Wanajukwaa poleni kwa kumbukumbu ya kifo cha muasisi wa Taifa letu,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Bila shaka baada ya Hukumu ya Lengai Ole Sabaya kuhairishwa tarehe 1/10/2021 ilipangwa kwamba itatolewa leo. Hivyo tuelekeze masikio yetu katika viunga vya mahakama.
=======
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili leo Ijumaa Oktoba 15, 2021 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kusikiliza hukumu ya kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha.
Hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Amalia Mushi aliahirisha hukumu hiyo Oktoba Mosi, 2021 baada ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo, kutokamilisha kuandika hukumu hiyo.
Agosti 24 mwaka huu, Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu na Daniel Mbura walikamilisha kujitetea mahakamani hapo baada ya Jamhuri kukamilisha mashahidi 11 na vielelezo vinane.
Sabaya alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Juni 4, mwaka huu baada ya kukamatwa Mei 27 wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Chanzo: Mwananchi
UPDATE: SABAYA NA WENZAKE MIAKA 30 JELA
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wamehukumia na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.