Lengai Ole Sabaya aachiwa Huru kwa sharti la kutofanya kosa la Jinai kwa kipindi cha mwaka mmoja
Inamaana gani kupigwa faini ya 5mn Tano kama hakukutwa na hatia alafu achiwe Tena kwa masharti
Baada ya kukiri mtuhumiwa anatiwa hatiani halafu adhabu itatolewa na mwendesha mashitaka kwa makubaliano maalum (plea bargaining).
Kwa hiyo, maelezo ya kuachiwa huru siyo sawa, kwa kuwa hapo kuna hatia na adhabu ila kwa utaratibu tofauti na ule wa kawaida.
 
Hongera sana Sabaya Mungu ni mkubwa sana sasa upo mtaani waliokufitini wataona aibu kubwa sana

USSR
Kuna uwezekano wa wale wanaodai "mungu ni fundi" kuukana ufundi huo leo....huku wakijiongezea uchuro na dhambi.
 
Una maanisha mbowe nae hataweza kugombea nafasi yoyote? Maana alikutwa na hatia
Mbowe hakukutwa na hatia, alikuwa na kesi ya kujibu. Kwa maneno mengine alitakiwa ajitetee, na inawezekana baada ya ushahidi wa utetezi ingewezekana akaachiwa huru kwa kuonekana hana hatia.
Kwa hiyo, kesi ya Mbowe iliondolewa na mshitaki au mlalamikaji (jamhuri).
 
Huyo ni mafia akiwa uraiani, hizi comments za hapa Jf zisiwafanye muone maisha ni mepesi hivyo.

Tukiweka ligi ya kutafutana kati yako na Sabaya huku uraiani, nina uhakika hata wiki haiishi unakuwa umepotezwa ila hapa unatamba[emoji1].

Juilize ni nani amethubutu kumalizana na Makonda licha ya kwamba yupo uraiani miaka yote?
Bila Madaraka hasa Polisi hana umafia, wowote,aanze ujinga wake aone
 
Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya, ambaye amekuwa akikabiliwa mashtaka saba ikiwemo uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka na kuongoza genge la uhalifu leo Aprili 05, 2023 ameachiliwa huru.

Taarifa zaidi zitakujia hapa hapa baadae.

Chanzo: Jambo TV

===

Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, leo April 5, 2023 ameachiliwa huru na mahakama baada ya kufutiwa mashtaka saba yaliyokuwa yakimkabili, ikiwemo uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka na kuongoza genge la uhalifu.

Mahakama imetoa uamuzi wa Lengai Ole Sabaya kulipa kiasi cha shilingi milioni 5 kama fidia kwa mwathirika na hapaswi kufanya kosa lolote la jinai kwa muda wa mwaka mmoja.

Sabaya ambaye mapema asubuhi ya leo alifika kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Moshi, kabla uamuzi wa kuachiwa haujatangazwa, kupitia Kifungu cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai namba 91 kifungu cha 1A, kesi yake ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 2022 ilifanyiwa marejeo kama upande wa mshtakiwa ulivyoomba.

Mawakili upande wa Jamhuri waliiomba mahakama kubadilisha mashtaka ya Lengai Ole Sabaya kutoka kuwa ya kesi ya Uhujumu Uchumi na kufungua kesi yenye Mashtaka ya Makosa ya Jinai baada ya Lengai Ole Sabaya kuomba kufanya mazungumzo nje ya mahakama na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Ombi hilo la Sabaya lilikubaliwa na Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Salome Mshasha baada ya Mawakili wa Lengai Ole Sabaya kuridhia na kufutwa kwa kesi yake namba 2 ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 2022.

Baada ya kuridhia hilo, kesi mpya aliyofunguliwa Sabaya ni kesi kesi ya Jinai Namba 31/2023 ambayo ndani yake kulikuwa na mashtaka mawili mapya dhidi yake, kosa la kwanza likiwa ni kuchukua madaraka ambayo siyo yake.

Imeelezwa kuwa Lengai Ole Sabaya na wenzake, Januari 19, 2021 katika eneo la Masama Mbosho wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, bila kibali walivamia duka la Alex Evarest SwaI na kuchukua mali na kuzizuia na kujipatia kaisi cha fedha shilingi milioni 50.

Kosa la pili ni kuzuia upatikanaji wa haki ambapo Januari 19, 2021 katika maeneo tofautitofauti katika Wilaya ya Hai na Tulia jijini Arusha na maeneo tofauti ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, walikula njama za kumfanya Alex Swai kuwa ametenda kosa la kukwepa kodi.

