sasa kama hapa penye taarifa hii. Neno kuachiliwa huru hapa linatatiza maana hakuna mahali inaposema kuwa amefutiwa mashitaka yake, kwa maana hiyo huwezi kusema kuwa yuko huru ikiwa ametolewa jela kwa dhamana na anangoja kesi yake itajwe tena. Mtu kuwa huru ni kuwa unaweza kufany autakalo na kwenda utakako bila ya kuviarifu vyombo vya dola na kuruhusiwa.

Labda wanaotuma hizi taarifa watueleze kuwa huyu mtu yuko huru wakimaanisha hana kesi tena na yuko huru kufanya yake kama watanzania wenzake au yuko nje kwa dhamana na masharti?
 
Atakua amejifunza vzur huu msemo
"Ishi vizur na watu,ujafa ujaumbika"[emoji4]
Awapi, huyo hata kwa muonekano inaonekana alikuwa VIP huko gerezani, sasa katoka atafune vizuri hela alizochuma enzi za JPM.
 
AHIMIDIWE YESU ALIKUFA NA KUFUFUKA ILI WATU WAKE WAPONE. KARIBU SAANA KAKA YETU NA MCHAPAKAZI NDUGU YANGU SABAYAA. KARIBU TUSHEREHEKEE SIKUKUU YA KUFUFUKA KWA BWANA YESU MWOKOZI WA ULIMWENGU. HAKIKA YESU WETU NI HAKIII. YAAANI NIKO NATIRIRIKWA NA MACHOZI YA FURAHA KWA KUACHIWA HURUU KAKA YANGU HUYU. MUNGU IBARIKI MAHAKA ZETU NA WANASHERIA WOTE WA SERIKALI.
 
Hapa ndipo panapo hitajika mabadiliko makubwa ya kikatiba, haiwezekani huyu anatoka ingawawa anatuhuma nzito ila kwa sababu ni mbowe au sabaya anatolewa na yule anafungwa kwa kwa vituhuma vile vya kijinga tuu ila kwa vile ni mtoto wa muuza vitumbua anaozea jela , maana ya kuwa na sheria ninini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…