Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya, ambaye amekuwa akikabiliwa mashtaka saba ikiwemo uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka na kuongoza genge la uhalifu leo Aprili 05, 2023 ameachiliwa huru.
View attachment 2577142
Taarifa zaidi zitakujia hapa hapa baadae.
Chanzo: Jambo TV
KINACHOENDELEA MAHAKAMANI MOSHI KUHUSU KUACHIWA HURU OLE SABAYA KESI ya UHUJUMU UCHUMI...
5 April 2023
KINACHOENDELEA MAHAKAMANI KUHUSU KUACHIWA HURU OLE SABAYA KESI ya UHUJUMU UCHUMI...
Mapema leo Aprili 05, 2023 kulisambaa taarifa za kuachiwa huru kwa Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Ole Sabaya.
Hata hivyo, hadi sasa Global TV ipo mahakamani Moshi na taarifa za uhakika ni kwamba siyo kweli kwamba Sabaya ameachiwa huru kama baadhi ya vyombo vinavyoripoti.
Hadi sasa kesi hiyo inasubiriwa kuanza kusikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Moshi, Salome Mshasha hadi hivi sasa 6:47 mchana bado shauri lake halijaanza kusikilizwa.
Kesi inayomkabili Sabaya ni ya Uhujumu Uchumi namba 2/2022 ya mwaka 2022. Msingi wa kesi hiyo iliyokuwa na mashtaka saba inadaiwa Sabaya na wenzake wanne walijipatia kitita cha shilingi milioni 30 kutoka kwa mfanyabiashara Alex Swai wakimtisha kutoa taarifa zake za ukwepaji kodi.
Kesi hiyo tangu kufunguliwa kwake Juni 1, 2022 haikuwahi kusikilizwa kutokana na sababu mbalimbali za kisheria, lakini ilipofika Septemba 7, 2022 washirika wanne wa Sabaya waliachiwa huru kwa makubaliano ya nje ya Mahakama na mwendesha mashtaka Mkuu wa Serikali.
Washirika hao waliokuwa watuhumiwa katika kesi hiyo ni pamoja na Sylvester Nyegu, Nathan Msuya, John Aweyo na Antero Asey ambao Mahakama iliwakuta na hatia na kutakiwa kutoa faini ya shilingi 50,000/= na fidia ya shilingi milioni 1 kwa muathirika wa tukio hilo ambaye ni Alex Swai.
Habari hii kwa hisani kubwa ya : Source : Global TV online