Baada ya kusomewa mashtaka, Sabaya alikiri kufanya makosa yote hayo mawili mbele ya hakimu Salome Mshasha.
Mahakama imeshindwa kazi, imemleta kwenye mahakama ya mtaani
 
Mbowe hakukutwa na hatia, alikuwa na kesi ya kujibu. Kwa maneno mengine alitakiwa ajitetee, na inawezekana baada ya ushahidi wa utetezi ingewezekana akaachiwa huru kwa kuonekana hana hatia.
Kwa hiyo, kesi ya Mbowe iliondolewa na mshitaki au mlalamikaji (jamhuri).
Huna unalojua, alishajitetea ndio hapo mahakama imamkuta na hatia. Alikua anasubiri hukumu
 
Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya, ambaye amekuwa akikabiliwa mashtaka saba ikiwemo uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka na kuongoza genge la uhalifu leo Aprili 05, 2023 ameachiliwa huru.

Taarifa zaidi zitakujia hapa hapa baadae.

Chanzo: Jambo TV

===

Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, leo April 5, 2023 ameachiliwa huru na mahakama baada ya kufutiwa mashtaka saba yaliyokuwa yakimkabili, ikiwemo uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka na kuongoza genge la uhalifu.

Mahakama imetoa uamuzi wa Lengai Ole Sabaya kulipa kiasi cha shilingi milioni 5 kama fidia kwa mwathirika na hapaswi kufanya kosa lolote la jinai kwa muda wa mwaka mmoja.

Sabaya ambaye mapema asubuhi ya leo alifika kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Moshi, kabla uamuzi wa kuachiwa haujatangazwa, kupitia Kifungu cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai namba 91 kifungu cha 1A, kesi yake ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 2022 ilifanyiwa marejeo kama upande wa mshtakiwa ulivyoomba.

Mawakili upande wa Jamhuri waliiomba mahakama kubadilisha mashtaka ya Lengai Ole Sabaya kutoka kuwa ya kesi ya Uhujumu Uchumi na kufungua kesi yenye Mashtaka ya Makosa ya Jinai baada ya Lengai Ole Sabaya kuomba kufanya mazungumzo nje ya mahakama na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Ombi hilo la Sabaya lilikubaliwa na Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Salome Mshasha baada ya Mawakili wa Lengai Ole Sabaya kuridhia na kufutwa kwa kesi yake namba 2 ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 2022.

Baada ya kuridhia hilo, kesi mpya aliyofunguliwa Sabaya ni kesi kesi ya Jinai Namba 31/2023 ambayo ndani yake kulikuwa na mashtaka mawili mapya dhidi yake, kosa la kwanza likiwa ni kuchukua madaraka ambayo siyo yake.

Imeelezwa kuwa Lengai Ole Sabaya na wenzake, Januari 19, 2021 katika eneo la Masama Mbosho wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, bila kibali walivamia duka la Alex Evarest SwaI na kuchukua mali na kuzizuia na kujipatia kaisi cha fedha shilingi milioni 50.

Kosa la pili ni kuzuia upatikanaji wa haki ambapo Januari 19, 2021 katika maeneo tofautitofauti katika Wilaya ya Hai na Tulia jijini Arusha na maeneo tofauti ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, walikula njama za kumfanya Alex Swai kuwa ametenda kosa la kukwepa kodi.

Baada ya kusomewa mashtaka, Sabaya alikiri kufanya makosa yote hayo mawili mbele ya hakimu Salome Mshasha.

Hongera kwake naamini atakuwa kajifunza!!! Lakini sheria inasemaje hapo kwenye kuachiwa? Maana tayari alihukumiwa.... na hii sio nzuri maana wafungwa wapo wengi kwann iwe ni msamaha ambao sio wa raisi kama tulivyozoea? Wanasheria naomba ufafanuzi wa hili.

Karibu mtaa bwana sabaya ila sasa uwe na utulivu.... mungu akikupa nafasi tena yakutumia taifa hili heshimu kila mtu na usiwe juu ya sheria
 
Huyo bagamoyo hana akili. Mbowe mwenyewe alitiwa hatiani

Hukumu ipi ya Mahakama Kuu ilimtia hatiani na kumpa kifungo jela, faini, kucharazwa viboko, kufanya kazi bila mshahara, kifungo cha nje au kulazimika kufuatiliwa kwa karibu awe na tabia njema kwa kipindi fulani mwenyekiti wa CHADEMA taifa Hon. Freeman Aikaeli Mbowe
 
Timu gaidi watanyooka tu wasiyempenda anakuja
Amekiri kuwa alikuwa anaendesha genge la washenzi na amekiri makosa yake na atalipa plea bargain so amejifunza mvinyo wa madaraka ni mbaya.
 
Agudishwe kwenye wilaya na kupewa stahiki zake zote na mishahara ikiwemo
Nyie ni majinga kabisa,huyu jambazi amekiri na amekubali kulipa plea bargains, maana yake ni mtu asiyeaminika na wala si mtu sahihi kupewa madaraka yoyote tena,cha kushangaza ni kuwa amekiri kupora milioni 50 halafu anaambiwa amlipe aliyempora shilingi milioni 5 tu,hizo 45 huyu mhanga anazipataje?
 
Back
Top Bottom