Lengai Ole Sabaya aachiwa Huru kwa sharti la kutofanya kosa la Jinai kwa kipindi cha mwaka mmoja
Gaidi! Nimesema hivii, hiyo kauli yangu itaishi. Chuga sio mchezo mchezo. Mtumishi gani wa umma unakutwa na mizigo ya pesa tena cash nyumbani? Alipata wapi kama sio mwizi? Mahakama imeshaamua lakini kila mtu anajua Sabaya ni jambazi na mwizi. Haki itapatikana kwingine kama mahakamani imekosekana. Tuupe muda nafasi.
Vipi yule kijana wa Nyari jambazi wa wizi wa magari na kuondoa maisha ya watu bado anaishi?
 
Sasa atamfanyia kiburi nani wakati jamaa yake kashadedi? Hawa wasasahivi watamtia ndani tena akileta upuuzi wake

Nimshauri tu Sabaya kama yupo humu:

Nakushauri ubadilike kabisa. Kwenda kwako ndani siku zote hizo sio mwanadamu kaamua bali ni Mungu wa Mbinguni aliona azuie usiendeleze uonevu na dhuluma. Mungu anakupenda ndio maana ametaka Ubadilike uwe mtu Mwema. Ikiwezekana Ungama kwa unayojua hayakuwa ya haki uliyowafanyia watu kwa kutumia nafasi yako.
Kumbuka Mungu huwainua Wafalme na Kuwashusha pia.

Nafasi bado unayo
 
Akafunge ndoa Sasa akafuge na ngombe kama wamasai wengine. Asahau vya kidimbwi
Ningekuwa moderator humu kazi yangu ingekuwa napitia comments za watu na kuwatoa kwenye hili jukwaa wajinga wajinga ningeanza na wewe,Mana unaandikaga ujinga sana alafu ueleweki na unajaza tu saver.
 
Kama anayo hekima japo ya kizibo cha soda, aende kwa aliowapigilia misumari na kuwakata masikio, akawaombe msamaha.

Halafu afanye tafakari kwa nini shetani alifanya makao katika nafsi yake. Aliweka mazingira gani hata yakawa kichocheo cha kuona kwenye nafsi yake ndipo mahali salama pa kuishi.

Matendo ya Sabaya, ni vigumu kuamini kama yanaweza kufanywa na binadamu halisi. Yalikuwa ni matendo ya kinyama yanayoweza kufanywa na shetani pekee. Na ili shetani akutumie kwa kiwango kikubwa kama ilivyokuwa kwa Sabaya, ni lazima uwe umemtengenezea mazingira mazuri ya pekee.
 
Ama kweli tutafute sana hela na ikishindikana basi tutafute ata connection za grade za Taifa

Maana haya maisha hayajawahi kuwa Fair ata siku moja, Ambao hawana HATIA siku zote wanaozea JELA

NB: sijasema jamaa Ana HATIA
 
Kumbe wanyang'anyi nao huachiwa huru hata baada ya kukutwa na hatia.
 
Afadhali sabaya kaingia jela kamalizana na walimwengu ataishi kwa amani...
Kuliko makonda anayeishi kwa mashaka mtaani hana furaha maisha yamesimama...
Humjui Makonda na maisha yake uraiani, moja kati ya watu waliochuma pesa za kutosha kwenye ule utawala basi ni Makonda na Bashiru.

Yani ni sawasawa na jinsi ambavyo Mwiguru anazichuma sasahivi, kisha utarajie eti akistaafishwa ataishi maisha ya taabu kiuchumi huku uraiani.

Wanasiasa wanalitafuna sana hili taifa.
 
Hongera sana Sabaya Mungu ni mkubwa sana sasa upo mtaani waliokufitini wataona aibu kubwa sana


USSR
Hakuna fitna alipelekwa ajifunze maisha na kuheshimu wakubwa.
Kwa sasa ataenda kuswaga tu ngombe
 
Back
Top Bottom