Lengai Ole Sabaya aachiwa Huru kwa sharti la kutofanya kosa la Jinai kwa kipindi cha mwaka mmoja
Mungu huyo atakuwa mjinga kupambania majangili, wezi, wauwaji.
Angeshawaua basi.

Unapokuwa unadhani kuwa Mungu hufanya kama afanyavyo binadamu ni kuwaza kinyume.

Neno wokovu halimhusu aliye katika usahihi. Wokovu na msamaha ni kwa aliye na dhambi yaani jangili, mwizi, muuaji na wsnaofanania hivyo.

Katika Mungu hakuna ujinga. Hakuna anayeweza kuzichunguza hekima na akili za Mungu.
 
Kwakweli leo nimefurahishwa na Serikali ya awamu ya sita.

Wapo makini sana na mambo yao.

Kudos.
IMG-20230406-WA0002.jpg
 
Sabaya amehukumiwa kifungo cha nje kwa mwaka. Yuko probation. Atakuwa huru baada ya mwaka mmoja.
Probation maana yake anapaswa kuacha tabia kushauri watu. (kujidai ana hekima na kuanza kushauri watu.)Aache tabia ya kugombanagombana na watu,muuza chipsi,bartender,.
Cautiously awakaribishe watu kumkosoa;itakuwa tragedy kama watu ishara zote kwamba anafanya mambo ambayo yatamrudisha gerezani halafu wakashindwa kumwambia .
Pia tukumbuke kwamba amekaa jela muda mrefu,ambapo Askari magereza wanamfanyanyia harsh Kama mfungwa yeyote wa kawaida(au kuliko mfungwa wa kawaida).
Probation is not quite freedom. The difference must be understood. Au sivyo watu wataingia hasara.
 
Angeshawaua basi.

Unapokuwa unadhani kuwa Mungu hufanya kama afanyavyo binadamu ni kuwaza kinyume.

Neno wokovu halimhusu aliye katika usahihi. Wokovu na msamaha ni kwa aliye na dhambi yaani jangili, mwizi, muuaji na wsnaofanania hivyo.

Katika Mungu hakuna ujinga. Hakuna anayeweza kuzichunguza hekima na akili za Mungu.
Asante
 
Wakuu naomba kufahamishwa makosa ya jinai ambayo mtu anaweza plea bargain,

Je ubakaji,mauaji na ujambazi pia vyaweza kuwa kwa plea bargain!?
 
Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya, ambaye amekuwa akikabiliwa mashtaka saba ikiwemo uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka na kuongoza genge la uhalifu leo Aprili 05, 2023 ameachiliwa huru.


Taarifa zaidi zitakujia hapa hapa baadae.

Chanzo: Jambo TV

===

Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, leo April 5, 2023 ameachiliwa huru na mahakama baada ya kufutiwa mashtaka saba yaliyokuwa yakimkabili, ikiwemo uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka na kuongoza genge la uhalifu.

Mahakama imetoa uamuzi wa Lengai Ole Sabaya kulipa kiasi cha shilingi milioni 5 kama fidia kwa mwathirika na hapaswi kufanya kosa lolote la jinai kwa muda wa mwaka mmoja.

Sabaya ambaye mapema asubuhi ya leo alifika kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Moshi, kabla uamuzi wa kuachiwa haujatangazwa, kupitia Kifungu cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai namba 91 kifungu cha 1A, kesi yake ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 2022 ilifanyiwa marejeo kama upande wa mshtakiwa ulivyoomba.

Mawakili upande wa Jamhuri waliiomba mahakama kubadilisha mashtaka ya Lengai Ole Sabaya kutoka kuwa ya kesi ya Uhujumu Uchumi na kufungua kesi yenye Mashtaka ya Makosa ya Jinai baada ya Lengai Ole Sabaya kuomba kufanya mazungumzo nje ya mahakama na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Ombi hilo la Sabaya lilikubaliwa na Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Salome Mshasha baada ya Mawakili wa Lengai Ole Sabaya kuridhia na kufutwa kwa kesi yake namba 2 ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 2022.

Baada ya kuridhia hilo, kesi mpya aliyofunguliwa Sabaya ni kesi kesi ya Jinai Namba 31/2023 ambayo ndani yake kulikuwa na mashtaka mawili mapya dhidi yake, kosa la kwanza likiwa ni kuchukua madaraka ambayo siyo yake.

Imeelezwa kuwa Lengai Ole Sabaya na wenzake, Januari 19, 2021 katika eneo la Masama Mbosho wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, bila kibali walivamia duka la Alex Evarest SwaI na kuchukua mali na kuzizuia na kujipatia kaisi cha fedha shilingi milioni 50.

Kosa la pili ni kuzuia upatikanaji wa haki ambapo Januari 19, 2021 katika maeneo tofautitofauti katika Wilaya ya Hai na Tulia jijini Arusha na maeneo tofauti ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, walikula njama za kumfanya Alex Swai kuwa ametenda kosa la kukwepa kodi.

Baada ya kusomewa mashtaka, Sabaya alikiri kufanya makosa yote hayo mawili mbele ya hakimu Salome Mshasha.
Sasa vipi kuhusu hizo hasara walizopoteza hao walalamikaji.

I hope walalamikaji wanaweza kukata rufaa kama hawajaridhika na uamuzi wa kesi
 
Mahakama haipo huru ndiyo maana ilimkuta na kesi ya kujibu Mbowe juhusu ugaidi wake lakini akaachiwa huru
Kukutwa na kesi ya kujibu sio kuhukumiwa Wewe kilaza
Mara ngapi watu hukutwa na kesi ya kujibu kisha kupangua mashtka?
Vipi mbona mbowe alihukumiwa kbs ile ya akwilina na akakata rufaa na kushinda sembuse procédure ya kukutwa na kesi ya kujibu?
 
Back
Top Bottom