MAANDIKO yanaema muuaji na mtesaji kwa watu wasio na hatia damu hizo zitawalilia mpaka kizazi cha nne, sababya ni kizazi cha kwanza cha utesaji akiridhi kwa baba yake.
Ole Sabaya kakulia Serengeti kwetu wakati baba yake Thomas Ole Sabaya akiwa DC wa Serengeti.
Babake alikuwa muuaji na mtu aloumiza watu wengi sana, so mtoto kafuata nyayo za babake! Babake aliwahi kuchoma nyumba za wananchi wa kijiji cha Nyamuma akidai wamejenga hifadhini na ni raia wa Kenya.
Baada ya kuzichoma huku wengine wakifia humo aliwasomba na magari kuwapeleka mpakani na kuwabwaga huko akidai si watanzania! Serikali ya Kenya ikawakataa na kuwapa masaa waondoke upande wa Kenya maana haiwatambui.
Alifikishwa Tume ya haki za binadamu ambapo alitiwa "hatiani" na kuamriwa serikali iwalipe fidia milioni 800 na kuwarejesha maeneo yao.
Tume ya Haki za Binadamu ikamfungulia mashtaka Mahakama Kuu lakini mpaka leo Jaji wa kusikiliza kesi hiyo hajapangwa! Imagine tangu utawala wa Mkapa mpaka leo? Akahamishiwa Songea akampiga makofi katibu tarafa kwa kushindwa kusimamia ujenzi wa sekondari za kata, katibu tarafa akamkaba zikapigwa ndo wacha wacha ya OCD ikaamua ugomvi!
Akafikishwa kamati ya maadili ya CCM akatiwa hatiani kwa kosa la kupigana hadharani, baadae Kikwete katika badilisha badilisha ya ma-DC akamtupia virago! Ikumbukwe kabla ya kuwa DC Serengeti alikuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arumeru ambako wananchi walimkataa wakaandamana wakachoma nyumba yake kwa kupandisha kodi ya maendeleo ( kichwa) kutoka 3000 mpaka 5000 bila kushirikisha mtu! Akajiuzulu, Sumaye akiwa Waziri Mkuu akampa pande la u-DC ( yeye na Sumaye wameoa mji mmoja